Showing posts with label Cellebs. Show all posts
Showing posts with label Cellebs. Show all posts

26 October, 2016

Mkongo amvuruga Kadjanito, abadili na dini

Msanii wa Bongo fleva Khadija Said Maige maarufu kama Kadjanito amefunguka na kusema kuwa amepagawa na mapenzi ya Tresor Lisimo mchezaji wa mpira ambaye ndiye anataka kufunga naye ndoa tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka huu. 

Kadjanito kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na kituo cha Tv EATV anasema aliona amekaa peke yake kwa muda mrefu hivyo ameamua kuwa mke wa mtu ili na yeye awe mwanamke aliyekamilika sababu amempata mtu anayependana naye na mtu ambaye wanaelewana.

"Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina 'Inspire' watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu, najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki"

Ameendelea kusema "Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana. Aisee mimi nafunga ndoa ya Kikristu yaani jamaa nimemzimia mpaka nimeamua kumfuata katika imani yake, kiukweli ninamfuata" alisema Kadjanito

25 October, 2016

Sipendi 'bifu' na msanii yeyote - Joh Makini

Msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Joh Makini amesema katika vitu ambavyo hapendi kwenye kazi zake za kisanii ni kuwa na 'bifu' na msanii mwenzake katika tasnia ya sanaa nchini.
Makini ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva waliokusanyika kushuhudia program maalumu ya Kamatia Kitaa katika  kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
“Sipendi kuwa na bifu na msanii yeyote , mimi naamini katika muziki wangu na kuheshimu kila mmoja katika kazi yake” Amesema Makini
Aidha Makini ameongeza kuwa katika mambo ambayo humuumiza sana ni kuona kazi za wasanii zikiwa zimezagaa mtaani na kuuzwa bila wasanii kunufaika na chochote.
“Jambo hili inabidi serikali iingilie kati kwa sababu ugumu wa maisha mtaani umefanya vijana kuanza  kudurufu kazi zetu na kuziuza bila sisi kunufaika na chochote na jambo hili linatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha “ Amesema Joh Makini.

Pamoja na hayo Makini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwani kundi la weusi limejipanga vyema katika kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.

CHANZO: eatv.tv

Kelele zamuondoa Justin Bieber jukwaani kwa hasira

Justin Bieber aliondoka katika jukwaa la tamasha yake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati anapoimba.

Wakati wa tamasha zake tatu zilizopita katika mji huo ikiwa miongoni mwa ziara yake ya dunia nzima mwanamuziki huyo alisema : Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi munayonipa na nathamini ukarimu wenu.Lakini kelele munazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe.Tafadhali na ahsanteni.Sidhani ni muhimu ninapojaribu kusema kitu na nyinyi munapiga kelele.

Na mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele zao aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa,huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.
Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha yake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.

''Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho ,munajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.

22 October, 2016

Jay Mo amwagia misifa Juma Nature

Msanii Jay Mo amesema ukongwe wa Juma Nature kwenye game ya bongo fleva ni kitu cha kuthaminiwa sana kwani ameleta mchango mkubwa kwenye muziki huo mpaka kufikia hapa ulipo.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jay Mo amesema wataendelea kumheshimu Juma Nature kwani vitu ambavyo amevifanya, ndivyo vimesababisha wasanii kama kina Diamond kujulikana kimataifa.
“Tutamkumbuka kwa kufanya vitu ambavyo vimewafanya mpaka kina Diamond wakajulikana, muziki anaoimba Juma Nature ni ule muziki wa watu wa chini, amegusa maisha ya watanzania halisi, unajua sisi hata kama tulikuwa tunafanya muziki lakini haikuwa kama ya Juma Nature, kipindi hicho unaenda kweny show ya Juma Nature unakuta watu wanapanga foleni ndefu kukata tiketi, alikuwa anaweka kiingilio cha chini ili kila mtu aweze kuingia, hajajichukulia mi super star na kuvaa ukinondoni au u ilala, muziki wake ulikuwa umelalia maisha ya mtaa na watu wengi, alikuwa mjanja kutarget hawa watu wenye uwezo wa chini kimaisha”, alisema Jay Mo.

Jay Mo amesema kutokana na aina hiyo ya muziki wa Juma Nature, ndiyo ume'inspire' vijana wengi na kufuata nyayo zake, ikiwemo yeye mwenyewe na kuandika mistari ya wimbo wa stori 3 na Jua na mvua.

CHANZO: eatv.tv

21 October, 2016

Nguli wa muziki wa afro jazz Kenya Achieng Abura afariki dunia

Mwanamuziki nguli wa nyimbo za mtindo wa Afro Jazz kutoka Kenya Achieng Abura amefariki dunia.

Mwanamuziki huyo aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta (KNH) jijini Nairobi.
Lydia Achieng Abura, alipata umaarufu miaka ya 1990 kwa wimbo wa injili kwa jina I Believe.

Baadaye, alianza kukumbatia mitindo mingine ya uimbaji kama vile jazz.
Kwenye ujumbe katika ukurasa wa Facebook mapema mwezi huu, alikuwa amedokeza kwamba hakuwa buheri wa afya.

Alisema alikuwa amepoteza uzani wa kilo 50 katika kipindi cha miaka mitatu pekee, na madaktari walikuwa wamemshauri kuongeza uzani.
"Kutembea ni shida na ninaumwa kila pahali," aliandika
Kwenye mahojiano na gazeti la Business Daily mwezi Julai, alikuwa amesema alikabiliwa na matatizo ya kifedha kutokana na afya ya mwanawe wa kiume aliyehitaji kufanyiwa matibabu ambayo yangegharimu Sh4 milioni (dola 400,000 za Marekani).

"Niliandaa mchango lakini waliohudhuria walikuwa chini ya 10," aliambia gazeti hilo.

Abura alishinda tuzo ya muziki ya Kora mwaka 2004.
Alikuwa pia jaji katika shindano la kuwatafuta wanamuziki wenye vipaji la Tusker Project Fame ambalo liliwashirikisha vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki.

Wanamuziki wenzake, viongozi na mashabiki wameeleza kushangazwa kwao na kifo hicho na wamekuwa wakituma salamu za rambirambi mtandaoni.

Pete yangu siyo ya kishirikina - Young Killer

Msanii wa Hip Hop kutoka Mwanza Young Killer amesema pete yake aliyoivaa katika kidole chake ni urembo kama urembo mwingine kama miwani au hereni na siyo ya kishirikina au ya bahati kama watu wanavyoidhania.
Akiongea ndani ya Kipindi cha eNewz Msodoki amesema amekuwa ni mtu mwenye bahati kabla hata ya kuivaa pete hiyo au kuwa Young Killer hivyo pete hiyo haihusiki katika mafanikio yake “hofu ndo ugonjwa wako na kama mtu anafanya ushirikina ni imani yake imempelekea awe hivyo lakini kwa mimi sina imani na mambo ya kishirikina japokuwa najua kuwa yapo” alisema Msodoki.

Hata hivyo Msodoki alisema pamoja na mawazo ya watu kuhusisha pete yake na mambo ya kichawi lakini yeye hawezi kuivua itaendelea kukaa kidoleni kwake "... na kwa wale wanaoona tofauti waendelee tu kuwa na imani yao kwa kuwa ni vyema kutafuta haki yako bila kumkwaza mwenzako" alimalizia hivyo Young Killer

CHANZO: eatv.tv

Nikki wa Pili aonesha utofauti wake na Joh Makini

Rapa Nikki wa Pili ambaye hivi sasa bado anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Sweet Mangi' amefunguka na kusema kuwa kimuziki kati yake yeye na Joh Makini kwa mtazamo wake yeye anaona kuwa Joh Makini amemzidi mbali sana katika sanaa,
Kutokana na hilo, Nikki amewataka watu watambue kuwa Joh Makini ana kipaji kikubwa zaidi yake na uzoefu pia.

Nikki wa Pili alisema hayo kupitia kipindi cha 'Ngaz kwa Ngaz' na kusema kuwa Joh Makini yupo kwenye muziki muda mrefu, ana uzoefu mkubwa zaidi na amefanya mambo mengi ambayo yeye yamemrahisishia katika muziki.
"Kwanza Joh Makini ana experince kuliko mimi, halafu naweza kusema 'In terms of music' yeye ana ujaribu mkubwa kuliko mimi kwani amethubutu vitu vingi kuliko mimi ambavyo mimi kwangu baadaye nimevitumia kama 'Benefits'. Lakini Joh Makini Its all do respect, talent wise amenipita mbali kwa mimi ninavyotazama" alisema Nikki wa Pili
Chanzo: eatv.tv

20 October, 2016

Maua Sama: Nipo tayari kufanya kazi na label yenye mafanikio

Muimbaji wa Mahaba Niue, Maua Sama amedai kuwa anaweza kufanya kazi na label yoyote ile inayofanya vizuri na yenye mafanikio yanayoonekana.
Hata hivyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa THT na kwamba si rahisi kuhama, bali inawezekana kushirikiana na msanii yeyote nje ya uongozi wake.

Akiongea na kituo kimoja cha redio nchini, Maua amesema so far THT imemfikisha sehemu nzuri na haoni mapungufu yoyote kwenye muziki wake.
Kwa upande mwingine Maua amedai kuwa mashabiki wake watarajie kazi nzuri na mpya kutoka kwake.

Singeli imenipa nyumba na gari - Man Fongo

Msanii wa muziki wa Singeli nchini Man Fongo amefunguka na kusema anashangaa mafanikio makubwa ambayo ameyapata ndani ya muda mfupi kupitia muziki wa Singeli hususani kupitia kazi yake ya 'Hainaga ushemeji' ambayo imemtambulisha vyema kwa jamii.
Man Fongo
Man Fongo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV alisema kuwa muziki huo umebadilisha maisha yake ndani ya muda mfupi na sasa anaona maisha kwake ni kama mepesi akilinganisha na kipindi cha nyuma.
"Kupitia Singeli saizi nimepanga nyumba nzima Tabata, nina miliki gari yangu Toyota Altezza , unajua haya kwangu ni mafanikio yaliyokuja kwa muda mfupi sana kutoka kuishi gheto chumba kimoja mpaka sasa naishi nyumba nzima, familia saizi inaniangalia mimi hivyo naweza kusema Singeli ina neema sana kwangu na mafanikio kwangu yamekuja haraka mpaka nashangaa" alisema Man Fongo
 CHANZO:EATV.TV

Wapo watu wanatamani nifeli - Sam wa Ukweli

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye awali aliwahi kutamba na wimbo 'Sina Raha' amefunguka na kusema kwenye muziki wapo watu ambao wanatamani kuona akifeli katika muziki.
Sam wa Ukweli alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho Jana kilikuwa kinaruka moja kwa moja kutoka Ukonga Banana na kudai kuwa hakuamua yeye kukaa kimya kwenye muziki bali mkataba aliokuwa amesaini na uongozi wake wa awali ndiyo ulimpelekea yeye kukaa kimya kwani uongozi huo uliyumba kiuchumi na wakawa hawataki kumuachia kutokana na mkataba aliosaini.

"Wapo watu wanatamani mimi nifeli. Unajua hata ukimya wangu kwenye muziki ulitokana na 'Management' yangu ya pili, uongozi uliyumba kiuchumi na mkataba niliokuwa nimesaini ulikuwa unanizuia kufanya kazi na mtu mwingine na wao wakawa hawataki kuniachia hivyo ilinibidi nisubiri mpaka muda wa mkataba na wao uishe ili niwe huru na kazi, ndiyo kama hivi sasa nimemaliza muda huo ndiyo maana nimekuja na kazi yangu hii mpya 'Kisiki'" alisema Sam wa Ukweli

Mbali na hilo Sam wa Ukweli ameachia wimbo wake mpya ambao unafahamika kama 'Kisiki' ambao ndani yake amezungumzia mambo makuu matatu, Afya, Mapenzi na Pesa kwani yeye anasema hivi ni vitu vitatu vinavyoendana.

18 October, 2016

ROMA apangua skendo za watoto nje ya ndoa

Msanii Roma Mkatoliki amempa zawadi ya wimbo mtoto wake anayeitwa Ivan katika siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka minne, lakini kuna tetesi kuwa rapa huyo ana mtoto mwingine nje ya ndoa.
Ukiongelea wasanii ambao wanafanya vizuri kwa upande wa hip hop huwezi kuacha jina la Roma Mkatoliki. 

eNewz ilipiga story na Roma na alisema kuwa hizo skendo hazikuanza leo kwa sababu tayari aliwahi kupata skendo ya yeye na aliyekuwa mtangazaji wa kipind cha TV cha Nirvana, Lotus Kyamba kuwa mtoto aliyenaye ni wa kwake licha ya kwamba siyo kweli na kwamba yeye ana mtoto mmaja pekee ambaye ni Ivan

“Mimi kiukweli nina mtoto mmoja tu wa kiume ambaye ni Ivan na hizo story za mimi kuwa na mtoto nje zipo niliwahi kuambiwa nina mtoto na lotus kumbe siyo kweli na huwa sipendi kuziongelea sana kwa sababu mimi nina mke wangu na nina mtoto mmoja tu ambaye ni Ivan”

CHANZO: EATV.TV

WCB Wasafi wananihitaji ila sipo tayari - Z Anto

Msanii Z Anto ambaye aliwahi kutamba na ngoma kibao kali kama 'Binti kiziwi, Mpenzi jini, Kisiwa Cha Malavidavi amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji na kuhitaji kufanya naye kazi.
Z Anto
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo Z Anto amesema alipata ofa kujiunga na WCB Wasafi lakini yeye mwenyewe anadai anatamani kufanya kazi nje ya WCB Wasafi hivyo hawezi kujiunga nao.

"Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka saizi kuna 'label' nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati ya hizo. Maana nikibugi kuchagua 'label' ambayo inaweza kunisimamisha kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip Top Connection" alisema Z Anto 

Msanii huyo alitoa sababu kubwa yeye kutamani kufanya kazi nje ya Wasafi akidai tayari chini ya 'label' hiyo kuna mafahari hivyo hadhani kama mafahari wawili wanaweza kupatana au kwendana 

"Sisi ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya kazi sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo mengi mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi muda si mrefu' alisema Z Anto.

CHANZO: EATV.TV

16 October, 2016

Najiamini hata pasipostahili--Ney wa Mitego

Msanii Ney wa Mitego amesema maisha aliyokuwa anaishi yamemjengea ujasiri na kujiamini hata pasipostahili, na ndio kitu kikubwa kilichomfanya aweze kufanya muziki wa tofauti hata asipoungwa mkono na watu.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ney wa Mitego amesema maisha hayo yalimfanya asimuogope mtu yeyeite hata kama kamzidi umri, lakini ili mradi ameridhisha nafsi yake.

"Life style ambayo niliishi ilinijenga ujasiri wa kipuuzi ambao ninao, nilikuwa najiamini kupita maelezo, kabla sijaleta rap yangu ya maisha niliyokuwa naishi kwenye muziki, nilikuwaga mtu ambaye hata nikikaa tu maskani ukinikera mi nitakwambaia, uwe mkubwa, uwe mdogo uwe baba uwe mama, ntakwambia tu hapo hapo alafu roho yangu inakuwa safi, sitojali wewe utalipokea vipi, nilikuwa mtu wa kujichanganya sana", alisema Ney wa Mitego.
Ney wa Mitego aliendelea kusema kuwa kitendo hicho ndio kilichomsababisha awe anaandika nyimbo tofauti ambazo zinakuwa gumzo, hata asipopata suport kutoka kwa watu.

"Naweza nikafanya muziki wa tofauti na wenzangu, najua watu watashangaa, may be wanaweza wasisuport laiki acha nifanye, so niliamua, ndio maana wimbo wangu wa kwanza nilimzungumzia baba yangu, nilimzungumzia mama yangu ijapokuwa tafsiri yake ilikuwa tofauti, kwa wanawake ambao wanatupa watoto", alisema Ney wa Mitego.

CHANZO:EATV

13 October, 2016

Janet Jackson,athibitisha ni mja mzito akiwa miaka 50

Mwana-Muzik Janet Jackson amethibitisha rasmi kwamba anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50.

Ameliambia jarida la People: "Tunashukuru Mungu kwa baraka tuliyonayo", na akapigwa picha na tumbo lake linalozidi kuwa kubwa kudhihirisha uja uzito.
Fununu kuhusu uja uzito wake zilizuka Aprili alipojitokeza kuahirisha shughuli zake na tamasha la kimataifa 'Unbreakable' akisema anataka kupanga uzazi na mumewe Wissam al-Mana.

Ameonekana hivi karibuni London akinunua vitu katika duka la watoto.
Jarida la The People limenukuu duru iliyo karibu na familia ya Jackson aliyesema: "Ana furaha sana kuhusu uja uzito wake na anedelea vizuri sana. Ana raha kuhusu kila kitu."

Katika video iliowekwa kwenye Twitter mwezi April, amewaambia mashabiki wake kuwa ana ahirisha shughuli zake, kwasababu "kumekuwa na mabadiliko ya ghafla".Janet Jacket katika video ya Twitter
"Nilidhani ni muhimu mujue kwanza. Mimi na mumewangu tunapanga familia yetu," alisema, na kuongeza: "Tafadhali iwapo munaweza, jaribu muelewa kuwa ni muhimu nifanye hivi kwa sasa."
Aliendelea kusema: "Ni lazima nipumzike, ni agizo la daktari."

Janet Jackson ni nani:Janet Jackson (Mei 2010)
  • Janet Damita Jo Jackson alizaliwa Mei 16 1966 Gary, Indiana Marekani
  • Ni mdogo katika ndugu tisa na ni dadake muimbaji nyota Michael Jackson
  • Alitoa albamu yake ya kwanza Janet Jackson mnamo 1982
  • Ana albamu 11 ya hivi karibuni ikiwa ni Unbreakable, iliotolewa 2015
  • Ni mshindi mara 7 wa tuzo ya Grammy
  • Alianza taaluma yake kwa kushiriki katika kipindi cha televisheni The Jacksons mnamo 1976 na ameshiriki katika filamu kadhaa ikiwemo ya Tyler Perry 'Why Did I Get Married'
  • Muimbaji huyu ameolewa na mumewe wa tatu, Bilionea raia wa Qatari Wissam al-Mana, 2012.
Janet Jackson sio mwanamke maarufu wa kipekee kuzaa katika umri mkubwa.
Mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry amezaa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47, miaka mitatu iliyopita.
Mkewe John Travolta, Kelly Preston amezaa mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.

CHANZO:BBC

10 October, 2016

Mwanamuziki raia wa Rwanda aliye na hofu ya kurudi nyumbani

Corneille alipoteza familia yake yote mwaka 1994
Mwaka 1994 alikuwa na umri wa miaka 17 akiishi nchini Rwanda kwenye familia moja tajiri na ndoto yake ilikuwa ni ya kuwa muimbaji maarufu.

Lakini maisha ya Corneille Nyungura yalichukua mkondo mwingine kwa ghafla wakati yalitokea mauaji ya kimbari ya mwaka mwaka 1994 wakati takriban watu 800,000 wa kabila la watusi na wahutu wachache wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Wakati kundi la wauaji lilipowasili nyumbani kwao, Corneille alijificha nyuma ya sofa wakati familia yake yote ilichinjwa.Takriban watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda mwaka 1994
Sasa yeye ni raia wa Canada na mmoja wa wanamuziki bora zaidi wa RnB kutoka nchini Rwanda na amekuwa akiimba kwa miaka 20 iliyopita
Akijaribu kukubaliana kile kilichotokea nchini mwake mwaka 1994, Corneille anasema kuwa na uoga wa kurudi nyumbani kwao.

06 October, 2016

Rapper Fetty Wap Aionyesha mahakama Jeuri ya Pesa

Fetty Wap Rapper huyu kutokea pande za Unyamwezini a.ka.a kwa Obama kaamua Kuionyesha mahakama jeuri ya Fedha alizo nazo(Watoto wa mjini wanakuambia KAVIMBA).

The Patterson, NJ repper aliingia mahakamani na Kiasi cha $165k(sawa na Fedha ya Tanzania 3608797.5) ili kulipa Fine ya Kiasi cha $365 (sawa na Fedha ya Tanzania798309.75)  aliyo amriwa na mahakama Kulipa hapo jana Juma tano. 

Rapper huyo alilazimika kulipa Fine hiyo baada ya kubainika kwamba kavunja mashariti ya Driving license huko marekani.

20 September, 2016

Justin Bieber na mpenzi wake Sofia Richie waachana

Penzi la mwanamuziki maarufu ulimwemguni Justin Beiber na Sofia Richie ambaye ni mtoto wa mwanamuziki mkongwe nchini Marekani Lieonel Richie Limeingia wenda wazimu na hatimaye wawili hoa wamwagana-  Mtandao wa TMZ umeripoti.

Chanzo cha karibu na wapenzi ho kiliuambia mtando huo wa TMZ kwamba wawili ho hawakuawa teyari kuanza safari hiyo ya mapenzi licha ya kuonekana pamoja nchini Mexico kwenye Birthday ya Mwanadada Sofia Richie ambapo alikua akitimiza miaka 18, tangu hapo hawakuonekana tena hadharani na hawakuwa wakiongea tena pamoja.

Mwana dada Sofia Richie alionekana mnamo Siku ya Juma pili akiwa na marafiki zake wakila bata bila kuwaza chochote yani.


Snura: Mimi ni Malkia Wa uswazi

Mwanamuziki na Muigiazajia Snura amejipa cheo cha malkia wa Uswazi kwa madai  kwamba amekulia maisha ya Uswahilini, hata nyimbo anazo imba zina maudhui na mazingira ya Uswahilini, hivyo ni sahihi kujiita jina hilo.

"Mimi ni Malkia wa Uswazi, kwanza nmekulia huko, nimekaa huko, na hadi sasa nakaa huko na nyimbo zangu ni za uswazi, hivyo sioni kama kuna shida nikijiita Malkia wa Uswazi" -Alisema Snura.

Snura alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kufafanua kuwa hajali kwamba ataelewekaje,  kwa madai kwamba hata mashabiki  wanamuita kwa jina hilo na Pia ndiye Malikia wa Kisingeli kutokana na Muziki anao fanya.
Nyota huyo alisema hata kama yupo mwanamuziki mwenzake Shaa, ambae kwanzia hapo awali alikua akijiita jina hilo na kudai kwamba watu tuu wenyewe wanajua tu nani Malkia wa Uswazi.

19 September, 2016

Nguli wa muziki Afrika Kusini Mandoza afariki dunia

Mandoza

Nguli wa muziki nchini Afrika Kusini, Mduduzi Tshabalala, al-maarufu Mandoza, amefariki baada ya kuugua saratani kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 38.

Mandoza alisifika kwa albamu kadha za muziki aina ya Kwaito, aina ya muziki wa Afrika Kusini ambao hukaribiana sana na Hip Hop.MandozaNyimbo zake nyingi sana zilivuma, zikiwemo nyimbo kutoka albamu yake ya kwanza Nkalkatha. Familia ya Mandoza imesema mwanamuziki huyo aligunduliwa kuwa na saratani baada ya kuanza kuumwa na kichwa sana pamoja na kutatizwa na macho mwaka mmoja uliopita.

12 September, 2016

Ushahidi: Jaden Smith hajafa

Jaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.com Ingawaje mitandao inalazimisha kwamba nyota huyu kinda kutoka marekani amefariki, lakini taarifa hizo hazina ukweli wowote.
 Taarifa hizi zilianza kuzagaaa mitandaoni kwamba nyota huyu kajitoa uhai wake. Taarifa hizi zilipata Nguvu pale ambapo Jaden aliacha kupost chochote katika account za social media anazo miliki.
 Na good news ni kwamba jamaa kaonekana mtaani kiroho safi akiwa na Bibie Sara kama picha zifuatazo zinavyo onyesha.Jaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.comJaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.comJaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.com

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...