Watch the Trailer
08 October, 2016
Week-End Movie: The Birth of a Nation
Watch the Trailer
Ureno yaichapa Andorra 6-0, Ronaldo aweka Rekodi mpya
Cristiano Ronaldo amefunga magoli manne wakati Ureno wakitoa kichapo
cha magoli 6-0 dhidi ya Andorra kwenye mchezo wa kuwania kufuzu
kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Ronaldo alifunga magoli mawili moja kwa kichwa jingine kwa mguu ndani ya dakika nne za kipindi cha kwanza na kuwaweka mbele mabingwa wa taji la Euro 2016.
Joao Cancelo aliongeza bao la tatu kisha Ronaldo akafunga goli la tatu kukamilisha hat-trick yake katika mchezo huo.
Ronaldo alirejea kambani kwa mara nyingine kufunga goli lake la nne katika mchezo huo huku likiwa ni goli la tano kwa Ureno kabla ya Andre Silva kuhitimisha party ya magoli dhidi ya Andorra ambao walipoteza wachezaji wao wawili kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu.
Ureno kwa sasa wapo nafasi ya tatu katika Kundi B wakiwa wamepoteza mchezo dhidi ya vinara wa kundi hilo Switzerland ambao wameifunga Hungury 3-2 kwenye mchezo wao wa Ijumaa.
Hat-trick hiyo inamfanya Ronaldo aweke rekodi ya kufikisha jumla ya hat-trick 42 katika maisha yake yote ya soka.
Ronaldo alipata majeraha kwenye mchezo wa fainali ya Euro 2016, mchezo dhidi ya Andorra ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza wa kimataifa tangu fainali ya Euro ambapo Ureno ilishinda 1-0 dhidi ya Ufaransa.

Video: Snura – Chura
Msanii Snura hatimaye ameachia video yake mpya ya wimbo wa “Chura”, baada ya kufunguliwa kwa wimbo huo.
06 October, 2016
Rapper Fetty Wap Aionyesha mahakama Jeuri ya Pesa
Rapper huyu kutokea pande za Unyamwezini a.ka.a kwa Obama kaamua Kuionyesha mahakama jeuri ya Fedha alizo nazo(Watoto wa mjini wanakuambia KAVIMBA).
The Patterson, NJ repper aliingia mahakamani na Kiasi cha $165k(sawa na Fedha ya Tanzania 3608797.5) ili kulipa Fine ya Kiasi cha $365 (sawa na Fedha ya Tanzania798309.75) aliyo amriwa na mahakama Kulipa hapo jana Juma tano.
Rapper huyo alilazimika kulipa Fine hiyo baada ya kubainika kwamba kavunja mashariti ya Driving license huko marekani.

Patashika Dimbani leo Timu mbalimbali kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia
Leo timu za nchi mbalimbali zitaingia uwanjani kukipiga kusaka tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Moldova - Serbia.
Kosovo - Croatia.
Jamuhuri ya Ireland - Georgia.
Liechtenstein - Albania.
Macedonia - Israel.
Iceland - Finland.
Turkey - Ukraine.
Huku mchezo mkali ukiwa kati ya mabingwa wa mwaka 2006 Italia dhidi ya mabingwa wa 2010 Hispania.
Samsung Galaxy Note 7 yalipuka kwenye Ndege.
Simu ya kampuni ya Samsung aina ya
Galaxy Note 7, ambayo ilikuwa imethibitishwa na kampuni hiyo kuwa
ilikuwa salama, imelipuka kwenye ndege nchini Marekani.
Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege moja yake, iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland, waliondolewa kwenye ndege kwa dharura kabla ya ndege hiyo kupaa Jumatano.
Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu za Note 7 kuzirejesha kwa kampuni hiyo baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo kwenye betri zake.
Samsung imesema bado inachunguza kisa hicho cha Jumatano.
"Tunashirikiana na maafisa wa serikali na maafisa wa shirika la Southwest kupata simu hiyo na kuthibitisha chanzo (cha moto huo)," kampuni hiyo imesema kupitia taarifa.
Msemaji mmoja wa shirika la Southwest Airlines amemabia BBC: "Abiria mmoja alitufahamisha kuhusu moto uliokuwa unafuka kutoka kwa simu. Abiria wote na wahudumu wa ndege waliondolewa salama kutoka kwenye ndege."Mmiliki wa simu hiyo Brian Green, akizungumza na Jordan Golson wa shirika la The Verge, amesema alinunua simu hiyo tarehe 21 Septemba.Amesema simu hiyo ilikuwa na alama ya mraba ya rangi nyeusi kwenye pakiti yake, alama ambayo iliongezwa na Samsung kutofautisha kati ya simu zilizokuwa zimeuzwa awali ambazo zilidaiwa kutokuwa salama na simu mpya zilizokuwa zimechunguzwa.
Audio Mpya: Jux ft Vanessa--JUU
Umefikia muda wa kuikata kiu yako uliyoitunza kwa muda mrefu. Wapendanao Vanessa
Mdee na Jux wameachia bonge moja la kolabo linalokwenda kwa jina la "Juu" ambalo
limeachiwa kwa mara ya kwanza kabisa kwenye Mkito. Ngoma hii imetengenezwa na
Lufa- Switch Records.
Huu umekuwa mwaka mzuri kwa wawili hawa. Wamepiga tour za kutosha nchini kwenye Fiesta huku wimbo wa "Wivu" wa Jux ukiendelea kusumbua kwenye chati mbalimbali za muziki. Vanessa anatuwakilisha kwenye msimu mpya wa Coke Studio Africa unaoanza jumamosi hii huku pia akiwa mmojawapo wa wasanii wa nyumbani wanaogombania tuzo za MTV Base MAMAs kwenye kipengele cha Msanii bora wa kike. Atakinukisha tena wikiendi hii mjini Mombasa akiwa na wakali kama Wizkid na Chris Brown.
KUUPATA WIMBO HUO BOFYA DOWNLOAD HAPO CHINI.

04 October, 2016
Facebook kuzindua Messenger Lite Kenya.
Facebook imezindua aina mpya ya programu tumishi yake ya kutuma ujumbe ambayo inawalenga watu wa mataifa yanayoendelea.
Itazinduliwa katika nchi nyingine baadaye.
Messenger Lite imeundwa kutotumia sana data, jambo ambalo huwa tatizo kubwa mataifa yanayoendelea kutokana na gharama pamoja na kasi ya mtandao.
Programu hiyo ya simu za Android pia inaweza kufanya kazi kwa urahisi maeneo ambayo huduma ya mtandao si ya kutegemewa.
"Messenger Lite ukubwa wake ni chini ya 10MB, hivyo ni rahisi sana kuiweka kwenye simu na kuifungulia," taarifa ya Facebook imesema.
"Inatumia nembo inayokaribiana na ya Messenger, lakini rangi zake ni kinyume."
Wanaotumia programu hiyo ya Messenger Lite kwenye simu zao bado wataweza kutumia huduma muhimu zikiwemo uwezo wa kutuma ujumbe, picha na vihusishi vya kurasa za mtandao.
Hata hivyo, hawataweza kupiga simu za kawaida au za video kwa kutumia programu hiyo kama ilivyo kwa programu za kawaida za Messenger.
Facebook pia huwa na aina 'nyepesi' ya programu tumishi ya Facebook ambayo huitwa Free Basics na ambayo hufaa sana watu wasio na huduma ya kutegemewa ya mtandao.
Programu hiyo hupatikana katika mataifa kadha.
Afisa mkuu mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg mara kwa mara amekuwa akisema lengo ya kampuni yake ni kuhakikisha kila mtu duniani anaweza kutumia huduma ya mtandao.
Inakadiriwa kwamba watu bilioni moja duniani hutumia programu ya Messenger kutuma au kupokea ujumbe kila mwezi.
Fifa kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia Kufikia 48
Rais wa Fifa Gianni Infantino
ameshauri kuongezwa wa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48
zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa
atafikisha timu 40.
Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.
Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.
''Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,'' alisema Infantino mwenye miaka 46.
Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.
02 October, 2016
Uvaaji wa Suti kwa wanaume ni suala la uzoefu. Suti kali kwa maharusi 2016.
Kabla ya yote tambua yakwamba Uvaaji na Ununuaji wa suti ni jambo la Experience, Huwezi ukajitokea huko na kutaka kuvaa suti tuu, hili vazi lina watu wake bwana.. Kwa Muda sasa nmekua nikifuatilia na kutizama harusi za wengine hasa wanaume na kinachonifanya nifuatilie hayo ni namna gani bwana atakavyo kua ametupia suti yake, saa na Kiatu.
Najua una mchecheto wakufahamu suti gani utakayotupia siku yako ya Harusi yako maana hiyo ni Moja ya ndoto ama wazo lililoko katika kila kichwa cha Maharusi watarajiwa.. Leo nmekuandalia dondoo kadhaa ambazo zitakufanya uonekane mwenye Furaha ana kupendezwa na harusi yako...
Kama nilivyoeleza hapo juu kwamba Uvaaji wa Suti ni jambo la Experience hivyo wakati utakapo vaa nguo hiyo hakikisha unatia tabasamu la maana katika uso wako. Huwezi vaa hili vazi na Ukanunua aisee unaharibu utaratibu..
Hakikisha unachagua Rangi sahihi itakayo endena na wewe pamoja na Tukio kwa ujumla. Usikurupuke maana Utaaibika Vilivyo.
Hizi zifuatazo ambazo zimefanya Poa mwaka 2016...
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...