21 October, 2016

IZZO B -Bado tunawekana sawa na YCEE, ngoma inakuja

Mkali wa Rap kutoka Mbeya City IZZO B amesema wimbo wao wa The Amaizing walioimba na YCEE utatoka bila ya msanii YCEE kusikika na baadaye watafanya Remix ya wimbo huo ambayo YCEE atasikika.
Izzo
Amesema kuwa hiyo ni kutokana na kutoafikiana na kutokubaliana kibiashara baina ya wasanii hawa.

Akipiga story ndani ya kipindi cha eNewz Izzo amesema "Kuna sababu za kibiashara ambapo bado kuna vitu tunaweka sawa kwa kuwa hatutaki kukaa kimya kwa muda mrefu tutatoa wimbo halisi na baadaye tutakuja tena na marudio ya wimbo huo (remix)".

Pia Izzo alisema kuwa kutokana na muda kuwa mrefu na kuna vitu ambavyo bado wanaviweka sawa juu ya makubaliano ya kibiashara na kwamba wimbo huo ni wa siku nyingi zaidi hivyo wameona watoe wimbo halisi kwanza kwa kuwa wanavyozidi kukaa muda utakuwa mrefu zaidi.

CHANZO: eatv.tv

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...