25 July, 2015
PHARRELL WILLIAMS – FREEDOM (OFFICIAL VIDEO)
Mwimbaji wa muziki nchini marekani ambaye pia ni rapper na mwandishi
mzuri wa mashairi ya muziki nchini humo, Pharrell Williams ameachia
video yake mpya ya wimbo unaoitwa ‘Freedom’ Directed by Paul Hunter.
Chukua time hii kuitazama video hapa ukimaliza tunakuomba usibanduke
kwenye tovuti yetu kwani bado tunaendelea kukujuza zaidi.
KWA MARA YA KWANZA TONI BRAXTON & BABYFACE KUFANYA TOUR AFRICA
R&B superstars Toni Braxton and Kenny “Babyface” Edmonds kutoka marekani wanategemea kuperform ngoma zao kwa mara ya kwanza South Africa na Zimbabwe katikati ya tarehe 28, Agust 2015 – tarehe 3, September 2015, mashabiki watakiwa kukaa mkao wa kula na kuzisubiria siku hizo kwani, 28 August 2015 – watakuwa Harare, Zimbabwe – Borrowdale Racecourse, 30 August 2015 – watakuwa Durban – Moses Mabhida Stadium, 1 September 2015 – watakuwa Cape Town – Grand Arena, Grandwest, 3 September 2015 – watakuwa Johannesburg.
MAKALA: HIFADHI ZA WANYAMA TULIZO NAZO NI UZURI TOSHA WA TANZANIA
Na Francis Mawere.
Ni matumaini yangu yakwamba uu mzima na nipende kukupatia pole kwa mihangaiko ya hapa na pale.
Leo ningependa kidogo kuongelea juu ya HIFADHI ZA WANYAMA TULIZO NAZO HAPA KWETU.
Ni kweli kabisa TANZANIA ni nchi iliyo barikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii vikiwepo vileee vya hifadhi za wanyama. pata kuvijua hii leo.
Hifadhi ya Serengeti
Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.
Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia katika kaskazini-magharibi mwa Tanzania na inaenea kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Inaenea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.
Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi duniani,[1] ambao hua ni tukio wa nusu mwaka . Uhamiaji huo ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu ya kusafiri.
Kanda hii ina hifadhi za taifa na hifadhi mchezo kadhaa. Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai hasa, "Serengit" kumaanisha "Kiwara kisichoisha".
Inakadiriwa mamalia 70 kubwa na baadhi ya spishi 500 avifauna (yaani ndege) hupatikana huko. Tofauti hii ya juu upande wa spishi ni shughuli makazi mbalimbali kuanzia misitu ya riverine, mabwawa, kopjes mbuga na misitu. Nyumbu bluu, swara, punda milia na nyati ni baadhi ya mamalia kubwa ambao kwa kawaida hupatikana katika kanda hii.
Karibu Oktoba, karibu wanyama wanaokula majani (si nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. Katika mwezi Aprili, wao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena kuvuka Mto wa Mara. Jambo hili la mara kwa mara huitwa kwa Kiingereza "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu zaidi ya 250,000 pekee watakufa safarini kutoka Tanzania kwenda katika mbuga ya wanyama ya Masai Mara huko Kenya pande za juu, ambayo ni jumla ya maili 500. Kifo mara nyingi unasababishwa na maudhi au uchovu. Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.
Historia ya Hifadhi ya Serengeti
Sehemu kubwa wa Serengeti hapo awali ilijulikana kama Maasailand kwa wageni.
Wamasai walijulikana kama shujaa wakali, na waliishi pamoja na wanyamapori huku wakila mifugo yao pekee.
Nguvu zao na sifa zilisababisha wasafiri kutoka Ulaya kutotumia wanyama na rasilimali ya nchi yao vibaya.
Janga la "rinderpest" na ukame wakati wa 1890 ulisababisha kupungua kwa idadi ya Wamasai na wanyama. Uwindaji haramu wa wanyamapori na ukosefu wa moto, ambayo yalikuwa matokeo ya shughuli za binadamu, yaliweka hatua ya maendeleo ya misitu na vichaka kwa miaka 30-50 ijayo.
Uongezekaji wa chafuo sasa ulisababisha kutokuwa kwa makazi ya binadamu katika eneo hili.
Moto, tembo, na nyumbu walikuwa na ushawishi mkubwa katika kuamua sasa muundo wa Serengeti.
Mnamo miaka ya 1960, idadi ya binadamu ilivyoongezeka, moto, aidha kuwashwa kwa makusudi na Wamaasai ili kuongeza eneo ya malisho ya mifugo, au kwa ajali, ulisababisha kuchomeka kwa miche mipya ya miti.
Mvua nzito ilichangia ukuaji wa majani, ambao ulikuwa kama mafuta kwa moto wakati wa misimu mikavu ifuatayo. Miti mizee ya Acacia, ambayo huishi tu miaka 60-70, ilianza kufa. Awali tembo, ambao hula miti michanga na mizee, walilaumiwa kwa kumaliza misitu. Lakini majaribio yalionyesha kulikuwa na sababu nyingine muhimu zaidi. Wakati huo huo, idadi ya tembo ilipunguzwa kutoka 2,460 mwaka 1970 hadi 467 katika mwaka 1986 kutokana na uwindaji haramu.
Mnamo miaka ya 1970 idadi ya nyumbu na nyati wa Afrika ilikuwa imeongezeka, na walikuwa wakipunguza idadi ya majani kwa kasi, na kusababisha upungufu wa mafuta ya kusambazaa moto. kupunguka kwa ukali wa moto umesababisha Acacia kuwa imara tena.
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini. Kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi 19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na kufunikwa na theluji.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.
- Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiti hadi arktiki.
Kuna njia sita ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni.
- Njia iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo makao makuu ya hifadhi.
Hifadhi ya Mikumi
Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimukatika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
-Ndani ya hifadhi ya Mikumi kuna simba ambao huwa wanaonekana wakiwa katika himaya yao na mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.
-Wanyama wengine wengi hukimbilia katika eneo la miombo nyakati za mvua ambako unaweza kuwaona katika safu za milima. Hapo makundi makubwa ya nyati katika ukanda wa miombo wanaweza kuonekana.
-Kwa upande wa ndege, wakati wa mvua huongezeka na kufikia zaidi ya aina 300. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, nyakati hizi kunakuwepo na makundi ya ndege wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Asia ambayo, huungana na makundi ya ndege wakazikama vili chole.
-Makundi makubwa ya viboko, pundamilia na nyumbu huonekana katika eneo hili.
Ni matumaini yangu umeweza kufahamu Mbuga zetu maarufu zinazoipa Nchi yetu Uzuri unao washusha UDENDA na kumeaza MATE wazungu. Nipende kukushkuru ww uliechukua muda wako wa thamani kuipitia MAKALA hii.
OMBI LANGU KWAKO
Tuipende Nchi yetu, na mali zake zote kwani ni nchi pekee inayofaa.
Wayne Rooney amesema yuko tayari kuwa mfungaji bora wa Manchester Unites kwa mara nyingine
Wayne
Rooney amesema yuko tayari kuwa mfungaji bora wa Manchester Unites kwa
mara nyingine na amewapa changamoto wenzake ya kuandika Historia msimu
ujao.
Nyota
huyo wa England alicheza namba nyingi msimu uliopita chini ya Louis van
Gaal na ikifika wakati akashushwa mpaka kiungo cha chini.
Kwasasa Rooney anataka kucheza namba anayoipenda yaani namba 9 na amesema yuko tayari kufunga magoli.
“Niko
tayari kubadili akili yangu na kuwa moja ya wafungaji wa magoli,”
Amesema nyota huyo wa zamani wa Everton ambaye msimu uliopita aliifungia
United magoli 12.
“Nataka kucheza nafasi ya mshambuliaji ambapo nadhani ninaweza kufunga, naamini naweza kulitekeleza hilo”
Msimu
wa 2009-10 na 2011-12, Rooney alifunga magoli 34 kwenye mashindano yote
akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na kama atarudishwa nafasi hiyo
anaweza kufanya vizuri.
Siku
za karibuni, kocha wa Man United, Louis van Gaal alisema anatarajia
kumtumia Rooney kama mshambuliaji wa kati msimu ujao na maneno haya ya
Wayne ni majibu kwa bosi wake.
24 July, 2015
Baada ya kumuomba raisi Obama amsaidie hatimaye Chris brown aruhusiwa kuondoka ufilipino
Chris brown hatimaye ameachiwa kuondoka nchini ufilipino baada kuzuiwa na uhamiaji wa nchini humo kwa madai ya kutotokea kwenye show ya usiku wa mwaka mpya ambayo alikua amelipwa tayari, waandaji wa show hiyo walimshitaki Chris brown na kuomba serikali isimruhusu kuondoka hadi atakapo lipa pesa yao.
Chris brown ameweka video kwenye mtandao wa Instagram akiondoka Nchi humo,
Picha : Raisi Barack Obama awasili Kenya
Raisi wa Marekani, Barack Obama Tayari amewasili nchi Kenya kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili, baada ya Kenya raisi Obama anatarajia kutembelea nchi ya Ethiopia. Hii ni mara ya kwanza kwa raisi Obama kutembelea nchi ya kenya tangu achaguliwe kuwa raisi wa Amerika.
Hizi ni baadhi ya picha zake akiwasili nchi Kenya jioni ya leo,
Navy Kenzo na Vanessa Mdee: Game (Video)
Ni siku chache tu zimepita toka Navy Kenzo waachie wimbo wao mpya uitwao Game ambao ndani yake ameshirikishwa Bongo Fleva superstaa ambaye alishiriki MTV MAMA 2015 pia, Vanessa Mdee.
Navy Kenzo hawajachelewa kutusogezea video ya wimbo huo, saa chache zilizopita imenifikia hii video ambayo Navy Kenzo wameachia, ungependa kuiona? bonyeza Play kuicheki hapa.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni atoa wimbo mpya wa kampeni!
Wimbo mpya umetolewa nchini Uganda mwimbaji akiwa rais wa Uganda Yoweri
Museveni . Lakini bado bado haijafahamika wazi ikiwa yeye binafsi ndie
aliyeutoa ama alishiriki katika kuutoa.
Hata hivyo kuna tetesi kwamba ni wimbo mpya wa kampeni za uchaguzi mkuu ujao 2016. Sauti bila shaka ni rais Museveni, wimbo unaitwa Yegoma. Maana yake kwa taji --- kama la ufalme.
Maneno ya wimbo yanelezea uchungaji wa ngombe , ala za muziki na maisha marefu.
Beti ya kwanza inasema (Oruyogo-yongo - orwa Kabale) ikimaanisha usisalimu amri. Katika picha ya Video ya wimbo huo inaonyesha ndege aina ya Kulastara akijaribu kummeza chura, lakini chura anamkaba ndege kooni. Oruyongoyongo ni ndege anayekula nyoka na panya.
Na katika ubeti wa mwisho Rais anazungumzia maisha marefu na kuwaambia wasikilizaji kwamba wimbo kama Yengoma na Mpenkoni zinatakiwa kubaki katika jamii wakimukumbuka. Wimbo wa ''Mpenkoni'' yaani nipe fimbo, ulitumiwa na katika kampeni bwana Museveni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.
Wimbo huu mpya umetolewa ikiwa rais Yoweri Museveni anakabiliwa na upinzania mkubwa katika chama chake tawala cha NRM.
Aliyekuwa waziri wake mkuu Amama Mbabazi na makamu wake wa zamani Prof.Gilbert Bukenya wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais kwa chama tawala anachokiongoza rais Museveni.
Hata hivyo kuna tetesi kwamba ni wimbo mpya wa kampeni za uchaguzi mkuu ujao 2016. Sauti bila shaka ni rais Museveni, wimbo unaitwa Yegoma. Maana yake kwa taji --- kama la ufalme.
Maneno ya wimbo yanelezea uchungaji wa ngombe , ala za muziki na maisha marefu.
Beti ya kwanza inasema (Oruyogo-yongo - orwa Kabale) ikimaanisha usisalimu amri. Katika picha ya Video ya wimbo huo inaonyesha ndege aina ya Kulastara akijaribu kummeza chura, lakini chura anamkaba ndege kooni. Oruyongoyongo ni ndege anayekula nyoka na panya.
Na katika ubeti wa mwisho Rais anazungumzia maisha marefu na kuwaambia wasikilizaji kwamba wimbo kama Yengoma na Mpenkoni zinatakiwa kubaki katika jamii wakimukumbuka. Wimbo wa ''Mpenkoni'' yaani nipe fimbo, ulitumiwa na katika kampeni bwana Museveni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2011.
Wimbo huu mpya umetolewa ikiwa rais Yoweri Museveni anakabiliwa na upinzania mkubwa katika chama chake tawala cha NRM.
Aliyekuwa waziri wake mkuu Amama Mbabazi na makamu wake wa zamani Prof.Gilbert Bukenya wametangaza nia ya kugombea kiti cha urais kwa chama tawala anachokiongoza rais Museveni.
23 July, 2015
Video: Kama wewe ni shabiki wa Tamthilia ya “Empire” nimekuwekea trailer ya Season 2
Tamthilia ya “Empire” msimu wa pili itaanza kuoneshwa rasmi tarehe 23 mwezi september mwaka huu, huku kukiwa na orodha ndefu ya watu maarufu ambao wataonekana ikiwa ni pamoja na kelly rowland,chris rock, Luda cris na wengine wengi. Hii ni Trailer ya Msimu wa pili
Luda cris akithibitisha kuwa mmoja wa watakaoonekana kwenye msimu wa pili wa “Empire”
IT’S OFFICIAL ARTURO VIDAL NI MCHEZAJI WA BAYERN MUNICH
C.E.O wa Bayern Munich ame-conferm kuhusu usajili wa Vidal kujiunga na club yao leo hii. Karl-Heinz Rummenigge ametoa taarifa rasmi kwa vyombo habari kuhusu uhamisho huo.
“Ninaweza kuthibitisha kwamba kimsingi tumefanikiwa kufikia muafaka kati yetu na Juventus pamoja na Vidal. Kilichobaki ni kupitia vipimo vya afya na kusaini mkataba wenyewe. Tunategemea mambo yataenda vizuri na haraka ili ajiunge na mazoezi ya club wiki ijayo”.
Vidal ameisaidia club yake ya Juventus kucheza hadi fainali ya UEFA na pia timu yake ya taifa kuchukua kombe la Copa America.
klabu ya PSG imeghairi kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Angel Di Maria
Tetesi za usajili wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Angel
Di Maria kuondoka Old Trafford na kujiunga na Paris Saint Germain leo
zimechukua sura mpya.
Kwa siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimekuwa vikiripoti kwamba mchezaji huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Euro Millioni 60 na angetambulishwa rasmi na PSG Ijumaa hii, lakini kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha BeIN Sports kinachomilikiwa na bwana Nasser Ghanim Al-Khelaifi, ambaye mmiliki wa klabu ya PSG – ni kwamba klabu hiyo imeghairi kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo baina ya United na PSG yameisha rasmi.
Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kulipa kiasi cha £59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini muargentina huyo ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na inaaminika anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa kuafikiana juu, huku CEO wa United akiripotiwa kutaka kurudisha fedha zote walizotumia kumpata winga huyo.
Kwa siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimekuwa vikiripoti kwamba mchezaji huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Euro Millioni 60 na angetambulishwa rasmi na PSG Ijumaa hii, lakini kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha BeIN Sports kinachomilikiwa na bwana Nasser Ghanim Al-Khelaifi, ambaye mmiliki wa klabu ya PSG – ni kwamba klabu hiyo imeghairi kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo baina ya United na PSG yameisha rasmi.
Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kulipa kiasi cha £59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini muargentina huyo ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na inaaminika anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa kuafikiana juu, huku CEO wa United akiripotiwa kutaka kurudisha fedha zote walizotumia kumpata winga huyo.
22 July, 2015
Master J Aeleza Kwanini Aliachana na Mke Wake ‘Watu Waelewe tu Kuwa ni Bonge la Mwanamke’
Master J ameamua kuweka wazi sababu za kuachana na mke wake aliyezaa naye watoto watatu wa kike.
Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi wiki hii, producer huyo mkongwe alidai kuwa pamoja na ndoa yao kufa, mke wake ni mwanamke wa pekee.
“Wewe unaweza kuwa mtu mzuri na yeye anaweza kuwa mtu mzuri lakini when it comes to the matters of the heart ikawa inashindikana,” alisema. “Lakini sio kwamba mtu mmoja yeye ni mbaya, mimi ni mzuri zaidi, hapana. Watu lazima waelewe I can’t take away from her – ni bonge la mwanamke. Anajiheshimu and she is a good mom. Ni basi tu kwamba we were different.”
Hata hivyo Master J amekiri kuwa mke wake na wanae hawajatoa baraka zao kwa uhusiano wake na Shaa.
“Hiyo issue ngumu sana mpaka sasa hivi,” alisema J. “Unajua hii issue inawatesa sana watoto, separation yoyote watoto ndio wanaoteseka, kwahiyo najitahidi sana kuwa nao karibu, tunawasiliana everyday whenever I get time, tunahang out, lakini haijafika stage kwamba tunahang out kihivyo.”
Akiongea kwenye kipindi cha Mkasi wiki hii, producer huyo mkongwe alidai kuwa pamoja na ndoa yao kufa, mke wake ni mwanamke wa pekee.
“Wewe unaweza kuwa mtu mzuri na yeye anaweza kuwa mtu mzuri lakini when it comes to the matters of the heart ikawa inashindikana,” alisema. “Lakini sio kwamba mtu mmoja yeye ni mbaya, mimi ni mzuri zaidi, hapana. Watu lazima waelewe I can’t take away from her – ni bonge la mwanamke. Anajiheshimu and she is a good mom. Ni basi tu kwamba we were different.”
Hata hivyo Master J amekiri kuwa mke wake na wanae hawajatoa baraka zao kwa uhusiano wake na Shaa.
“Hiyo issue ngumu sana mpaka sasa hivi,” alisema J. “Unajua hii issue inawatesa sana watoto, separation yoyote watoto ndio wanaoteseka, kwahiyo najitahidi sana kuwa nao karibu, tunawasiliana everyday whenever I get time, tunahang out, lakini haijafika stage kwamba tunahang out kihivyo.”
Master Jay Akiwa na Watoto Wake |
Master anadai kuwa kipindi suala hilo limetokea na vyombo vya habari kutaka kujua kutoka kwake alipata shida kuzoea na ilimsumbua.
“Kwa utamaduni wetu sisi hapa Tanzania ni issue nzito sana. Watu kama ndoa imeshindikana wako tayari wakae tu kwenye hiyo ndoa mpaka siku Mungu akikuita but it’s not healthy.”
BUSUNGU, MWASHIUYA, WAIPA YANGA USHINDI WA KWANZA KAGAME
Mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na klabu ya Yanga akitokea
Mgambo JKT ya Tanga, Malimi Busungu, leo amefanikiwa kufunga magoli
mawili kati ya matatu wakati Yanga ikicheza dhidi ya Telecom ya Djibouti
kwenye mchezo wa Kundi A michuano ya Kagame Cup na kuifanya Yanga
kuandika ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo inayozidi kuchukua sura
mpya.
Shilole Atoboa Sababu ya Kuachana na Nuh Mziwanda
Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedai kuwa wivu ndiyo uliosababisha yeye na mchumba wake Nuh Mziwanda kuachana.
“Nuh haniamini kabisa na ana wivu kupitiliza ndo chanzo cha kuachana” Shilole amenukuliwa na Eatv.tv akieleza.
Wawili hao wamekuwa wakijibizana kwa maneno ya shombo kwenye midandao ya kijamii mara baada ya kuachana.
VIDEO ikimuonesha Straika wa Napoli, Gonzalo Higuain akizinguana na watu mjini Ibiza, Hispania.
Kuna video moja imeonekana leo ikimuonesha Straika wa Napoli, Gonzalo Higuain akizinguana na watu mjini Ibiza, Hispania.
Kwa mujibu wa ripoti, video hiyo ilirekodiwa alfajiri ya leo wakati nyota huyo mwenye miaka 27 akiondoka katika klabu moja ya usiku inayojulikana kwa jina la Pacha iliyopo kisiwani humo.
Higuain alikuwa anakula bata na mshambuliaji wa PSG, Ezequiel Lavezzi katika klabu hiyo, wanaripoti El Mundo.
Baada ya mshambuliaji huyo kuamua kurudi nyumbani, alizingirwa na mashabiki ambao walitaka asaini autograph, lakini Higuain alikataa na kuanza kuzinguana nao mpaka kufikia hatua ya kutaka kupigana.
Higuain alishikwa na mlinzi wake, na alipogundua tuko lile limerikodiwa alifoka kwa sauti:
“Futa video vinginevyo nitakupasua kichwa”.
Hata hivyo tukio hilo halikuendelea….Tazama video hapa chini:
Kwa mujibu wa ripoti, video hiyo ilirekodiwa alfajiri ya leo wakati nyota huyo mwenye miaka 27 akiondoka katika klabu moja ya usiku inayojulikana kwa jina la Pacha iliyopo kisiwani humo.
Higuain alikuwa anakula bata na mshambuliaji wa PSG, Ezequiel Lavezzi katika klabu hiyo, wanaripoti El Mundo.
Baada ya mshambuliaji huyo kuamua kurudi nyumbani, alizingirwa na mashabiki ambao walitaka asaini autograph, lakini Higuain alikataa na kuanza kuzinguana nao mpaka kufikia hatua ya kutaka kupigana.
Higuain alishikwa na mlinzi wake, na alipogundua tuko lile limerikodiwa alifoka kwa sauti:
“Futa video vinginevyo nitakupasua kichwa”.
Hata hivyo tukio hilo halikuendelea….Tazama video hapa chini:
Victoria Kimani aibua mjadala mkali hasa baada ya mashabiki wengi kuweka wazi hisia zao dhidi yake
Star wa muziki Victoria Kimani wa nchini Kenya, amekuwa kivutio cha
mjadala mkubwa katika mtandao wa twitter, hasa baada ya mashabiki wengi
kuweka wazi hisia zao dhidi ya diva huyo.
Baadhi yao wameelezea kuwa, msanii huyo amekuwa si mzalendo na mwenye
uwezo mdogo, akibebwa na sapoti ya usimamizi mzuri wa muziki wake.
Majadiliano hayo yamezuka baada ya mwanadada huyo kutoa lawama zake kuwa wakenya wamekuwa na uzalendo mdogo katika kuwasapoti wasanii wao kuweza kufanya vizuri nje ya nchi, binafsi akionekana kuwa mbali na nchi yake, akiwa anasimamiwa na lebo kutoka Nigeria.
Hata hivyo, staa huyo hajaonesha kurudishwa nyuma na matani mengi ya mashabiki kuhusu muziki wake huo, na kuwashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao kuhusu yeye wakitumia trend ya #someonetellVictoriakimani.
Majadiliano hayo yamezuka baada ya mwanadada huyo kutoa lawama zake kuwa wakenya wamekuwa na uzalendo mdogo katika kuwasapoti wasanii wao kuweza kufanya vizuri nje ya nchi, binafsi akionekana kuwa mbali na nchi yake, akiwa anasimamiwa na lebo kutoka Nigeria.
Hata hivyo, staa huyo hajaonesha kurudishwa nyuma na matani mengi ya mashabiki kuhusu muziki wake huo, na kuwashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao kuhusu yeye wakitumia trend ya #someonetellVictoriakimani.
#SomeoneTellVictoriaKimani that I agree with her. I believe in her. I adore her work @VICTORIA_KIMANI u need to mobilize local #254 votes
— Dr Kenneth Wameyo (@wameyokw) July 20, 2015
#SomeoneTellVictoriaKimani we know she is using the principle of " Controversy Sells" to get our attention, now that her music couldnt
— INKATHA (@kathaibui) July 20, 2015
#someonetellvictoriakimani here is the List of people who know her songs pic.twitter.com/G5izeuai02
— Victor Mateso Tupu™ (@victormatara) July 20, 2015
#SomeoneTellVictoriaKimani when she said difference btwn Nigeria n kenya is money well tafuta sponsor uko nje u reduce competition
— Black Dynamite (@ColnHarun) July 20, 2015
#SomeoneTellVictoriaKimani Someone is listening to her songs pic.twitter.com/nea87Ec8xG
— @Senkarani (@senkarani) July 20, 2015
Alright, I gotta go now😂I had FUN thanks for making #victoriakimani and #someonetellVictoriakimani TREND please continue to #supportYourOwn
— VICTORIA KIMANI (@VICTORIA_KIMANI) July 20, 2015
Louis Van Gaal amelalamikia kiwango kibovu alichokionesha kiungo wa kijerumani Bastian Schweinsteiger
Matarajio ya mashabiki wa timu
mbalimbali za soka duniani ikitokea wachezaji wamesajiliwa na timu zao
kwa ada kubwa ya uhamisho, wanasubiri kuona wachezaji hao wanafanya
vizuri katika timu mapema.. na hali hiyo sio kwa mashabikio pekeyao ila
hata Kocha wa Manchester United Louis van Gaal.
Licha ya ushindi wa goli 3-1 walioupata Man United dhidi ya San Jose Earthquakes, kocha wa Man United Louis Van Gaal amelalamikia kiwango kibovu alichokionesha kiungo wa kijerumani Bastian Schweinsteiger ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea FC Bayern Munich ya Ujerumani kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pound milioni 15.
“Mchezaji
anaweza kucheza vibaya kama amefanya mazoezi kwa siku tatu hadi sita,
lakini anaweza kumudu kucheza kwa dakika 45. Schweinsteiger alicheza
vibaya, nafikiri mechi ya kwanza alicheza vizuri ila kwa hii amecheza
vibaya”>>>Louis van Gaal
Tazama magoli yote ya Manchester United na Highlights za mechi:
Radio na Weasel kutoka Uganda wameitambulisha leo hii ‘Juicy Juicy’…(Video)
Radio na Weasel kutoka Uganda wamerudi tena kwenye Pande za burudani baada ya kuachia Video yao mpya inayoitwa ‘Juicy Juicy’ iliyoongozwa na Savy Filmz.
Nakukaribisha uitazame hapa mtu wangu…
AUDIO: Navy Kenzo na Vanessa Mdee “Game”
Navy Kenzo ni kundi lenye mapendekezo ya kuwania tuzo za Kilimanjaro
Tanzania Music Awards (KTMA) mara mbili mfululizo katika kipengele cha
kundi bora la mwaka, ikiwemo mwaka huu pia. Rekodi ya “Game” ni nyimbo
ya pili kutoka kwenye albamu yao ya “Above In a minute”
Nyimbo hii “GAME” imetayarishwa na Nahreel (The Industry Studios)
Huu wimbo mpya wa Mr Blue ‘Changamoto’ usikilize hapa
Baada ya kutoa video na Navio wa Uganda, Mr Blue ametoa wimbo wake mpya ‘Changamoto’ usikilize hapa kwa kubonyeza Play.
21 July, 2015
Wasafi Records ya Diamond Platnumz kuanza kurekodi nyimbo bure kusaidia chipukizi..
Diamond Pltnumz ni mmoja ya wasanii wa Tanzania ambao wana mafaniko ya
kutosha, Diamond Platnumz kaamua kushare mafanikio yake kwa kufungua
studio ya muziki na kurekodi nyimbo bure kabisa kwa wasanii chipukizi
wasiokuwa na uwezo.Kupitia kipindi cha Jump Off cha Timez fm Diamond Platnumz amesema “Wasafi
Records’ sio nimelenga biashara itakuwa uongo,Lakini hiyo studio
nilivyokuwa nimeiweka nimesema arekodiwe msanii yeyote mwenye kipaji,
akiwa mtu ana kipaji kizuri ana nyimbo nzuri mrekodie mpe. Lakini pia
iko na kibiashara kwa wasanii wengine sio msanii ameshatoka aje pale
aimbe bure,kuna wasanii ambao watakuwa chini ya management yangu chini
ya kampuni yangu mfano huyu anaitwa Hamonizer”.
NICKI MINAJ ATINGA CLUB BILA WALINZI..!!!
Rapper wa kike Nicki Minaj ameingia kwenye stori kubwa baada ya
kwenda klabu bila kuwa na ulinzi huku akiambatana na mpenzi wake Meek
Mill, kwa kitendo hiko kimepelekea watu wengi kumshangaa staa huyo
kutinga Hollywood nightclub akiwa na beau Meek Mill
Mbali na kufanya hivyo ilikuwa ni maangalizi kuwa ana maadui kwake au marafiki ambao wanapenda kazi zake, hiko ndio kipimo tosha kwa mtu maarufu duniani kujiangalia kuwa unapendwa vipi na kujua nini mtaa unataka.
Mbali na kufanya hivyo ilikuwa ni maangalizi kuwa ana maadui kwake au marafiki ambao wanapenda kazi zake, hiko ndio kipimo tosha kwa mtu maarufu duniani kujiangalia kuwa unapendwa vipi na kujua nini mtaa unataka.
How To Become A Woman That Every Man Desires (Regardless Of Your Appearance)
Whether you are single and serially first-dating, or you are struggling with a distant boyfriend who you want to open up to you, or you want to get that ex boyfriend back – Alex Carter has got a technique for you!
Alex Carter is a well-known relationship expert and dating coach. He has dedicated his life to the art of helping women get their dream man by studying the art of attraction and developing a system to help women in every situation get the man they want. He has compiled all of his research and knowledge into an easy to read e-book: ‘Make Him Desire You’.
If you are interested in learning some unconventional ways to get a guy attracted to you. If you have relationship problems and want to fix them, or if you simply want to understand men in general better, then this book is for you.
Make the man of your dreams desire you
* P.S At the very end of this presentation, you will also discover a man’s most intense and secret desire, that he never shares with any woman.
Man City yaichapa AC Roma kwa penalti 5 kwa 4
Klabu ya Manchester City imeshuka dimbani leo hii kucheza mechi yake ya kwanza ya michuano ya International Champions Cup dhidi ya AS Roma ya Italia… Michuano hiyo inayoandaliwa na Audi inafanyika Australia katika Uwanja wa Melbourne Cricket Ground na kushirikisha jumla ya timu tatu za Real Madrid, AS Roma na Man City.
Man City imeshinda mechi yake ya kwanza dhidi ya AS Roma ya Italia kwa mikwaju ya penati 5 kwa 4 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2… magoli yaliofungwa na Raheem Sterling dakika ya 3 na Kelechi Iheanacho dakika ya 51 kwa upande wa Man City huku yale ya AS Roma yakifungwa na Miralem Pjanic dakika ya 8 na Adem Ljajic 87.
Huu pia ni mchezo wa kwanza kwa Raheem Sterling toka ajiunge na klabu ya Man City akitokea Liverpool kwa dau la pound milioni 49.
Nimekusogezea picha na video za magoli mtu wangu.
Hapa kuna video zinazoonesha magoli yote yalivyofungwa.
Penalti zote hizi hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...