Ligi Kuu ya Tanzania Bara raundi ya 12 inaendeleaLeo(Jumamosi) kwa
michezo sita ambako mabingwa watetezi Young Africans ya Dar es Salaam
itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba
mkoani Kagera.
Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa
mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri
hadi Mtwara kucheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona
wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye
mchezo utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.
Majimaji itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa
Majimaji huko Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00
jioni kwa saa za Afrika Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT
Ruvu itaanza saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi-Mbagala
Dar es Salaam.
Jumapili itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo
itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati
Tanzania Prisons itapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment