Baada ya Uganda kupangwa Kundi D sambamba na timu za Misri, Ghana,
pamoja na Mali kwenye micuano ya AFCON 2017, kocha wa Uganda Cranes
Micho Sredojević ametoa wito kwa serikali kuhakikisha timu inapata
support ya kutosha kwa ajili ya maandalizi ya mapema.
Licha ya timu yake kupangwa kwenye Kundi gumu, Micho hana budi bali ni kupambana na changamoto iliopo mbele yake.
“Hakuna namna ya kukwepa, unaweza ukasema pengine ndiyo mwisho wetu,
ni sawa na Kundi tulilopo kwenye Kombe la Dunia lakini safari hii ni
fainali za AFCON dhidi ya Ghana na Misri. Ni kundi gumu lenye
ushindani,” alisema Micho mara baada ya draw ya upangaji makundi
kukamilika.
Ghana walipoteza kwenye mchezo wa fainali katika michuano iliyopita
ya FCON iliyofanyika Equatorial Guinea 2015 dhidi ya Ivory Coast. Misri
ni nchi yenye uchu ikiwa imeyakosa mashindano hayo kwa miaka misimu
mitatu iliyopita, lakini wakiwa ni mabingwa mara tatu mfululizo
waliopta, Mali ndani ya fainali tatu za AFCON wameshika nafasi ya tatu
mara mbili, ni kundi gumu.
Ghana na Uganda zilitoka suluhu kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi E
kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na
wanatarajia kucheza mara mbili dhidi ya Misri baada ya michuano ya AFCON
kumalizika.
“Ukiangalia kila kitu, utaona tunatakiwa kuanza maandalizi sasa kwa
upendo na support kutoka waganda wote, wachezaji na wote wenye wajibu wa
kuiandaa timu yetu kuwa timu yenye ushindani, hapa nafikiria maandalizi
pamoja na mechi za kirafiki ambapo tutakuwa makini na kila taarifa.
Naamini katika soka hakuna kinachoshindikana bali kila kitu
kinawezekana.”
“Ninaiamini timu na wachezaji tulionao, naamini katika kile
tunachokifanya, ninaamini serikali ya Uganda itatusaidia kuhakikisha
tunaliwakisha taifa katika njia bora.”
“Hatua tuliyofikia ni nusu ya safari, ili safari yetu ikamilike
tunahitaji kuanza maandalizi sasa, tunastahili kuwa hapa lakini
tunahitaji kuonesha hilo kwa vitendo tukiwa uwanjani na si kwa kuongea.”
Uganda wataanza kampeni yao kwa mchezo wao wa ufunguzi January 17
dhidi ya The Black Stars, kisha watashuka tena uwanjani kukabiliana na
mapharao wa Msri January 21 kabla ya kuhitimisha hatua ya makundi dhidi
ya Mali January 25.
Makundi
GROUP A: Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea Bissau
GROUP B: Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe
GROUP C: Cote D’Ivoire, DR Congo, Morocco, Togo
GROUP D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda
20 October, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment