17 October, 2016

Mourinho kuchunguzwa na FA juu ya kauli kwa mwamuzi

Matamshi ya Jose Mourinho kuhusu uteuzi wa mwamuzi anaeshabikia Manchester United Anthony Taylor kwa mchezo wa ligi kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool utakaochezwa leo jumatatu yatachunguzwa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchini humo FA.
Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa.
'Mtu mmoja akiwa na lengo anaweka shinikizo kwake' alisema Mourinho
Kwa kawaida makocha hawatakiwi kuzungumza lolote kuhusiana na mwamuzi kabla ya mchezo.Anthony Taylor hajatoa kadi yoyote nyekundu msimu huu

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...