04 July, 2015

Wayne Rooney ameendelea kufurahia siku chache za mwisho za likizo yake(Picha)

Rooney 5Wayne Rooney ameendelea kufurahia siku chache za mwisho za likizo yake kabla ya kujiunga na Manchester United siku ya Jumatatu asubuhi kwa ajili ya kuanza mazoezi kujiandaa kwa msimu ujao.
Nahodha huyo wa England amepigwa picha akiwa na familia yake wakila maisha na kufurahia huku akiendesha speed boat.
Rooney 3Rooney hatakuwa nyumbani kwa muda kwasababu kikosi hicho chini ya Van Gaal kitaelekea Marekani baadae mwezi huu kukamilisha ziara kabla ya kuanza kwa msimu (pre-season tour).
Rooney 4Mashetani wekundu watakipiga na Club America Julai 17 kabla ya kutimkia San Jose siku nne badae.
Rooney 7
Baada ya hapo, ratiba ya United itakuwa ngumu kwani watakipiga na mabingwa wa kombe la vilabu bingwa Ulaya klabu ya FC Barcelona na Paris Saint-Germain.
Rooney 6

Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...