21 October, 2016

Kamera Ya Mbele (Selfie) Mbioni Kutumika Kama 'Password' Ili Kuweka Ulinzi Zaidi

Kamera ya mbele maaru kama ‘Selfie Camera’ itakua haina kazi chache tuu kama tulivyoziea kuzifanya katika kamera hiyo.Kumbuka wengi wetu huwa tunaitumia katika kupiga picha tuu na wengine pengine hawaitumii kabisa kulingana na uwezo wa kamera hiyo.
Lakini kumbuka pia kamera ya mbele (selfie) imejipatia umaarufu mkubwa kutokana na zile picha ambazo watu huwa wanajipiga wenyewe. Kutokana na hili makampuni yamekaa na kutafuta namna au njia nyingine ambayo kamera hii inaweza ikatumika.
 Matumizi ya kamera hii ya mbele hata kwa sasa yanatumika katika App za Uber, HSBC na Mastercard kama njia moja wapo ya usalama baina ya App na mtumiaji wa App hiyo.Yaani ni hivi makampuni mengi kwa sasa wana mpango wa kufanya kamera ya mbele ya simu yako iwe ni kama Password yako.

 Hapo utaachana na kuingiza manamba au maneno au hata ‘patterns’.Kwa mfano App ya Mastercard imeapa kuwa itabadilisha kabisa password za kawaida kwenda katika mfumo wa ‘selfie’ yaani hii inamaanisha kuwa mtumiaji au mteja wa Mastercard atakuwa na uwezo wa kuiangalia kamera yake ya selfie ili kuweza kupata huduma Fulani katika akaunti yake.

Mpaka sasa makampuni mengi bado yapo katika majaribio na maboresho ya teknolojia hii lakini hii pia haimanishi kuwa ‘password’ za kawaida na ‘finger print’ zinapotea. Kingine kizuri ni kwamba watu hawatakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza nenosiri gumu ambalo mtu mwingine hatoweza kulikisia.

CHANZO:  http://teknokona.com/

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...