Showing posts with label MAISHA. Show all posts
Showing posts with label MAISHA. Show all posts

14 October, 2015

Je, unayafahamu haya kuhusu wanawake?


Kuna usemi mmoja nimezoea sana kuusikia “I can’t understand women” hii ni nyimbo kila mwanaume anaimba, inawezekana ikawa kweli, kutokumuelewa mwanamke, inawezekana ikawa inasababishwa na wewe kutokuelewa mambo kadhaa yanayowahusu wanawake, hapa tafiti wa  kisayansi  na zisizo za kisayansi  zitakusaidia kumuelewa mwanamke kisaikologia na kitabia.
  1. Mapigo ya moyo ya mwanamke hupiga haraka kuliko mwanaume.
Maumbo ya wanawake huwa si makubwa kama ya wanaume , kwahiyo mioyo yao huwa inapiga mara nyingi, moyo wa mwanamke unapiga mapigo 78 ndani ya dakika moja.

  1. Mwanamke anaongea maneno 20,000 kwa siku wakati mwanaume anaongea maneno 13,000 tu kwa siku. Inawezekana ni watu wa maneno mengi na stori nyingi pia.

  1. Mwanamke hulia mara 30-64 kwa mwaka. Inasemekana tatizo la homoni, kuna asilimia 60% ya homoni inayoitwa prolaktini kwa wanawake kuliko kwa wanaume

  1. Mtaalamu wa Kwanza wa Program za Kompyuta (computer programmer) ni Mwanamke. Nani kasema wanawake hawawezi hesabu , Ada Lovelace (1815 -1852 ) ndio mwanamama  wa kwanza kufanya program za kompyuta.  Na inasemekana  katika rekodi zilizowahi kuwekwa  mtu wa kwanza kugundulika kuwa na  Uwezo mkubwa wa kufikiri (IQ)  ni Mwanamke.

  1. Wanawake wanapenda sana Chokoleti kuliko Tendo la ndoa. Utafiti unaonyesha wanaume wanapenda sana kufanya mapenzi kuliko wanawake, wanaume hutumia sana akili wakati wanawake ni watu wahisia zaidi,(emotions) hisia gani wanazipata wanawake wakila chokoleti hilo ni kwa wanaume kujiuliza.

  1. Asilimia 30 tu ya wanawake huwa wana furahia tendo la ndoa, wanawake wengi huwa hawatimiziwi haja zao za mwili na wengi wao hudanganya kama wameridhika, ila ukweli ni kwamba wachache kufikia haja zao kikamilifu. Inaweza ikawa ni matatizo ya kisaikologia au wanaume kutokujua wapenzi wao wanaridhika na nini.

  1. Kila mwanamke ana kitu kimoja hapendi juu ya mwili wake. Inaweza ikawa ni ukubwa wa matiti yake, tumbo lake au miguu yake hii inategemaa na mtu na mtu

  1. Akili ya mwanamke ni safi kuliko ya mwanaume, hii ni kwasababu mwanamke ni mtu wa vitu vingi akili ya mwanamke inaweza kuwa safi mara nyingi kuliko wanaume, akili chafu au wanaita Dirty mind hii ni kwa wanaume zaidi.

  1. Wanawake wana uwezo mkubwa wa kusikilizaa, wanaume wanasikiliza na upande mmoja tu wa ubongo,upande wa kushoto wa ubongo wao katika kusikiliza wakati wanawake wanatumia pande zote mbili katika kusikiliza .

  1. Wanawake wanaishi miaka mingi kuliko wanaume Dunia . Hii inaweza kuelezwa na sababu mbalimbali , kiwango cha homoni (Testosterone na estrogen) wanawake wana  uwezo mkubwa wa kuzoea mazingira kuliko wanaume . Hata hivyo, kuwa na muda mrefu wa kuishi haina maana wanawake wana  afya bora  kuliko wanaume.  Ila mazingira ambayo wanaume wanaweza yakawashinda wanawake wanayaweza.

15 May, 2015

Petr Cech anaondoka Chelsea? huu ndio msimamo wa klabu yake

cech
Baada ya klabu ya Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England..sasa wameanza mikakati ya kukiboresha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu. Kipa wao Petr Cech baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2004 uongozi wa timu yake umempa uhuru wa

15 April, 2015

KAMA UNATAKA MAISHA YAKO YAWE MAZURI ACHA UOGA WA KUTHUBUTU.

Success-quotes-16428993-640-480[1]
“Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa Sana”Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani kwa mfano kufungua miradi, kufanya biashara, kusoma kwa bidii na mambo mengine kibao.
Ngoja nikuulize tena, maana najua utakua ushaulizwa hili swali mara nying, Hivii unatamani kuishi au uwe kama nani ? wengi wetu mtasema natamani kuishi maisha mazuri na bora.

04 April, 2015

Jinsi ya Kuishi Maisha Yenye Furaha

Mwanamke akiitazama familia yenye furaha





“Nitakuwa na furaha nikifunga ndoa na kupata watoto.”
“Nitakuwa na furaha nikimiliki nyumba yangu mwenyewe.”
“Nitakuwa na furaha nikipata kazi.”
“Nitakuwa na furaha nikiwa na . . .”
JE, UMEWAHI kuhisi hivyo? Je, ulipopata kile ulichokuwa unatamani, furaha yako ilidumu, au ilianza kupungua? Kwa kweli, kufikia lengo au kupata kitu tulichotamani kunaweza kutufanya tuwe na furaha, lakini furaha hiyo huenda isidumu. Furaha ya kudumu haitegemei tu mafanikio au vitu tulivyo navyo. Badala yake, furaha ya kweli inategemea mambo mengi kama tu jinsi mtu anavyohitaji kufanya mambo mbalimbali ili awe na afya nzuri.
Mahitaji yetu yanatofautiana. Kinachokufurahisha wewe huenda kisimfurahishe mwingine. Kwa kuongezea, tunabadilika tunapoendelea kukua. Ingawa hivyo, uthibitisho unaonyesha kwamba kuna mambo ambayo huhusianishwa na furaha. Kwa mfano, furaha ya kweli inahusiana na kuridhika, kutowaonea wivu wengine, kuwapenda watu, na kutokata tamaa. Acheni tuchunguze mambo hayo.

1. KURIDHIKA

Mwanamume mmoja mwenye hekima alisema hivi: “Pesa ni ulinzi.” Hata hivyo, aliongezea kusema hivi: “Anayependa fedha hatatosheka na fedha, wala anayependa mali hatatosheka na mapato. Hilo pia ni ubatili.” (Mhubiri 5:10; 7:12) Alimaanisha nini? Ingawa ni kweli tunahitaji pesa ili kuishi, tunapaswa kuepuka pupa, kwa sababu hatuwezi kutosheleza tamaa hiyo! Mfalme Sulemani wa Israeli la kale, aliyesema maneno hayo, alifanya utafiti ili kuthibitisha ikiwa kuishi maisha ya anasa kunaleta furaha ya kweli. Aliandika hivi: “Sikuyanyima macho yangu chochote ambacho yaliomba. Sikuunyima moyo wangu shangwe ya aina yoyote.”—Mhubiri 1:13; 2:10.
Baada ya kujikusanyia utajiri, Sulemani alijenga majumba makubwa, alitengeneza mabwawa ya kuogelea na bustani maridadi, na alikuwa na wafanyakazi wengi. Alipata kila kitu alichotaka. Alijifunza nini? Mambo hayo yalimletea furaha kwa kiasi fulani, lakini si kwa muda mrefu. Aliandika hivi: “Na, tazama! kila kitu kilikuwa ubatili na kufuatilia upepo, wala hapakuwa na lolote lenye faida.” Hata aliyachukia maisha! (Mhubiri 2:11, 17, 18) Kwa kweli, Sulemani alitambua kwamba maisha ya kujistarehesha tu hayaleti furaha ya kudumu. *
Je, utafiti wa kisasa unakubaliana na jambo hilo? Makala moja kwenye Jarida la Masomo ya Jinsi ya Kuwa na Furaha (la Kiingereza) inaeleza hivi: “Mara baada ya mtu kutosheleza mahitaji yake ya msingi, vitu vingine atakavyozidi kupata havitamwongezea furaha.” Kwa kweli, utafiti unaonyesha kwamba ikiwa mtu anaamua kufuatilia maisha ya anasa na kupuuza viwango vya maadili na vya kiroho, anaweza kupoteza furaha.
KANUNI YA BIBLIA: “Namna yenu ya maisha iwe bila upendo wa pesa, huku mkiridhika na vitu vya sasa.”Waebrania 13:5.

2. EPUKA KUWAONEA WIVU WENGINE

Kamusi moja inafafanua wivu kuwa “uchungu au kinyongo kinachotokana na kutambua kwamba mwingine ana kitu ambacho huna, na pia tamaa ya kutaka kuwa na kitu hicho.” Kama tu uvimbe hatari unaoenea haraka, kuwaonea wivu wengine kunaweza kutawala maisha ya mtu na kumfanya akose furaha. Mtu huanzaje kuwaonea wivu wengine? Tunawezaje kutambua kama tuna tatizo hilo? Na tunawezaje kukabiliana nalo?
Kulingana na kitabu Encyclopedia of Social Psychology watu huwa na mwelekeo wa kuwaonea wivu watu ambao wanalingana nao, huenda katika umri, uzoefu, au malezi. Kwa mfano, si rahisi kwa mfanyabiashara kumwonea wivu mwigizaji maarufu. Lakini huenda akamwonea wivu mfanyabiashara mwenzake mwenye mafanikio kuliko yeye.
Mfano: Maofisa fulani katika utawala wa zamani wa Uajemi, hawakumwonea wivu mfalme, badala yake walimwonea wivu Danieli ofisa mwenzao. Kwa sababu ya wivu wao hata walifanya mpango wa kumwua Danieli! Hata hivyo mpango huo haukufanikiwa. (Danieli 6:1-24) Kitabu Encyclopedia of  Social Psychology kinaendelea kusema hivi: “Ni muhimu tutambue kwamba wivu unaweza kutufanya tutake kuwadhuru wengine. Ndiyo maana kuna visa vingi vya ukatili katika historia ya wanadamu ambavyo vimesababishwa na kuwaonea wivu wengine.” *

3. WAPENDE WATU

Kitabu Social Psychology kinasema: “Ikiwa watu wana uhusiano mzuri miongoni mwao, jambo hilo linaweza kuwafanya wafurahie maisha hata kuliko furaha inayopatikana kwa kuwa na kazi, mshahara mnono, kukubaliwa katika jamii, au kuwa na afya nzuri.” Kwa ufupi, ili wanadamu wawe na furaha ya kweli, wanahitaji kupenda na kupendwa. Mwandikaji mmoja wa Biblia alisema hivi: “Ikiwa . . . sina upendo, mimi si kitu.”—1 Wakorintho 13:2.
Sisi sote tuna nafasi ya kusitawisha upendo. Kwa mfano, Vanessa alikuwa na baba mkatili na mlevi kupindukia. Alipokuwa na umri wa miaka 14, alitoroka nyumbani na hakuwa na makazi maalumu, na hata alimwomba Mungu amsaidie. Kisha, inaonekana kwamba Mungu alimsaidia kwa sababu alianza kuishi na familia iliyofuata kanuni ya Biblia inayosema “upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili.” (1 Wakorintho 13:4) Kuishi na familia hiyo na kujifunza Biblia, kulimsaidia Vanessa kupona kihisia na kiakili. Alisema hivi: “Nilianza kufaulu masomoni na alama zangu zikawa bora.”
Vanessa bado anakumbuka mambo yaliyompata zamani. Hata hivyo, sasa ana ndoa yenye furaha na ni mama wa wasichana wawili.
KANUNI YA BIBLIA: “Jivikeni upendo, kwa maana huo ni kifungo kikamilifu cha muungano.”Wakolosai 3:14.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...