16 October, 2016

Wasanii hawa walitamani jukwaa la EATV AWARDS

Tuzo kubwa za muziki na filamu zinazotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza tar 10 Desemba 2016 jijini Dar es salaam Tanzania, zimeleta hamasa kubwa wasanii wa nchi za Afrika Mashariki wakisema ni neema kwao, huku wengine wakilitamani jukwaa lake.
Wakizungumza na East Africa Tv na East Africa Radio kwa nyakati tofauti tofauti, baadhi ya wasanii wamesema wapo tayari kutoa burudani siku ya kutolewa kwa tuzo hizo, burudani ambayo itaandikwa kwenye historia ya EATV AWARDS.

Kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, msanii Peter Msechu alisikika akisema iwapo hatakuwa nominated kwenye tuzo hizo, anatamani apewe fursa ya kutoa burudani ambayo itaacha historia kwake na kwa mashabiki.

"Yani acha niseme tu kwa kweli, hata nisipokuwa nominated au kushinda hizo tuzo, basi naomba nipewe fursa ya kuperfom kwenye EATV AWARDS, na siku hiyo nawaambia nitatoa burudani ya kufa mtu, kwa mara ya kwanza nitaperfom tumbo wazi, nitavua shati ili watu wote waone litumbo langu siku hiyo, naitamani hiyo siku kama nini", alisema Peter Msechu.
Naye msanii mkongwe wa rap hapa bongo ambaye alikaa kimya kwa muda mrefu na kurudi kwa kishindo, King Crazy GK, amesema anatamani angeperfom kwenye sherehe za utoaji wa tuzo hizo, kwani itakuwa ni furaha kubwa kwake.

"EATV AWARDS tunaisubiria kwa hamu, na natamani yani natamani sana, achana na kupata tuzo, japo hata kuperfom katika tukio kama hilo", alisema King Crazy GK.

EATV AWARDS ndio tuzo kuwa za kwanza kuanzishwa na media Afrika Mashariki, ambazo zitahusisha wasanii wa filamu na muziki wa nchi za Afrika Mashariki moja kwa moja.

CHANZO: EATV

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...