Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

17 December, 2015

MH. ZITTO AFUNGUKA KUHUSU PROF. SOSPETER MUHONGO!

http://habarikwanza.com/wp-content/uploads/2015/12/zitto-663x445.jpg
Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe amefunguka na kuandika ujumbe mrefu unao muhusu Prof. Sospeter Muhongo kwenye ukurasa wake wa Facebook, kama ifuatavyo:
“Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪#‎TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC.
Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya ‘capacity charges’ kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo”

14 December, 2015

Godbless Lema ashinda Ubunge jimbo la Arusha

post-feature-imageMgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA katika Jimbo la Arusha,GODBLEES LEMA ameibuka mshindi na kutangazwa kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya siasa, LEMA amepata kura Elfu-68 na 848 kati ya kura Laki-1,Elfu-4 na 353 zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi,PHILEMON MOLLEL aliyepata kura Elfu-35 na 907.

14 October, 2015

Magufuli azungumzia samaki, Lowassa ageukia madini


Magufuli azungumzia samaki.

Mgombea wa urais kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema akiwa rais ataendelea kukamata meli za kigeni zinazovua samaki kwenye bahari ya Tanzania kinyume cha sheria kama alivyowahi kufanya akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Alisema hatakubali kuona samaki wa Tanzania wanageuzwa shamba la bibi, hivyo samaki watakaokamatwa kwenye meli zinazovua kiholela watagawiwa kwa wananchi kama kitoweo. Dk. Magufuli alisema hayo kwenye mikutano yake ya kampeni katika majimbo ya Mchinga na Kilwa Kusini mkoani Lindi na pia Kibiti mkoani Pwani.

Mgombea huyo alisema kuna watu wanamchonganisha na wavuvi kwa kudai kwamba akiingia madarakani atachoma nyavu zao na hawatakuwa na fursa za kuendesha shughuli zao.

Alisema yeye atakuwa rafiki mkubwa wa wavuvi wadogo na atawawezesha kwa mikopo na zana bora za uvuvi ili wavue kisasa na kuondokana na umaskini. Alisema atapambana na meli kubwa za uvuvi ambazo zimekuwa zikiiba samaki ambao ni mali ya Watanzania.

Sitaruhusu samaki walio kwenye bahari yetu wawe shamba la bibi. Wanaojijua kuwa wanaiba samaki wetu arobaini zao zimefika, mimi nitakamata na kugawa bure kwa wananchi, maana samaki ni mali yao…. kama niliweza kufanya hivyo nikiwa waziri wa kitoweo, siwezi kushindwa nikiwa rais,” alisema.

Lowassa ageukia madini

Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atahakikisha mikataba yote mibovu ya madini inapitiwa upya ili kujenga uchumi imara kwa manufaa ya taifa.
 
Lowassa ambaye alishaahidi kuifumua pia mikataba ya mafuta na gesi wakati akiwa mkoani Mtwara, aliyasema hayo jana kwenye mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni katika kata ya Katoro, Jimbo la Busanda mkoani Geita.
Iwapo nitashinda na kuwa rais, nitahakikisha mikataba mibovu ya madini na gesi inapitiwa tena ili kulinufaisha taifa,” alisema na kushangiliwa na maelfu ya watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
 
Mgombea huyo anayeungwa mkono pia na vyama vingine vinavyounda muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema mbali na kupitia mikataba ya madini na gesi, pia atahakikisha kuwa anaibadili Tanzania na kulikabili kwa ukamilifu tatizo la umaskini linalowakabili mamilioni ya wananchi. 
 
Kadhalika, alisema serikali atakayoiongoza itaboresha elimu na kilimo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakwamua Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini.
-Nipashe

24 August, 2015

Dk. John Pombe Magufuli ataja vipaombele 25 nakusema kuwa anayatambua matatizo ya watanzania

magufuli
Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Kimezindua rasmi Kampeni zake za Uchaguzi wa Mwaka 2015 huku Mgombea wake Dk. John Pombe Magufuli akisema kuwa anayatambua matatizo ya watanzania na kutaja vipaumbele 25 vikiwemo Mapambano dhidi ya Rushwa, Elimu na Ajira.
Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CCM Dk Magufuli ajinadi kushughulikia rushwa. Aahidi kujenga mahakama maalum ya wala rushwa asema serikali yake itakuwa ya viwanda, Lakini pia adai anayajua matataizo ya watanzania na kusema yeye ndiye mwenye kuweza kuleta mabadiliko.
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za mwana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo

21 August, 2015

Kikwete azijibu hoja za Ukawa

Tanzania's President KikweteRAIS Jakaya Kikwete, amesema Serikali yake iko imara ikijivunia utekelezwaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo na wote wanaosema nchi imemshinda, wanajidanganya kwa kufurahisha nafsi zao.

Alisema miezi michache kabla ya kumaliza muda wake, kumekuwa na uhuru mkubwa kwa watu kutoa maoni yao na wengine kupitiliza, lakini Serikali haipo tayari kuona mtu anatumia vibaya uhuru huo, kuleta machafuko na kuvuruga amani iliyopo nchini.

Hivi karibuni, baadhi ya viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), walimtuhumu Rais Kikwete na kudai nchi imemshinda kutokana na umaskini mkubwa wa Watanzania.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora akitumia fursa hiyo kuwaaga na kusisitiza kuwa, haki za binadamu na utawala bora vikiheshimiwa, vitasaidia kulinda amani na utulivu wa nchi.

"Maneno ya wapinzani wetu kisiasa hayanisumbui, anayesema nchi imenishinda mpuuzeni, haijanishinda na wanajidanganya wenyewe, mimi sina wasiwasi na hilo lakini hatutakubali kuona mtu anatumia uhuru huo kuleta migogoro ya kidini au ukabila," alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa, hata wale wanaosema nchi za Ulaya zina demokrasia ikiwemo Marekani, wajue hata huko sheria zao haziruhusu maandamano ya watu karibu na Ikulu, lakini hapa kwetu Tanzania, wanasiasa wanataka kuandamana Kariakoo wakiamini wana kundi kubwa la watu kumbe wengi wao ni vibaka wanaoiba bidhaa za wafanyabiashara.

"Ukitaka kuandamana, nenda Jangwani na ukiheshimu sheria ndio haki za binadamu zinapoheshimiwa, hata kama unayo haki lakini timiza wajibu upate haki," alifafanua Rais Kikwete.

Alisema katika utawala wowote, lazima kuwepo na uhuru na hilo kama halipo, watu wataidai kwa njia mbalimbali ili wapate haki yao, wakishindwa wanaweza kutumia bunduki kudai uhuru huo kwa kuwa msingi mkubwa wa amani ni haki.

Rais Kikwete alisema baadhi ya nchi zenye migogoro, chanzo kikubwa ni ukosefu wa haki; hivyo watu wanaweza kudai kwa mazingira ya kawaida na baadaye kupitia wanaharakati, nchi yoyote isiyo na haki za binadamu na utawala bora, si nchi tena bali ni msitu kwa sababu watu wanaweza kufanya lolote kwa wengine wasio na nguvu.

Migogoro ya ardhi

Akizungumzia migogoro ya ardhi, Rais Kikwete alisema lazima kuwepo mpango wa kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji ambao wanapaswa kupunguza mifugo yao.

Alisema migogoro mingi ya ardhi inachangiwa na baadhi ya viongozi ambao si waaminifu kwa kuuza kiwanja kimoja kwa watu wawili au watatu huku wananchi wakiwa hawana elimu ya kutosha juu ya masuala ya ardhi hali inayowafanya wenye uwezo kutumia fursa hiyo kuchukua ardhi yao.

"Tumeshughulikia migogoro mingi ya ardhi, jambo hili hatuwezi kuliacha kwani kuna viongozi ambao ndio chanzo, tangu niingie madarakani kila anayetaka ardhi kubwa lazima niidhinishe.

"Maombi yote yaliyofika kwangu, niliagiza lazima Mkuu wa Wilaya katika eneo husika, aitishe mkutano na wananchi ili awaambie na wakikubali nami ndio naidhinisha kwa kutia saini," alisema.

Mauaji ya albino

Rais Kikwete alionesha masikitiko yake juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kutokana na ukatili wanaofanyiwa ukiwemo wa kukata viungo vyao kwa ajili ya imani za kishirikina.

"Inauma sana, wakati mwingine unachukia hadi unaamua kulala lakini tangu niingine madarakani, sijawahi kutoa idhini ya kunyonga zaidi ya kufungwa maisha, jambo hili kwa nchi yetu bado hivyo ni kazi yenu
tume kutoa elimu juu ya masuala haya," alisema Rais Kikwete.

Aliishukuru tume hiyo kwa kufanya kazi nzuri ya kutoa elimu inayohusu masuala mbalimbali yakiwemo mauaji ya albino kwani huwezi kuwatenga kwa kuwapa majengo yao, barabara zao hivyo lazima nao waishi kama wengine ndio maana wanachanganywa hata shuleni.

Mwenyekiti wa tume

Mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga, alisema kipindi cha miaka 10, imepokea malalamiko 26,818 ya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

Alisema malalamiko 19,508 yalitolewa uamuzi na 7,310 yapo katika hatua za kupatiwa ufumbuzi ambapo hadi sasa kuna kesi 14 zilizopo mahakamani na tume inaendelea kufanya tafiti  mbalimbali katika
baadhi ya mikoa, kutembelea magerezani, kuangalia haki za wafungwa.

"Tunakushukuru sana Rais Kikwete, tunaviomba vyama vya siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jeshi la Polisi nchini watende haki ili kulinda haki za binadamu, utawala bora, kuendeleza amani iliyopo," alisema.

19 August, 2015

Fimbo ya Lowassa: Wajumbe 32 kumkabili

CCM kimepanga kuzindua kampeni zake za UchaguziChama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza Kamati ya Kampeni yenye wajumbe 32, wengi wao wakiwa ni wale waliowahi kuvaana na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa katika masuala tofauti.
Lowassa, Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, alijiondoa CCM mwishoni mwa mwezi uliopita na kujiunga na Chadema, ambayo ilimpa fursa ya kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, akiwakilisha vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD.
Tangu ahamie Chadema, Lowassa amekuwa akivuta wafuasi wengi kwenye shughuli za Ukawa, hali inayoashiria uwezekano wa kuwapo kwa upinzani mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Jana katika taarifa yake, CCM haikutoa maelezo mengi kuhusu kamati hiyo zaidi ya kutangaza kuwa itaongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana na kutaja majina ya wajumbe.
“Hii ni kamati ambayo itakuwa inafanya oparations za kila siku,” alisema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakati akitangaza kamati hiyo jana.
Kinana anajulikana kutokana na kazi aliyoifanya ya kuongoza kampeni kwa mafanikio, akifanikisha ushindi wa marais wawili mwaka 1995, wakati alipoongoza kampeni za Rais Benjamin Mkapa na 2005 wakati Rais Jakaya Kikwete akiingia Ikulu.
Licha ya Nape kutozungumzia majukumu ya kamati hiyo, mmoja wa wajumbe, January Makamba alisema wamejipanga vizuri na mwaka huu watafanya kampeni za kisasa.
“Tumejipanga na namna tunavyojipanga ni siri yetu, ni mambo ya ndani ambayo sisi wenyewe kwenye timu tunayafahamu na hatuwezi kutoa siri hizo kwa kuwa  ndizo silaha za maangamizi. Kwa kifupi tutashinda,” alisema naibu waziri huyo wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.
Makamba, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, alisema kampeni za CCM mwaka huu zitakuwa za kisasa zinazoendana na mazingira ya kisiasa ya msimu huu.
“Tumejitayarisha kushinda, juhudi zetu na ari yetu ni kushinda na kampeni zetu zitakuwa za kisasa zaidi,” alisema Makamba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo alitumia mfano wa mpira wa miguu kuelezea ukubwa wa kamati hiyo dhidi ya wapinzani.
“Timu hiyo ya kampeni ni sawa na kuileta Arsenal kuja kucheza na timu ya daraja la tatu. Kwa hiyo katika hali hiyo usiulize matokeo,” alisema Bulembo ambaye alikuwa mdau wa soka kabla ya kuingia kwenye siasa.
Kamati hiyo ina wajumbe ambao walitemwa kwenye mbio za urais ndani ya CCM, wajumbe wa Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, wajumbe ambao walikuwa kambi ya Lowassa alipokuwa kwenye mbio za urais ndani ya chama hicho, wajumbe ambao ni maarufu kwa kurusha vijembe dhidi ya wapinzani na wajumbe ambao walishaweka bayana uhasimu wao na mbunge huyo wa Monduli.
Nape alisema Kinana atasaidiwa na makamu wenyeviti wawili ambao ni Rajabu Luhwavi (Bara) na Vuai Ali Vuai (Zanzibar) ambao pia ni manaibu wake kwenye chama.
Wajumbe ambao ni wale waliotemwa kwenye mbio za urais ni Dk Asha-Rose Migiro, Samuel Sitta, Mwigulu Nchemba, Dk Harrison Mwakyembe, Makamba, Lazaro Nyalandu, Stephen Wasira, Bernard Membe na Makongoro Nyerere.
Pamoja na kutopitishwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, makada hao wamekuwa wakieleza kuwa hawawezi kuhama chama kama alivyofanya Lowassa na watakuwa wakionyesha kuwa wamevunja makundi kwa kushiriki kumpigia kampeni Dk Magufuli.
Kamati hiyo pia inamjumuisha Sitta, Spika wa Bunge la Tisa ambaye anajulikana kwa kuruhusu mijadala dhidi ya Serikali. Katika mijadala hiyo, Bunge lliliunda kamati iliyoongozwa na Dk Mwakyembe kuchunguza sakata la Richmond lililosababisha Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu.
Katika hotuba yake ya kujiuzulu, Lowassa alidai kuwa suala hilo lilipikwa na mahasimu wake wa kisiasa kwa sababu ya uwaziri mkuu.
Kundi jingine la wajumbe wa kamati hiyo linahusisha makada waliokuwa kambi ya Lowassa alipokuwa anawania urais kupitia CCM lakini hawakuhama naye. Wajumbe hao ni Christopher ole Sendeka, Sadifa Juma Khamis, Shamsi Vuai Nahodha na Sofia Simba, ambaye alipinga uamuzi wa Kamati Kuu wa kupitisha majina matano na kuacha mengine kinyume na katiba.
Wajumbe wengine ni Livingstone Lusinde, Abdallah Bulembo na Nape, ambao wanajulikana kwa kushambulia wapinzani. Lusinde alijipatia umaarufu katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, Machi 2012 alipoamua kutumia lugha chafu dhidi ya viongozi wakuu wa Chadema.
Tayari Kinana, Mwigulu, Nape, Bulembo na Wasira wameshanukuliwa wakirusha mashambulizi makali dhidi ya Lowassa na wote waliohama CCM kuwa ni makapi na mafuta machafu na kwamba Magufuli atashinda.
Vilevile, wamo makada waliowahi kutangaza hadharani kuwa mahasimu wa Lowassa tangu alipokuwa ndani ya CCM, akiwamo Anthony Diallo. Kundi jingine ni la makada vijana kama Ummy Mwalimu, Steven Masele na Pindi Chana.
Wakizungumzia uteuzi huo, baadhi ya wajumbe waliishukuru CCM kwa kuwaweka kwenye kamati hiyo huku wakitamba kwamba watahakikisha chama hicho kinaendelea kuongoza nchi.
Mwalimu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, alisema uteuzi wake ni jambo linaloonyesha kuwa anaaminika na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi kuhakikisha CCM inashinda.
“Kamati imejipanga,” alisema. “Kazi kubwa ni kuhakikisha Dk Magufuli anashinda na anaingia Ikulu kwa kuwa anauzika.
“Hatutishiwi na kitu, tunaamini katika kushinda na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha tunashinda kwa kupambana. Magufuli anauzika.”
Ahadi ya kufanya kazi kwa bidii pia ilitolewa na Mbunge wa Kiembesamaki, Waride Bakari Jabu ambaye alisema atajituma kwa asilimia 100 kuhakikisha CCM inashinda.
“Nimefurahi na nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote kuhakikisha kuwa tunashika dola Zanzibar na Bara,” alisema.
Wakati Jabu akiyasema hayo, Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Maua Daftari alitaka wananchi wawaunge mkono katika kazi hiyo.
“Hili jukumu si la kwanza, lakini ninachoweza kusema ni kuwa wananchi watuunge mkono ili tushinde,” alisema na kusisitiza kuwa watahakikisha kampeni zinafanyika kwa usalama na wala si kwa fujo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo alisema amepokea uteuzi huo na anachosubiri ni kukaa na kupanga kitakachofanyika.
Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), alisema hajapata taarifa rasmi kuhusu kuteuliwa kwake kwenye kamati hiyo.
Hata hivyo, alisema hiyo itakuwa ni mara yake ya pili kuwa kwenye kamati ya kampeni kwani aliwahi kufanya kazi kama hiyo alipokuwa NCCR-Mageuzi mwaka 1995. Alisema atazungumza zaidi kuhusu wajibu huo aliopewa pindi atakapopewa taarifa rasmi na Nape.
Wakati Diallo na Makongoro wakisubiri kikao, Nchemba, ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha, alitumia nafasi hiyo kumsifu Dk Magufuli.
“Sisi tunachokifanya ni kuweka njia tu ya kwa nini achaguliwe, kuwaambia Watanzania kwa nini anafaa, kwa kuwa awamu ya tano ni awamu ya kazi tu,” alisema.

....MWANANCHI

15 August, 2015

Zijue Sifa 10 za mgombea urais bora wa upinzani 2015

Lengo la uchambuzi huu ni kuwafanya Watanzania waanze kuwafahamu viongozi wao wajao na hata aina ya sifa wanazoweza kuwa nazo. Inawezekana kabisa kuwa wagombea waliochambuliwa asitokee mmoja wao kugombea au la, lakini hapa ninachoangalia ni kwamba tayari wananchi watakuwa “wamesogezwa karibu na ajenda ya uchaguzi” na hata akiletwa mgombea kutoka wapi, walau wananchi watakuwa wanajua wafanye uamuzi wa namna gani.

Ni jana tu nimemaliza uchambuzi wa watu wanaotajwa au waliojitokeza kugombea urais au wale ambao hawajajitangaza na hawana nia lakini jamii ndani na nje ya vyama vyao inawataja kama watu wenye sifa, uwezo na hata vigezo vya kuiongoza nchi yetu, kutoka vyama vya upinzani.

Lengo la uchambuzi huu ni kuwafanya Watanzania waanze kuwafahamu viongozi wao wajao na hata aina ya sifa wanazoweza kuwa nazo. Inawezekana kabisa kuwa wagombea waliochambuliwa asitokee mmoja wao kugombea au la, lakini hapa ninachoangalia ni kwamba tayari wananchi watakuwa “wamesogezwa karibu na ajenda ya uchaguzi” na hata akiletwa mgombea kutoka wapi, walau wananchi watakuwa wanajua wafanye uamuzi wa namna gani.

Leo nahitimisha hoja ya wagombea wa upinzani kwa kutoa sifa 10 za mgombea urais bora kutoka upinzani ambaye anaweza kupigiwa kura nyingi na Watanzania na hatimaye kuwa rais mpya wa Tanzania:

1. Mwenye umaarufu/umashuhuri na anayekubalika

Sifa hii ni muhimu, unapokuwa nje ya dola na nje ya chama tawala siyo rahisi kukishinda chama kinachoongoza Serikali. Umaarufu, umashuhuri na kukubalika ni mambo ya lazima. Ukitizama historia ya dunia na hata Afrika, vyama vikongwe vilipoondolewa madarakani waliofanya hivyo walikuwa wapinzani mashuhuri. Umuhimu wa sifa hii ni kuwa walau mtu maarufu na mashuhuri au anayekubalika, tayari amewekeza “mbegu” kwenye mioyo ya wananchi, wanaweza kumwamini ili waondoe hatima ya nchi mikononi mwa chama kilichowaongoza kwa miaka 50 na kuiweka mikononi mwa watu wapya. Wananchi wasipomwamini kiongozi wa upinzani anayekuja kwa sababu wanamkubali, ndipo huzuka ile kasumba ya “tupige kura kwenye zimwi likujualo”.

Hatari ya sifa hii

Umaarufu, umashuhuri na kukubalika vitaweza kufanya kazi kwa upinzani ikiwa mgombea husika hatatumia mwanya wa kukubalika kwake kujenga kiburi na hatimaye kuwasaliti wananchi. Ndiyo kusema kuwa vyama vya upinzani vitapaswa kuchagua mtu bora ambaye atatimiza matakwa ya wananchi “hata kama ni maarufu kuliko jua”.

2. Atakayebeba ajenda bora na kuifafanua vizuri

Kubeba ajenda bora na kuwa na uwezo wa kuifafanua kwa lugha rahisi ni jambo la muhimu kwa mtarajiwa kutoka upinzani. Moja kati ya makosa makubwa ya vyama vya upinzani katika bara la Afrika ni kutaka kubeba ajenda nyingi na kumrundikia mgombea urais, nakubali kuwa Afrika ina matatizo katika kila sekta ya maisha ya mwanadamu, lakini lazima iwe na vipaumbele vinavyowaumiza wananchi. Mgombea bora wa urais kutoka upinzani atapaswa kuwa na ajenda bora kuliko ile ya CCM na atapaswa kuwa na uwezo wa kuifafanua akaeleweka na mipango ya utekelezaji wake ikawa siyo ya “kusadikika”.

Hatari ya sifa hii

Ni pale inapotokea kuwa mgombea bora wa urais kutoka upinzani anazunguka nchi na ajenda iliyo bora kabisa lakini utekelezaji wake ukifanana au kushabihiana moja kwa moja na ule wa mgombea wa CCM. Wananchi wakiona upinzani unahubiri mipango na mbinu zilezile za CCM wataamua pia kuchagua “shetani wanayemjua” ili kujiweka kwenye mazingira ya usalama zaidi. Hivyo, ajenda ya mgombea bora wa upinzani na utekelezaji wake vinapaswa kuwa “vya kipekee”.

3. Mwenye uzoefu na rekodi ya uchapakazi

Uzoefu wa uongozi na uchapakazi unaofahamika ni jambo la msingi kwa mgombea bora wa urais kutoka upinzani. Vyama vya upinzani haviwezi kushinda uchaguzi na mgombea bora vitakayekuwa naye ikiwa mtu huyo si mzoefu na mchapakazi anayefahamika, mtu mwenye kujali wengine katika kazi lakini ambaye wananchi wataamini kuwa huyu atasimama pamoja na sisi usiku na mchana kuleta mabadiliko ya nchi.

Katika siasa, wananchi hupaswa kwanza kuamini na kisha hufanya uamuzi. Ikiwa mgombea bora wa urais wa upinzani hatakuwa na rekodi za uzoefu wa utumishi (katika taasisi za dini, serikali, vyama vya siasa na nyinginezo) si rahisi kumuuza kwa wananchi. Pia, ni lazima awe ni mtu ambaye rekodi zake zinatajwa kuwahi kuleta mabadiliko makubwa mahali alipofanya kazi.

Hatari ya sifa hii

Sifa hii hupaswa kuelezewa na kufahamika kwa wananchi kutoka kwa timu za kampeni za wagombea, wakati mwingine wapambe wa wagombea huchukua muda mwingi kutaja elimu ya mgombea wakidhani wananchi wanachagua elimu, kumbe elimu ni jambo moja tu kati ya sifa 100 za kiongozi. Ikiwa sifa hii muhimu haielezwi kwa uwazi kwa wananchi na hasa kwa kutaja rekodi bora za mgombea wa upinzani, wananchi wanaweza kumpa kisogo.

4. Mwenye uadilifu usio na shaka

Mgombea bora wa upinzani katika uchaguzi, anapaswa kuwa na uadilifu uliotukuka, usio na madoa wala shaka. Hapa nina maana kuwa, awe ni mtu ambaye uadilifu wake unatambulika kwa wananchi na kwa Taifa zima. Awe na rekodi za uadilifu kumshinda mgombea wa CCM, nina maana kuwa, wananchi wakimpima huyu wa upinzani na yule wa CCM – haraka haraka wasimame na kusema, “…naam! Huyu wa upinzani ni mwadilifu zaidi”. Marais wengi walioingia madarakani hasa hapa Afrika na hata Ulaya na Marekani kwa kuviondoa vyama vilivyokuwa madarakani, walipimwa kwa sifa hii.

Hatari ya sifa hii

Kigezo hiki hupata shida kubwa katika nchi ambazo uelewa wa wananchi vijijini na hata mjini si mkubwa. Wagombea waadilifu nao huweza kuchafuliwa ndani ya siku moja tu. Katika nchi ambayo si ajabu mgombea akawa hata na uwezo wa “kuhonga” chombo cha habari ili kimchafue mwenzake, sifa za mgombea bora zinaweza kuingizwa katika tope. Vyama vya upinzani vitapaswa kuwa na mfumo sahihi wa kuhakikisha uadilifu wa mgombea wake unazungumzwa kama ulivyo na haubadilishwi na propaganda za CCM.

5. Mwenye uwezo wa kusimamia, kuinua uchumi

Moja ya matatizo ambayo hayana dawa hapa Tanzania ni usimamizi wa uchumi. Nchi yetu inayumba kila mara na tunashindwa kutekeleza mipango yetu kwa sababu ya uchumi dhaifu, unaobadilika kila dakika na ambao hauna dira. Mgombea bora wa urais kutoka upinzani atapaswa kuwa na uwezo wa kusimamia na kuinua uchumi wa nchi. Awe ni mtu ambaye akisimama na kuweka ajenda ya uchumi mezani, Watanzania wote wanamwelewa, kwamba “naam, huyu ana uwezo wa kusimamia uchumi na kuondoa umaskini wa nchi”.

Hatari ya sifa hii

Ni pale mgombea wa upinzani atazunguka na mipango kabambe ya uchumi lakini yenye shaka kubwa kwenye utekelezaji au kuondoa umaskini, lakini pia ni pale mipango hiyo haitakuwa ya muda mfupi. Katika nchi maskini, wananchi wanahitaji matokeo haraka, vyama vya upinzani vitakuwa na jukumu la kuwa na mipango ya mfano ya muda mfupi ili kuwahakikishia wananchi kuwa ile ya muda mrefu pia itaweza kutekelezeka kwa wakati

6. Kuongoza mapambano dhidi ya rushwa

Rushwa ni adui wa haki na ni tatizo kubwa katika ukuaji wa uchumi wa Afrika. Mgombea bora wa urais kutoka upinzani atapaswa kuwa mtu wa kipekee ambaye moja ya sifa zake kuu ni mapambano dhidi ya rushwa, ndogo na kubwa. Awe ni Mtanzania ambaye si tu kwamba anapiga vita rushwa, bali anawachukia wala rushwa kama “kifo” na ni mtu ambaye yuko mbali kabisa na wala “rushwa”. Ndani ya CCM kwenyewe nadhani watatafuta mgombea wa namna hii ili kulinda hadhi yao, vyama vya upinzani vitakuwa na jukumu la kutafuta mpinga rushwa mahiri kuliko yule wa CCM, kwamba ukiwaweka pamoja hawa wawili – wananchi wenyewe waseme “…naam huyu wa upinzani anaweza mapambano haya zaidi kuliko huyu wa CCM”

Hatari ya sifa hii

Ikiwa upinzani utakuwa na mtu mashuhuri katika mapambano ya rushwa lakini ukawa hauna mipango ya kuhuisha haraka mifumo inayoleta mianya ya rushwa ndani ya nchi. Ndiyo kusema kuwa moja ya mipango ya upinzani inapaswa kuwa ni pamoja na kuweka wazi mifumo mipya ya usimamizi wa mapambano dhidi ya rushwa na hata kueleza watu watakaokuwa na sifa za kufanya kazi na mifumo hiyo.

7. Asiyependa kulipiza visasi na atakayefuata sheria

Jambo hili si dogo katika siasa. Rais ajaye kutoka upinzani anapaswa kuwa na sifa hii. Kwamba afahamike na kujulikana kwa kutokuwa na tabia ya kulipiza visasi lakini ambaye atazingatia matakwa ya sheria katika utendaji na awe na rekodi hizo. Unajua, kuna mambo ya kisheria ambayo ni lazima rais yeyote yule akiingia lazima ayafuate, mfano, wizi wa pesa za umma, hata kama umefanywa mwaka 1960 na ushahidi upo, lazima watuhumiwa wachukuliwe hatua leo, “jinai haifi wala kupotea”. Lakini kuna masuala mengine mengi tu ya kawaida ambayo yalikuwa yanatendwa na uongozi uliopita kwa sababu “za kipuuzi” na zisizo na maana, hayana haja ya kuwa kichwani kwa rais anayekuja.

Hatari ya sifa hii

Wananchi wengi huhofia masuala ya usalama iwapo vyama vipya vitaingia madarakani, hasa Afrika na moja ya masuala ambayo hupoteza usalama ni “kulipiza visasi”. Ndiyo maana vyama vya upinzani vinawajibika kuwa na mgombea ambaye hatalipiza visasi kwa makosa ya nyuma ya kiutendaji, ila atafanya hivyo kwa yale yaliyokosewa kwa makusudi na kwa kutofuata sheria.

8. Uwezo wa kubadilisha mfumo wa nchi

Tangu tumepata uhuru, nchi yetu imekuwa inasifika kwa kuwa na mifumo mibovu na isiyo na tija katika kila sekta. Hili ni janga kubwa. Rais bora ajaye kutoka upinzani ana kazi kubwa ya kubadilisha mfumo wa sasa wa nchi katika kila eneo ili mifumo ifanye kazi kwa mbio na kwa tija kubwa zaidi. Leo kuna watu walishtakiwa miaka ya 1990 na bado wako gerezani bila kuhukumiwa, kuna Kiwanda cha Sukari Kilombero na huko bei ya sukari ni kubwa kuliko Dar es Salaam. Haya ni matatizo makubwa ya kimfumo. Wananchi watahitaji kuwa na kiongozi ambaye atakuja kubadilisha kabisa mifumo ya utendaji kazi katika nchi. Kwa bahati nzuri, upinzani unaweza kuwa na hoja kama hii kwani vyama hivyo havikuwahi kuongoza Serikali na vimekuwa “waathirika” wa mfumo uliopo.

Hatari ya sifa hii

Ubadilishaji wa mifumo ukifanywa haraka na kwa pupa, utaingilia na kuvunja hata mifumo ambayo ilikuwa imeanza kukua na kukomaa kwa upande chanya. Ni jukumu la mgombea bora wa upinzani na timu zake kutambua mifumo yote ya utendaji katika sekta za jamii na kubainisha tangu wakati wa kampeni, ipi itavunjwa na ipi itarekebishwa ili kutoleta hofu yoyote kwa wapiga kura.

9. Msimamo unaoeleweka juu ya Katiba

Suala la katiba mpya ni ajenda muhimu katika uchaguzi wa mwaka huu. Mgombea bora wa upinzani atapaswa, yeye mwenyewe kuwa na busara za kutosha na msimamo thabiti juu ya masuala ya kikatiba na hasa mchakato wa Katiba Mpya. Naona kuna Watanzania wengi watapiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu kwa chama au mgombea ambaye atakuwa na misimamo ya wananchi katika suala la katiba. Hadi sasa hatuelewi kama katiba itapitishwa au la na hatuelewi kama wananchi wanaikubali au wanaikataa. Nani atatuvusha na kwa utaratibu gani? Majibu atakuwa nayo mgombea bora wa urais kutoka upinzani.

Hatari za sifa hii

Msimamo wowote ule wa mgombea urais wa upinzani katika jambo hili unaweza kuwa na athari chanya au hasi kulingana na namna wananchi wanavyolitazama suala la katiba. Kama mgombea huyu atakuwa na msimamo katika kuikataa Katiba Inayopendekezwa na kwamba ataanzisha mchakato mpya na ikiwa hayo ndiyo matakwa ya wananchi walio wengi, jambo hili peke yake litamuongezea kura za kutosha. La ikiwa kinyume chake, litakuwa na athari ya kiwango hichohicho bila kujali kama athari yenyewe ni chanya au hasi.

10. Uzoefu wa masuala ya kimataifa

Moja ya kazi kubwa za mkuu wa nchi ni kuliwakilisha Taifa katika masuala ya kimataifa. Rais bora kutoka upinzani hakwepi kuwa na rekodi imara ya masuala ya kimataifa, si kuishi Ulaya na Marekani, lakini kuwe na ushahidi wa kutosha kuwa amewahi kushiriki katika baadhi ya shughuli muhimu za kimataifa na kwamba huenda hata kimataifa yeye ni mtu bora. Nadhani CCM inaweza kuwa na mgombea mwenye sifa hii pia, ni jukumu la upinzani pia kuwa na mtu ambaye amejipanga vyema kimataifa na mambo aliyoyasimamia kimataifa pia yanajulikana, si lazima yawe ya kiserikali, yanaweza kuwa ya kijamii, ya kitaasisi au ya kitaaluma.

Hatari ya sifa hii

Sifa hii inaweza kufanywa moja ya propaganda za kuisaidia CCM, kwamba ndicho chama pekee chenye watu waliofanya kazi za kimataifa na wataifanya Tanzania ikubalike kimataifa. Vyama vya upinzani vitakuwa na jukumu la kupambana na propaganda hii kwa kuwa na mgombea ambaye tayari wananchi wanatambua kuwa ana uzoefu wa kimataifa usio na shaka ili kusiwe na tabu ya kuanza kumwelezea muda mrefu kwa wapigakura juu ya eneo hili.

HITIMISHO

Andiko hili peke yake haliwezi kujadili sifa zote muhimu za kiongozi bora kutoka vyama vya upinzani anayeweza kulivusha Taifa. Nimechokoza mjadala wa masuala muhimu tu. Tukumbuke kuwa, kazi ya kuongoza Serikali si nyepesi, inataka kujipanga kila idara na kuwathibitishia wapigakura kuwa mnaweza bila shaka. Tabia ya wapigakura huwa ni kutafuta namna gani watawaamini watu wanaowapa madaraka. Bahati nzuri vyama vya upinzani katika Taifa letu vimekwishafanya kazi ya kupigiwa mfano inayothibitisha, uzalendo, uadilifu, uzoefu uwajibikaji na utendaji kazi bora.

-Mwananchi

Lipumba Asisitiza kutokubaliana na uamuzi wa Ukawa kumsimamisha Lowassa kugombea urais

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda

Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.

Akihojiwa na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini, Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo.

Alipoulizwa jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.

“Wenzetu wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi, hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia malengo yao,” alisema.

Akizungumzia hatima yake kisiasa, licha ya kusema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF, alisema hatashiriki kufanya kampeni kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kuwa umoja huo umemsimamisha mwanachana wa CCM, Edward Lowassa.

“Kisiasa hatima yangu ni kama ya Mtanzania mwingine yeyote, Ukawa tuna mgombea kutoka CCM, amehama juzi tu, pia mle ndani ya Bunge la Katiba hakuunga mkongo Rasimu ya Katiba na ndiyo maana nikasema dhamira yangu inanisuta,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema wanachama wa CUF hawana sababu ya kuona kama amewaacha kwa kuwa bado yupo nchini.

Awali, akitangaza kujiuzulu, nguli huyo wa uchumi, alisema alifikia uamuzi huo kutokana na Ukawa kumkaribisha Lowassa kugombea urais kupitia umoja huo, hivyo dhamira yake inamsuta.

Membe afunguka kuanguka urais CCM

Tangu ashindwe kwenye kura hizo mapema mwezi uliopita, waziri huyo hakuwahi kuzungumzia kuanguka kwake, lakini jana aliweka bayana hisia zake.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amezungumzia kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM, akifananisha kushindwa kwake na kifo cha ghafla.

Akizungumza jana kwenye kongamano la Diaspora, Membe ambaye alivuka hatua ya awali ya mchujo akiwa mmoja wa watu watano ambao majina yao yalipelekwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, alishika nafasi ya mwisho kwenye kura akiwa nyuma ya Dk John Magufuli, Balozi Amina Salum Ali, Dk Asha-Rose Migiro na January Makamba.

Tangu ashindwe kwenye kura hizo mapema mwezi uliopita, waziri huyo hakuwahi kuzungumzia kuanguka kwake, lakini jana aliweka bayana hisia zake.

“Kwenye mpira unaweza kupata timu nzuri sana inacheza kwenye ligi, ikafanya vizuri,” alisema.

“Lakini mwishoni inapotoka droo (sare) na timu nyingine, timu zinakwenda kwenye penalti. Sasa inaweza kutokea ikafungwa penalti zote tano na timu nyingine ambayo wewe hukutegemea ikashinda vizuri tu.

“Kwenye lugha ya kimichezo, kile kitendo cha timu iliyocheza vizuri ikashindwa kwenye penalti, maana yake inakufa kifo kinachojulikana kama sudden death (kifo cha ghafla). Inapopata sudden death, huitegemei isimame na kueleza kilichotokea.”

Membe alikuwa anaonekana kuwa mmoja wa makada waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye urais, lakini alianguka vibaya kwenye kura za wajumbe wa Halmashauri Kuu.

Kuhusu kongamano hilo la siku tatu alilofungua kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, alisema licha ya kuwa anakaribia kuondoka madarakani atahakikisha anaendelea kupambana ili Watanzania wanaoishi nje wapate uraia wa nchi mbili.

“Ndipo tutakapopata maendeleo ya kweli ya wanadiaspora. Wanadiaspora watakuwa na kazi nzuri watakapokuwa nchi za nje na watakuwa wanaingiza mabilioni ya fedha nchini kama ilivyo kwa Kenya na Nigeria,” alisema.

Alisema hivi sasa Watanzania hao wanashindwa kusafirisha fedha zao kwa wingi nchini kwa sababu wengi wao ‘wamejilipua’ kwa hiyo wanazituma kinyemela, lakini pale watakapopata fedha wakiwa na uraia wa nchi mbili, wataweza kutuma bila kuficha.

“Natoka huku nikiendelea kuamini kwamba diaspora ya kweli ya Tanzania na isiyo na woga wowote ni pale watakapopata pesa za kufurahia uraia wa nchi mbili,” alisema.

14 August, 2015

Mrema asema UKAWA umepoteza mwelekeo

Mwenyekiti wa taifa wa TLP Augustine Mrema amewatahadharisha watanzania kuwa macho juu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umepoteza mwelekeo na kuyumba kisiasa na kudai kuwa hawafai kuingia ikulu na kuongoza nchi.
Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustino Lyatonga Mrema
Mrema ametoa tahadhari katika eneo la njiapanda baada ya kurejea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Moshi kuchukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo huku akisindikizwa na wafuasi wake.
Amesema, kitendo cha ukawa kumkashifu hadharani waziri aliyestaafu Mh
Edward Lowasa kuwa ni fisadi na baadaye kumpokea na kumteua kuwa mgombea wa urais ukawa imeonyesha udhaifu mkubwa na kwamba watanzania wa sasa si wakuburuzwa.
Mh. Mrema amesema kuwa haiwezekani mtu alieachwa na chama na kuonekana hafai kutokana na tuhuma za ufisadi kicha CHADEMA ndio wakaona anafaa kuwa mgombea huko ni kuonyesha kutokuwa na msimamo ndani ya hivyo ni vigumu kuwapa uongozi wa nchi.

11 August, 2015

Rais wa Tp Mazembe kugombea Urais Congo Drc.

Moise Katumbi, the governor of the Katanga region of the Democratic Republic of Congo and president of the TP Mazembe Lubumbashi football club, arrives for their African Champions league football match against Sewe Sport on March 23, 2014 at the Robert Champroux stadium in Abidjan. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Moise Katumbi, the governor of the Katanga region of the Democratic Republic of Congo and president of the TP Mazembe Lubumbashi football club, arrives for their African Champions league football match against Sewe Sport on March 23, 2014 at the Robert Champroux stadium in Abidjan. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Rais wa klabu ya Tp Englebert Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Moise Katumbi Chapwe ametajwa kuwa na mpango wa kuingia kwneye mbio za kuwania urais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo unaotarajia kufanyika mwakani.
Katumbi ambaye amekuwa gavana wa jimbo la Katanga kwa muda mrefu amekuwa pia rais wa klabu ya Tp Mazembe katika kipindi ambacho klabu hii imekuwa na mafanikio ikiwemo kutwaa ubingwa ligi ya mabingwa barani Afrika mara mbili mfululizo pamoja na kufika hatua ya fainali kwenye michuano ya klabu bingwa ya dunia .
Katumbi mwenyewe hajaweka wazi azma hii lakini vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo viko karibu na gavana huyu vimekuwa vikihabarisha kuwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa jamhuri ya kidemokrasi ya kongo Katumbi atatangaza azma yake wazi kwa kila mtu.
Chini ya Moise Katumbi Tp Mazembe imekuwa moja ya klabu bora barani Afrika.
Chini ya Moise Katumbi Tp Mazembe imekuwa moja ya klabu bora barani Afrika.
Gavana huyu ametajwa kuungwa mkono na mamlaka kubwa jijini Washington huku pia akiungwa mkono na wapinzani wakubwa wa rais Joseph Kabila huku yeye mwenyewe akionyesha kuwa na uhusiano mzuri na watu wa kambi ya upinzani.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa chini ya Joseph Kabila tangu mwaka 2011 wakati baba yake mzazi Laureant Desire Kabila alipouwawa na ameshinda uchaguzi katika miaka ya 2006 na 2011 huku kukiwa na shutuma za kuvurugwa kwa uchaguzi na ukosefu wa hali ya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Kikatiba Kabila hapaswi kugombea mwakani kwani anapaswa kukaa kwa mihula miwili pekee lakini rais huyo hadi sasa amekaa kimya na hajazungumza chochote hali ambayo imezua mijadala ya dhamira ya rais huyo kutaka kuongoza kwa Mhula wa tatu.

06 August, 2015

Je unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania? Huu ndio wasifu wake

post-feature-image
Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA), baada ya kusubiri kwa muda hatimaye umemtangaza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa mgombea wake wa urais.
Lowassa anagombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku vyama vingine vitatu vikimuunga mkono. Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.

Hatua ya mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Tanzania kuamua kujiunga na chama cha upinzani Chadema, ikiwa imebaki miezi mitatu tu kuelekea uchaguzi mkuu, kumebadilisha kabisa upepo wa kisiasa nchini Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.

Lowassa alikuwa Maziri Mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008 kabla ya kujiuzuLu wadhifa huo kufuatia sakata la kashfa ya rushwa iliyohusisha kampuni ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani Richmond Development Company LLC ya Houston Texas.

Hata hivyo wakati anatangaza kuhamia kwake Chadema, Lowassa alikanusha katu katu kuhusika kwa namna yoyote na kashfa hiyo na kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa ‘wakubwa’ walio juu yake. “Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa.

Kuhama kwake kunamfanya Lowassa kuwa ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa wa CCM kukihama chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mnamo mwaka 1992.

Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi kupigana wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79, Lowassa aliiambia hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu na nchi yake isingekuwa rahisi kubaki ndani ya CCM huku akiona chama hicho kimepoteza mwelekeo na sifa ya kuongoza nchi.

Lowassa amekimbilia upinzani baada jina lake kukatwa wakati alipoomba kuwa mgombea urais kupitia chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Wakati mchakato wa CCM wa kumtafuta mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa wagombea wote 42. Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia maelfu ya watu waliomuunga mkono.

Wakati chama cha CCM kilimtaka kila mgombea apate sahihi za wadhamini 450 lakini Lowassa alipata sahihi za wadhamini zaidi ya 700,000.
Hata hivyo mchujo wa chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa kwenye vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia’
“Nitakuwa mnafki nikisema bado nina imani na CCM. CCM niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia”, alisema, na kuongeza “kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi wakayatafute nje ya CCM”
Wakati sakala la Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya limsakama Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini. Lakini wakati chama hicho kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi nchini na kwamba hawawezi kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi kama Lowassa.
Wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja wa shughuli za serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘mzee wa maamuzi magumu’.
Moja ya mafanikio makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa ni mashuhuri pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule za kata ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi kupata nafasi shuleni.
Mtoto wa Mzee Ngoyai Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa ameanza harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere alimkatalia kushika nafasi hiyo. Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo
Ulipofika uchaguzi wa mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake alimnadi rafiki yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80.

20 July, 2015

Irene Uwoya Naye ajitosa kwenye Siasa......Achukua fomu ya Ubunge viti maalum Tabora

Msanii  wa  Bongo  movie, Irene  amechukua  fomu  ya  kugombea  ubunge  wa Viti  Maalum  kwa  tiketi  ya  CCM  huko  Tabora.
  Hizi  ni  picha  alizotutumia  wakati  akikabidhiwa  fomu  hiyo.


18 July, 2015

Ubunge CCM Kama Urais

wabunge+pixWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaowania kibali cha chama hicho ili wagombee ubunge, wamejitokeza kwa wingi katika baadhi ya majimbo na kufanya mchakato huo kuwa na mvuto wa aina yake, unaofanana na ule wa urais.

Jana ikiwa siku ya pili tu tangu kufunguliwa kwa pazia la uchukuaji fomu za kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini, idadi ya wanachama waliochukua fomu katika baadhi ya majimbo, imekuwa kubwa na kuelekea kulingana na wawania urais katika chama hicho, ambao walifikia 42. Jimbo jipya la Mbagala ndilo lilitia fora kwa kuwa na wasaka ubunge 17, waliolipa Sh laki moja na kuchukua fomu ya kuomba wanaCCM wapendekeze mmoja wao kuwania nafasi hiyo katika jimbo hilo.
Kwa mujibu wa Katibu Muenezi wa Wilaya ya Temeke, Rutami Masunu, mpaka jana siku ya pili ya utoaji fomu, waliojitokeza katika Jimbo hilo jipya ni wanachama hao 17.
Alitaja baadhi ya aliowakumbuka kuwa ni pamoja na Peter Nyalali, Richard Tambwe Hiza, Lucas Malegeli, Issa Mangungu, Mindi Dominck Haule, Ally Makwilo, Kivuma Msangi na wengine.
Katika Jimbo la Temeke waliojitokeza kuchukua fomu ni Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Abbas Mtemvu, Hamis Salim maarufu kama Chicago, Maimuna Chicago pamoja na Joseph Mhoha.
Masunu alisema kwa upande wa Jimbo la Kigamboni waliojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na Dk Faustine Ndugulile anayetetea nafasi yake pamoja na wanachama wengine watatu.
Kwa Wilaya ya Ilala, Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Ernest Charles aliliambia gazeti hili kuwa jumla ya waliojitokeza katika wilaya hiyo ni wanachama 26.
Aliwataja baadhi ya wanachama hao na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni Mussa Azzan Zungu, Mrisho Gambo, Waziri Kindamba (Ilala), Zahoro Lyasuka, Bona Kalua, Apruna Jaka, Siasa Chuma na Nicholaus, Baraka Omary, Christopher Japhet, Scholastica Kevela, Simon Kambe na Tunza Kanabe (Segerea).
Kwa jimbo la Ukonga ni Meya Jerry Slaa, Anthony Kalokola, Jacob Kasema, Hamza Mshindo, Fredrick Rwegasira, Ramesh Patel, Peter Kaseleko, John Machuta, Magesa Magesa, Amos Hangaya, Thomas Masegese, Edwin Moses na Ammo Mkuno.
Taarifa kutoka majimbo mengine ya Dar es Salaam, zilieleza kuwa katika Jimbo la Kinondoni walijitokeza wagombea tisa, Ubungo sita na jimbo jipya la Kibamba 10.
*Morogoro Kusini
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, lililopo katika Wilaya ya Morogoro Vijijini nalo lilijikuta likipata wasaka ubunge 12, akiwemo mbunge anayemaliza muda wake, Dk Lucy Nkya.
Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini, Shaibu Mtawa, alitaja baadhi yao aliowakumbuka kuwa ni Upendo Konyaki, Abdallah Mohammed, Athuman Maneno, Issa Dilunga na Semeni Mwinyimvua Kingalu.
Chilonwa, Morogoro
Mkoa mwingine ambao umepata wasaka ubunge wengi katika jimbo moja ni Dodoma, katika Jimbo la Chilonwa, lililokuwa likiongozwa na Hezekiah Chibulunje, ambaye alitangaza kutogombea tena ubunge. Waliochukua fomu mpaka jana mchana walifikia wagombea 12.
Miongoni mwa waliojitokeza kuwania jimbo hilo ni Godrick Ngoli, Paschal Ndolosi, Charles Ulanga, Peter Mlugu, Amos Kusakula na Chiuti Masagasi Jimbo la Mtera, mbunge anayemaliza muda wake, Livingstone Lusinde, naye amejikuta akikabiliwa na ushindani wa makada sita, akiwemo Charles Ulanga, Essau Mzuri na Dk Charles Msendekwa.

11 July, 2015

Hawa ndio watatu kwenye Urais wa Tanzania waliopitishwa na CCM

WATATU CCM 

 Updates kutoka Dodoma July 11 2015 ziko kila wakati, na zinazonifikia tu  na mimi nazisogeza kwako ili usipitwe, tuliifahamu TOP 5 ya Wagombea Urais wa CCM, tatu bora je?
Mitandaoni hii ina uzito tayari, majina matatu yaliyopitishwa na CCM kwenye wagombea Urais majina ni haya >>> John Pombe Magufuli, Asha-Rose Migiro na Amina Salum Ali.



10 July, 2015

Kama uliikosa hotuba nzima ya Rais Kikwete July 9 2015.

20101207 - Brussels , Belgium - European Development Days - The Energy Evolution - Mobilising Energy for Sustainable Development - H. E. Jakaya Mrisho Kikwete , President of the United Republic of Tanzania © European Union
Kama ulikosa time ya kumtazama au kumsikiliza Rais Kikwete kwenye hotuba yake akilivunja Bunge Dodoma June 9 2015 unaweza kuutumia muda wako kumsikiliza hapa chini.
Amezungumzia ishu nyingi sana ikiwemo Wasanii na alivyowasaidia, soka, miaka yake kumi ya uongozi na aliyoyafanya pamoja na mambo mengine

09 July, 2015

Hotuba ya Rais kikwete leo july 9

.Mh Dr Jakaya Kikwete ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amemaliza kulihutubia Bunge la kwa mara ya mwisho kwenye muhula wake wa urais muda mfupi uliopita.









Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

Kilichojadiliwa kwenye Kikao cha CCM Dodoma, Waziri Mkuu, Urais, Makundi.. Maneno ya Rais JK

Rais JK
Stori kuhusu Siasa zinapewa nafasi kubwa sana sasa hivi, Tanzania inaingia kwenye Uchaguzi Mkuu Mwezi October 2015… Tayari wapo waliotangaza Kugombea nafasi mbalimbali lakini macho ya wengi yako kwenye nafasi ya Urais, mpaka sasa kuna majina zaidi ya 35 ya watu waliotangaza Kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM.



 Hii ni Tweet ya Rais JK aliyoweka muda mfupi uliopita


Rais Kikwete yuko Dodoma, imenifikia hii Ripoti ya kilichoendelea jana wakati wa Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili cha CCM

Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

28 June, 2015

Steve Nyerere: Sijakurupuka Kugombea Ubunge

Steve  Nyerere: Sijakurupuka Kugombea Ubunge Staa wa Bongo Movies na aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye wiki iliyopita alitangaza niua yake ya kugombe ubunge mwaka huu wa uchaguzi amedai kua hajakurupuka kuutaka ubunge kupitia jimbo la Kinondoni na

01 June, 2015

Mbunge Augustino Mrema amelalamika tena kuhusu yaliyosemwa Jimboni kwake Vunjo !!

Voting
Ni zaidi ya mara mbili nasikia Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema akilalamika kuhusu kufanyiwa fitna na watu kwenye Jimbo lake la Vunjo, leo katika Kikao cha Bunge Dodoma amepewa nafasi tena.. kawasha kipaza sauti, kalalamika tena kuhusu anachofanyiwa Jimboni kwake.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...