Unapozungumzia wanasoka waliowahi
kupatwa na masaibu makubwa katika maisha yao, kiasi cha kusababisha
kuacha makovu kwenye miili yao, basi huwezi kuacha kuwazungumzia
wanandinga Frank Ribery pamoja na Carlos Tevez.
Frank Ribery ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga katika klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.
Ribery
ni moja ya wachezaji wanaosifika kwa ubora wake uwanjani kutokana kasi,
nguvu, mbinu na uwezo mkubwa wa kupiga pasi pindi awapo uwanjani. Hata
hivyo makovu mawili makubwa aliyonayo usoni ndio yanamtofautisha na
wachezaji wengine wa kiwango cha aina yake (World class players).
Katika mahojiano yake kadhaa
ambayo amewahi kufanya na vyombo vya habari, Ribery ametanabaisha kuwa
makovu yake yametokana na ajali ya gari aliyoipta pindi alipokuwa na
umri wa miaka miwili.
Ribery anasema, “Tatizo ni kwamba
nilikuwa nimekaa siti ya nyuma na wakati ajali ile ilipokuwa inatokea,
nilirushwa mpaka upande wa mbele wa gari.” Alipata jeraha kubwa kiasi ya
kwamba, mamia ya nyuzi yalitumika kushona jeraha lake ili angalau aweze
kurudi katika hali yake ya awali.
Lakini swali ni kwamba kwa nini
mpaka sasa ameendelea kubaki na makovu makubwa wakati, kulingana na
utajiri alionao ana uwezo wa kufanya upasuaji ili kuondoa makovu hayo?
Wakati alipowahi kuhojiwa na
gazeti la La Gazzetta dello Sport la nchini Italia, Ribery alisema,
“Najivunia makovu yangu, yamenipa nguvu na muonekano mpya…Lazima uwe
timamu kiakili ili uweze kuvumilia utani kutoka kwa watoto na kejeli za
watu wazima”.
Ribery alihitimisha mahojiano
yake kwa kuongeza, “unionavyo hapa, hii ndio sura yangu halisi, tena
ambayo watu wanaitambua. Ninaufurahia sana uso wangu. Kwa nini
nisiufurahie?”
Carlos Tevez pia ni moja ya
wachezaji wa kiwango cha juu kabisa katika ulimwengu wa soka ambaye
anajulikana uwanjani kutokana na matumizi yake ya nguvu na uwezo mkubwa
wa kufunga pindi awapo uwanjani.
Hata
hivyo kama ilivyo kwa Ribery, Tevez pia ana kovu kubwa ambalo lipo
maeneo ya shavu lake la kulia, ambalo alilipata akiwa na takribani miezi
kumi tu tangu atoke tumboni mwa mama yake. Kwa upande wake, Carlos
Tevez katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya, amelielezea tukio
lililopelekea kupata kovu hilo kwa kusema, “Mama yangu akiwa anapata
kinywaji na mwenzie (shangazi yangu) huku wakiwa wameniacha nimekaa peke
yangu.
Bila ya kujua nilitambaa mpaka kwenye birika ambalo lilikuwa na maji ya moto na ndipo yaliponimwagikia na kuniunguza.”
Hata hivyo alipoulizwa kwa nini
mpaka sasa hajaliondoa kovu hilo ambalo lilimpelekea kulazwa hospitali
kwa miezi miwili, alijibu kuwa ni sehemu ya maisha yake namna alivyo
pindi alipokuwa mtoto mpaka sasa ukubwani.
Tevez
alisema, “ni kumbukumbu kubwa sana kwangu. Kamwe siwezi kufanya
upasuaji. Ukinichukulia kama nilivyo au vinginevyo, sawa tu. Vivyo hivyo
kwa upande wa meno yangu. Siwezi kujibadilisha namna nilivyo sasa”
Makovu ya Carlos Tevez yanabaki
kuwa kumbukumbu yake ya mafanikio kwa mji wa Fuerte Apache huko Buenos
Aires ambao uligubikwa na uhalifu wa hali ya juu na ambapo ndipo
alipozaliwa.
Aliongeza, “Pengine ningeweza
kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kuishia kusikojulikana
lakini kwa bahati nzuri, nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu na kufikia
hapa nilipo.
Kiukweli maisha yangu ya utotoni
niliyafurahia sana. Nilijifunza mengi ambayo yamepelekea leo hii mimi
kuwa hapa nilipo: heshima, unyenyekevu na kutoa sadakaUsisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment