Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki waliotamani kuona
Diamond Platnumz na mwanadada Lady Jay Dee wakifanya kazi pamoja, wakali
hao wa bongo fleva huenda wakaja na 'collabo' ya hatari, siku chache
zijazo.
Hatua hiyo inatokana na msanii Diamond kufunguka kuwa hakuna sababu
yoyote inayowakwamisha kufanya kazi ya pamoja, isipokuwa muda na ratiba
zao kubana.
Dangote ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea ofisi za Kituo cha runinga EATV,
na kukutana na maswali mbalimbali ikiwemo sababu za wao kutofanya kazi
ya pamoja licha ya mashabiki kuitamani 'collabo yao.
"Siku si nyingi tutafanya kazi pamoja na Jay Dee, kilichotukwamisha
ni ratiba zetu, lakini pia nilikuwa sijafikiria hilo, ila sasa kwa kuwa
mashabiki wamekuwa wakiomba kila mara, nitawasiliana naye, na tutafanya
kazi ya pamoja muda mfupi ujao, hakuna sababu nyingine tofauti na
kubanwa na kazi nyingi, pamoja na ratiba zetu kutoendana"
Kuhusu ni lini mashabiki wategemee kazi hiyo, Dangote alisema kuwa
hawezi kuahidi tarehe, lakini ana uhakika 'collabo' hiyo inakuja.
CHANZO:eatv.tv
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment