02 September, 2016

Download Audio: Banana Zoro – Najihisi Nimechoka

Kazi mpya kutoka kwa mkongwe wa Muziki hapa nyumbani almaarufu kama Banana Zorro, inakwenda kwa jina la Najihisi Nimechoka. Bonyeza DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo kisha kumbuka kuwashirikisha wana kitaa.

DJ Khaled kusherehesha tuzo za Hip Hop za BET 2016

Mkuu wa vipindi wa BET,  Stephen Hill, alitoa tangazo hilo kupitia Snapchat na Khaled amekubali kwa moyo mmoja.
“They didnt want me to host the 2016 @bet Hip Hop Awards!! So guess what?? Im your host!! Tune in Oct 4th!! 8pm/7c #HipHopAwards #WeTheBest We have a lot of surprises!!!! Be ready! aliandika Khaled kwenye Instagram.

Pamoja na kuwa host,  Khaled anawania tuzo nane zikiwemo DJ of the Year, MVP of the Year, na Hustler of the Year.
Show hiyo itarekodiwa Sept. 17  huko Cobb Energy Performing Arts Centre, Atlanta,  lakini itarushwa kwenye runinga, Oct. 4.

Download Audio: Songa – Yule Jamaa

Kutoka Tamaduni Music,Sii mwingine muite Songa na hii ndio ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Yule Jamaa. Bofya Download hapo chini kuupakua wimbo huo. Kumbuka pia kuwashirikisha wana Kitaa.

Brazil, Argentina zashinda kufuzu kombe la dunia 2018

Mshambuliaji wa Brazil Neymer Jr
Michezo ya kuwania kuzufu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi mwaka 2018, kwa ukanda wa Amerika kusini, zimechezwa usiku wa kuamkia leo.

Wacheza samba timu ya taifa ya Brazil walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ecuador mshambuliaji Neymer junior, aliipatia timu yake bao la kwanza kwa penati beki wa kushoto wa Ecuador Walter Ayovi, akajifunga kisha kinda Gabriel Jesus, akihitimisha bao la ushindi kwa brazil.
Argentina nao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Urugway bao hilo likuwekwa kambani na mshambuliaji wao mahiri Lionel Messi.
Wekundu weupe wa Paraguay nao wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chile La Roja magoli ya Paraguay yakifungwa na Oscar Romero na beki Paulo da Silva huku bao pekee la Chile likifungwa na kiungo Arturo Erasmo Vidal.

01 September, 2016

Mashabiki wamtetea Chris Brown

Chris Brown
Mashabiki wanamtetea mwanamuziki Chris Brown ambaye anakabiliwa na shtaka la kushambulia baada ya kumtishia kwa bunduki mwanamke mmoja katika nyumba yake.
Wakili wake anadai kwamba madai hayo ni ya uongo na mashabiki wamekongomana katika mitandao ya kijamii kumuunga mkono.
Hii sio mara ya kwanza kwa Brown kukabiliwa na sheria ikiwemo visa kadhaa vya ghasia alivyotekeleza hapo awali.
Lakini ni kwa nini mashabiki wengi wanampenda?Mashabiki wanaomtetea Chris Brown
Chris Brown alimshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna mwaka 2009 ambapo ilikuwa habari kuu ya mwaka.
Maelezo ya shambulio hilo katika ripoti ya polisi pamoja na picha za majeraha ya Rihanna zilifichuliwa katika vyombo vya habari na kusababisha hisia kali.
Polisi waliitwa makazi ya Chris Brown na mwanamke aliyeomba msaada saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Malkia wa urembo, Baylee Curran ameambia gazeti la LA Times, kwamba mwanamuziki huyo alimwelekezea mtutu wa bunduki.
Hata hivyo walizuiwa kuingia na ilibidi wasubiri hadi kupata idhini ya jaji kabla kufanya msako wa kutafuta bunduki katika makaazi hayo.
Mwanamke huyo aliyewaita polisi baadaye aliambia vyombo vya habari kwamba walitofautiana na Brown kuhusu majohari.
Alisema alikuwa ameingia kwa Bw Brown akiwa na rafiki yake na mshirika wa kibiashara na alikuwa akiangalia mkufu wa thamani uliokuwa umevaliwa na mwanamume mmoja pale mwanamuziki huyo alipomkaripia na kumtaka aondoke mara moja akiwa amemwelekezea bunduki.

Acer yazindua laptop yenye kioo kilichojipinda

Acer yazindua laptopu yenye kioo kilichojipinda
Kampuni ya Acer imezindua laptopu ya kwanza ilio na kioo kilichojipinda.Acer inasema kuwa uvumbuzi huo utaiwezesha kucheza michezo ya video.
Televisheni kadhaa pia zimetumia uvumbuzi huo,lakini umezua mgawanyiko kwa kuwa una umuhimu na ubaya wake.
Kampuni hiyo ya Taiwan pia ilitangaza kwamba imefanikiwa kupata tekenolojia ya pet katika mkutano na wanahabari mjini Berlin. Acer yazindua laptopu yenye kioo kilichojipinda
Kampuni kadhaa za kielektroniki ikiwemo Samsung,Lenovo,DJI,Sony na Huawei zinatarajiwa kuzindua sura mpya ya laptopu zake katika maonyesho ya kiteknolojia ya Ifa katika mji mkuu wa Ujerumani wiki hii.
Laptopu hiyo ina kioo kikubwa ikilinganishwa na laptopu ya kawaida ya Acer,lakini ni umbo lake ambalo liliifanya kampuni hiyo kudai kuwa ya kwanza kuzinduliwa duniani.Runinga zilizojipinda CHANZO: BBC

Video: Tizama hapa Kionjo cha Video mpya ya Diamond Ft Neyo.

Msanii maarufu na anaye wika hapa bongo na Africa kwa wakati huu Diamond Plutnum a.k.a Simba, yupo nchini Marekani akishoot Video ya wimbo aliyo fanya na Mkali Neyo kutokea pande za Marekani. Tizama video hiyo hapo chini kisha kumbuka kuwashirikisha wana Kitaa.

Facebook yawapatia wateja fursa ya kutoa tahadhari

Huduma ya usalama facebook
Mtandao wa facebook umewapatia fursa wateja wake kutoa ishara ya tahadhari ya kiusalama iwapo watajipata katika hali hatari.
Kufikia sasa huduma hiyo ilikuwa inaweza kutolewa na wafanyikazi wa kampuni hiyo pekee.
Huduma hiyo ya usalama inawapatia watumiaji wa mtandao huo fursa ya kutoa ujumbe kwa marafiki ama familia zao kwamba wako salama kunapotokea janga la kibinaadamu mahala walipo.
Tetemeko la ardhi la hivi majuzi nchini Itali liliadhimisha mara 25 mwaka huu kwamba lilisababishwa.
Ujumbe huo wa usalama umewafikia watu bilioni moja mwaka 2016 pekee,kampuni hiyo imesema.
Katika kipindi cha miaka 2 iliopita kwa pamoja huduma hiyo ikutumika mara 11 pekee.
Timu ya facebook inayotoa huduma hiyo hutumia vigezo vitatu kubaini kuamua iwapo huduma hiyo inapaswa kutolewa:
  • Idadi ya watu walioathirika
  • Athari ya janga hilo
  • Na wakati wa tukio

T.I. Releases New Single “War Zone” Off Upcoming “Us or Else” EP

"CHARLOTTE, NC - MAY 20:  Rapper T.I. performs during the "New Era Cap Celebrates NASCAR All-Star Weekend" event on May 20, 2016 in Charlotte, North Carolina.  (Photo by Grant Halverson/Getty Images for New Era Cap)"

T.I. is gearing up his forthcoming EP “Us or Else,” and to build momentum for the project, the Atlanta rapper serves up a new single entitled “War Zone.”
Take a listen below, with the exclusive stream via TIDAL. “Us or Else” coming soon.

31 August, 2016

Video: Rayvanny-‘natafuta kiki’

Kutoka WCB, ni Rayvanny katuletea Video yake mpya Natafuta Kick, Audio imetengenezwa studio za Wasafi, na Video imetengenezwa Kwetu studio. Tizama Video hiyo hapo Chini kisha washirikishe wana Kitaa kadiri uwezavyo.
Bofya DOWNLOAD hapo chini kupakua Audio ya Natafuta Kick

New Music: DSM City RMX - Brian Lorenzo Ft. Godzilla

Brian Lorenzo ni msanii chipukizi anayeiwakilisha SinzaMusicGroup ambaye alikuwa nchini Botswana na sasa amerejea na huu ndio ujio wake. Bofya DOWNLOAD hapo chini Kuupakua wimbo Huo. Kumbuka pia kuwashirikisha wana Kitaa.

Video: Jeezy feat. 2 Chainz & Future – Magic City Monday

Jeezy turns “Magic City Monday” into a night out at the strip club in the video for his 2 Chainz and Future collaboration.

30 August, 2016

Rooney kustaafu soka la kimataifa ifikapo mwaka 2018

Wayne Rooney kustaafu soka ya kimataifa baada ya kombe la dunia la mwaka 2018
Mshambuliaji nyota na nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi.

Nyota huyo wa Manchester United alikuwa akizungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza toka kocha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza sam Allardyce athibitishe kuwa ataendelea kuwa nahodha.
Akihojiwa Rooney ambaye amefunga mabao 53 katika mechi 115 kwa Uingereza, amesema pindi Kombe la Dunia la Urusi litakapomalizika anadhani wakati wake wa kuaga soka la kimataifa utakuwa umefika.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.

Video: Ariana Grande Feat. Nicki Minaj – Side to Side

Fresh off her performance with Nicki Minaj at the VMAs, Ariana Grande unleashes the steamy video for “Side to Side.”
In the Hannah Lux Davis-directed clip, the pop princess echoes the fitness theme of her live rendition, setting it off by spinning with a team of dancers in a pink workout outfit and a hat that reads “Icon.” She hits the locker room for the second verse of the Caribbean-infused tune, dressing in a boxer’s warm-up robe, gracing the sauna with Minaj and Speedo-clad men as she doles out her verse. The video concludes with some wetness, as the dancers head to the showers for the finale..

New Music: Feza Kessy – Walete

waleteRadio presenter na Mwana Muziki Feza Kessy ameachia single mpya iitwayo WALETE, Bofya DOWNLOAD  hapo chini Kuupakua wimbo huo. Kumbuka pia kuwashirikisha wana kitaa kwa kadri uwezavyo.

Arsenal kumtoa Jack Wilshere kwa mkopo

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Jack Wilshere
Arsenal iko tayari kumtoa kwa mkopo kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere ili kupata fursa ya kujumuika katika kikosi cha kwanza cha timu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24,ambaye mchezo wake uliathirika kutokana na jeraha la mguu aliichezea Arsenal mara tatu pekee msimu uliopita baada ya kupata jeraha hilo.
Aliichezea Uingereza mara sita pekee msimu ulioipita ,ikiwemo mechi tatu katika mashindano ya Euro2016, lakini hakuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha mkufunzi Sam Allardyce wiki hii.
Arsenal ililipa pauni milioni 35 kumnunua mchezaji wa Switzerland Granit Xhaka msimu huu

Kampuni ya Apple kulipa kodi iliokwepa Ireland

Kampuni ya teknolojia ya Apple

Tume ya Ulaya inatarajiwa kuamrisha kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple kulipa mabilioni ya dola kama kodi iliyokwepa kulipa.
Hii inafuatia uchunguzi uliofanywa kubainisha makubaliano kuhusu kodi kati ya kampuni hiyo na serikali ya Ireland.
Tume ya Ulaya imewalalamikia mawaziri wa Ireland kwa kuipa Apple kandarasi inayoondoa kodi kwa makubaliano ya kutoa ajira kwa raia wa nchi hiyo.
Apple imesisitiza kwamba hakukua na muafaka maalum, na kwamba inalipa kodi kubwa nchini Marekani ambapo makao yake makuu yapo.
Kampuni ya Apple ni moja ya mashirika ya Marekani yanayolengwa na Tume ya Ulaya kutokana na mikataba yake ya kodi.

Mcheza filamu za vichekesho Gene Wilder afariki

Mcheza filamu Gene Wilder afariki dunia
Mcheza filamu za vichekesho nchini Marekani, Gene Wilder amefariki dunia akiwa na miaka 83.
Wilder amekua akiugua ugonjwa kwa kukosa fahamu{ Alzheimers}.
Aliwahi kucheza filamu maarufu ya , ''Willy Wonka-The Chocolate Factory''.


29 August, 2016

Hivi ndivyo ilivyokuwa red carpet ya MTV Video Music Awards 2016


Usiku wa August 28 ulikua ni usiku ambao tuzo kubwa ulimwenguni  MTV Video Music Awards zilikua zikitolewa. Hafla ya Tuzo hizo ilifanyika katika jiji la New York nchini Marekani. Wasanii wakubwa nchini marekani walihudhuria katika shereha za Utoaji wa tozo hizo. Baadhi wa wasanii walio tekelezea pande hizo ni Kanye West na Mkewe Kim-Kardashian, Meek-Mill na Mpenziwe Nick Minaj, Beyonce na Mwanawe Blue Eve na wengine kibao kama utakvyo waona hapo kwenye picha chini.
vma-arrivals-2016-1 vma-arrivals-2016-2 vma-arrivals-2016-3 vma-arrivals-2016-4 vma-arrivals-2016-5 vma-arrivals-2016-6 vma-arrivals-2016-7 vma-arrivals-2016-8 vma-arrivals-2016-9 vma-arrivals-2016-10 vma-arrivals-2016-11 vma-arrivals-2016-12 vma-arrivals-2016-13 vma-arrivals-2016-14 vma-arrivals-2016-15 vma-arrivals-2016-16 vma-arrivals-2016-17 vma-arrivals-2016-18 vma-arrivals-2016-19 vma-arrivals-2016-20 vma-arrivals-2016-21 vma-arrivals-2016-22 vma-arrivals-2016-23 vma-arrivals-2016-24 vma-arrivals-2016-25 vma-arrivals-2016-26 vma-arrivals-2016-27 vma-arrivals-2016-29

NA HIVI NDIVYO RIHANA ALIVYO PERFORM KATIKA JUKWAA LA MTV VIDEO MUSIC AWARDS.

video mpya ya Chris Brown ‘Grass Ain’t Greener’

Chriss Brown anazidi kufanya poa katika game maana kila baada ya ngoma hutoa ngoma kali zaidi. Ni mida mchache tuu umepita baada ya kuchia Audio ya ngoma hii  ‘Grass Ain’t Greener’, Chriss kaachia Video ya ngoma hii. Tizama hapo chini kisha washirikishe wana kitaaa.

Wanasayansi wanasema maji ya dunia yanahama

Ramani ya dunia
Wanasayansi wametumia picha za za setilaiti kuchunguza namna maji ya dunia yalivyohama kwa zaidi ya miaka 30. 

Walibaini kwamba kilo mita za mraba 115,000 za ardhini kwa sasa zimefunikwa na maji na kilomita 173,000 za maji zimefunikwa sasa na ardhi.
Ongezeko kubwa la maji limetokea katika eneo tambarare la betan , huku bahari ya Aral eneo kubwa la maji sasa limegeuka kuwa ardhi.
wanasayansi hao wanasema kuwa maeneo ya mwambao pia yamekuwa na mabadiliko makubwa .
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Deltares ya nchini Uholanzi umechapishwa na jarida la mabadiliko ya asili ya hali ya hewa. Tibetan Plateau
Watafiti walitathmini picha za setilaiti azilizochukuliwa na kituo cha wataalam wa masuala ya anga cha Nasa ,ambacho kimekuwa kikichunguza dunia kwa miongo kadhaa .
Waliweza kufuatilia mabadiliko ya sehemu ya juu ya dunia inayoweza kuonekana kwenye kipimo maalum .
Waliweza kubaini eneo pana ambalo wakati mmoja liliwahi kuwa ardhi ambalo sasa limekuwa na maji , eneo kubwa zaidi likiwa ni lile la maeneo tambarare yenye vilima ya Tibetambako barafu zilizoyeyuka zinasababisha maziwa makubwa .Korea kaskazini
Kuongezeka kwa idadi ya mabwawa pia kunaongeza kiwango cha maji, na kwa kutumia data za setilaiti , Timu hiyo ya wanasayansi iliweza kugundua shughuli za ujenzi ambazo hazikuripotiwa awali.
Dr Fedor Baart kutoka taasisi ya Deltares anasema : "Tulianza kuangalia kwenye maeneo ambayo hayakuwekwa kwenye ramani awali.
"Tulifahamu nchini Myanmar kwamba mabwawa kadhaa yalikuwa yanajengwa, lakini tuliweza kuona mengi . Na pia tuliweza kuona Korea kaskazini na tukaona mabwawa yanayojengwa huko karibu tu na mpaka wa Korea Kusini." bahari ya Aral
Vile vile watafiti waliweza kubaini kwamba hata maeneo makubwa ya maji yamebadilika kuwa ardhi sasa
Mabadiliko haya makubwa yalionekana katika bahari ya Aral Sea katika Asia ya kati.
Yale yaliyowahi wakati mmoja kuwa maziwa makubwa duniani kwa sasa karibu yanakauka kabisa baada ya wahandisi kuelekeza maji katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji.

CHANZO: BBC 

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...