27 August, 2016

Music: Emanuel Austin na Rajson Melody – Mapenzi Digitali

Emanuel Austin ni mwalimu wa Dance huko nchini Uingereza,  amekua akifanya kazi na wasanii kadhaa wa hapa nyumbani pia kama vile Ben Paul na wasanii wengine. Na hii ni ngoma yake nyingine alomshirikisha Rajson Melody, wimbo unakwenda kwa jina la ‘Mapenzi Digitali.’ Mkono wa Producer Bako Rapper. 

Bofya DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.

VideoMPYA: Dogo Janja- Kidebe

Baada ya kufanya poa katika ngoma yake iliyopewa jina la My Life, Mkali kutoka Tip-Top conection, Janjaro safari hii katuletea video yake Mpya inayokwenda kwa jina la Kidebe, Video hii imeongozwa na Director Mkali Director Hanscana. Enjoy Kidebe.  
Bofya DOWNLOAD hapa chini Kupakua Audio ya Kidebe.

Tizama hapa Video mpya ya Msanii Mo Music- Ado Ado

Mwanamuziki anaye fanya poa katika game la Muziki wa bongo Flava Mo Music, anatukaribisha kuitizama video yake mpya Ado Ado. Tizama video hiyo hapo chini kisha washirikishe wana kitaa kwa kadiri uwezavyo. Enjoy Ado Ado.  
Pia unaweza Kuupakua wimbo huo hapa hapa kwa Kubonyeza DOWNLOAD hapo chini.

26 August, 2016

New Music: Sam Misago na Quick Rocka – Vyura na Madanga

Kazi mpya ya mtangazaji wa EATV na rapper Sam Misago akimshirikisha Quick Rocka. Inaitwa Vyura na Madanga na imetayarishwa na Luffa kwenye studio za Switch Records. Bofya DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.

Droo Europa League: Man Utd kukutana na Robin van Persie

Robin Van Persie
Manchester United watakutana na klabu anayochezea nyota wao wa zamani Robin Van Persie- Fenerbahce- pamoja na Feyenoord na Zorya Luhansk hatua ya makundi Europa League.
Klabu ya KRC Genk anayochezea Mtanzania Mbwana Ally Samatta imewekwa kundi F na Athletic Bilbao ya Uhispania, Rapid Vienna ya Austria na Unione Sportiva Sassuolo Calcio kwa ufupi Sassuolo ya Italia.
Southampton, klabu nyingine ya Ligi ya England inayocheza michuano hiyo, imepangwa kucheza dhidi ya Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer Sheva.
Dundalk ya Ireland nayo imepangwa na h Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar na Maccabi Tel-Aviv baada ya droo kufanywa Monaco.Zlatan Ibrahimovic na Robin van Persie

Meneja wa United Jose Mourinho amesema hawafahamu vyema wapinzani wao Zorya, kutoka Ukraine, lakini amefurahia kuwekwa kundi moja na Fenerbahce na Feyenoord.
"Sote twafahamu kwamba shindano hili si kama Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya lakini kuwa na Manchester United ikikutana na klabu zenye historia ndefu kama vile Fenerbahce na Feyenoord ni jambo zuri kwetu," amesema.

Droo kamili:

Kundi A: Man Utd, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk
Kundi B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana
Kundi C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala
Kundi D: Zenit St Petersburg, AZ Alkmaar, Maccabi Tel-Aviv, Dundalk
Kundi E: Plzen, Roma, Austria Vienna, FC Astra Giurgiu
Kundi F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassuolo
Kundi G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos
Kundi H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor
Kundi I: Schalke 04, FC Red Bull Salzburg, Krasnodar, Nice
Kundi J: Fiorentina, PAOK Salonika, Liberec, Qarabag
Kundi K: Inter Milan, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva
Kundi L: Villarreal, Steaua Bucharest, FC Zurich, Osmanlispor

CHANZO: BBC

Mr. Nice apata shavu la kupiga show 47, ataja wasanii wakubwa waliomuomba kolabo

nic  Mwanamuziki mkongwe katika Burudani ya muziki na mwanzilisha wa ‘Takeu style’, Lukas Mkenda almaarufu kama Mr. Nice, amepata shavu kutoka katika kampuni moja ya Nigeria ambayo imempatia mkali huyo shows 47 ambazo atazifanya katika County mbali mbali huko nchini Kenya ambapo ndipo alipo kwa sasa akiendesha shughuli zake za Muziki. 
“Niko huku Kenya,kuna kampuni ya Nigeria imenipa dili la kufanya tour kwenye county zote za Kenya, ziko 47″ Mr. Nice aliiambia Radion one.

Pia Mr.Nice amesema ana project mpya na Jaguar na Wyre ambazo zitatoke hivi karibuni,
“Pia nina project na wasanii wengine wa Kenya ambao wameniomba nifanye nao kazi,tuko na project na Jaguar na nyingine na Wyre kwa hiyo soon mambo yatakuwa mazuri
Kila la Kheri Bro!

Wizkid kuungana na Davido Sony Music Worldwide

Mwanamuziki maarufu Nigeria na Africa kwa ujumla Wizkid yuko mbioni kutangazwa msanii mpya wa Sony Music Worldwide, kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Soundcity.Kituo hicho kimeripoti kuwa muimbaji huyo ataungana na Davido kwenye roaster ya label hiyo kubwa.
“Dili la Wizkid na Sony limekamilika. Habari itatoka hivi karibuni. Meneja wake Sunday Are ametuelezea kuwa hili litazungumzwa hivi karibuni,” kilisema chanzo.
Umaarufu wa Wizkid umeongezeka maradafu mwaka huu baada ya kushirikishwa na Drake kwenye wimbo One Dance ulioshika namba moja kwenye chati za Billboard Hot 100.

Music: Download wimbo mpya wa Juma Kakere- 'Shangwe ya harusi" -

Nguli wa nyimbo za Dansi aliyewahi kutamba na wimbo "Pole Kwa Safari" msanii Juma Kakere amedondosha ngoma mpya inayokwenda kwa jina la "Shangwe Ya Harusi". Bonyeza DOWNLOAD hapo chini kuupakua waimbo huo.

Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mwanasoka bora Ulaya


3795021500000578-3758562-image-a-16_1472147165310

Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa Ulaya baada ya kuwashinda wachezaji wengine wawili ambao wote wanatokea katika timu za jiji la Madrid nchini Hispania tuzo hizo zilitolewa Nchini France katika mji wa Monaco.3795011900000578-3758562-image-a-31_1472147265986
Katika Kura zilizopigwa na waandishi 55 wanachama wa UEFA katika Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2015/2016 matokeo yamekuwa hivi
Cristiano Ronaldo – 40
Antoine Griezmann – 8
Gareth Bale – 7
Mshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya Norway Ada Hegerber ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa upande wa Wanawake 2015/2016
CquGSTEWIAACxnY
Ada Hegerberg

Download new music; Man Fongo " Nani bado sijamtaja"

Baada ya kufanya vizuri kwenye single iitwayo ‘Hainaga Ushemeji’, time hii ametuletea hii single mpya ‘Kibaka’ imetayarishwa na producer Mensen Selekta, Bofya DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.. pia kumbuka kuwashirikisha wana kitaa.

Video: 2Baba Ft. Sauti Sol – Oya Come Make We Go

It’s a pan-african affair as West Africa links up with East Africa. 2Baba calls on the uber-talented Kenyan ensemble – Sauti Sol for “Oya Come Make We Go”. Enjoy the video, Share it to our friends as much as you can.

Samatta afunga na kusaidia klabu yake Genk kufuzu Europa League

Samatta

Mchezaji wa kitamataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Hii ni baada ya klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla wa 4-2 mechi ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.

Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa Alhamisi jioni.
Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.
Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.

Samatta pia alioneshwa kadi ya manjano dakika ya 69.
Droo ya hatua ya makundi itafanywa mjini Monaco baadaye leo Ijumaa mwendo wa saa tisa saa za Afrika Mashariki.

23 August, 2016

Rick Ross’ “Port of Miami 10th Year Anniversary Trailer

Rick Ross  
Rapper na nguli wa Hip-hop Marekan Rick Ross anatengeneza official Port of Miami behind-the-scenes trailer itakayo onekana kwenye mtandao maarufu wa Burudani TIDAL(Tidal.com/RICKROSS).

Mtandao huo utaonyesha moja kwa moja(live-stream) perfomance maalumu kutoka kwa boss huyo wa May-bach Music Group Rick Ross huko Port of Miami in Miami ifikapo Junatatu , August 29th.

Unaweza kuingalia trailer  hiyo hapa >>> BOFYA HAPA<<<

22 August, 2016

Semenya,Mo Farah na Brazil wawika Rio

Caster Semenya ashinda dhahabu

Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amejishindia dhahabu katika mbio za mita 800 .
Franchine Niyonsaba amechukua nafasi ya pili na kujishindia medali ya fedha huku mkenya Margeret Nyairera Wambui akichukua medali ya shaba .

Semenya alivunja rekodi ya taifa lake katika mbio hizo na kuweza kushinda kwa dakika moja dakika 55 na sekunde 28.
Mohammed farah

Mwanariadha huyo ambaye alizua utata mwaka 2012 alipofanyiwa ukaguzi wa kijinsia alijishindia fedha mwaka huo.
''Ndoto ya mwanariadha yoyote ni kushinda dhahabu hususan katika mbio za Olimpiki'',alisema Semenya.
Na Marekani imeshinda mbio za mita 400 mara 4 kupokezana vijiti kwa wanawake na kujinyakulia nishani ya dhahabu, baada ya kutimka kwa muda wa Sekunde 19.06.

Kina dada hao wameandikisha ushindi mara sita mtawalia katika mashindano ya Olimpiki.
Kikosi cha kina dada kutoka Jamaica kilizoa fedha, ilhali Uingereza ikajipatia nishani ya shaba.
Kikosi cha wanaume pia cha Marekani kimeshinda mbio za mita mia nne mara nne kupokezana vijiti.
Naye mwanariadha wa Uingereza Mohammed Farrah, ameandikisha ushindi mara mbili katika mbio ndefu za mita elfu kumi na elfu tano mtawalia, huku akizoa dhahabu baada ya kuwapiku wenzake kwa kasi huko Rio de Janeiro. 

Miaka minne iliyopita alizoa dhahabu mbili katika mbio hizo hizo, katika mashindano ya Olimpiki Jijini London.

Wakati huo huo, timu ya soka ya wenyeji Brazil, inafurahia nishani yake ya kwanza ya dhahabu, katika soka.
Mabingwa hao mara tano wa kombe la dunia waliwanyuka Wajerumani katika mikwaju ya penalti, baada ya mechi hiyo kumalizikia bao moja kwa moja, hata baada ya kipindi cha ziada

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...