Paul Pogba alifunga mara mbili
wakati Manchester United walipoibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya
klabu ya Fenerbahce katika kundi A.
Goli la Pili kwa United liliwekwa kimiani na Anton Martial kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku la mwisho likipachikwa na Jesse Lingard kwa shuti kali la chinichini.
Robin Van Persie aliiandikia timu yake ya Fenerbahce goli la kufutia machozi lililoshangiliwa na mashabiki wa pande zote akiwemo kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson.
Matokeo mengine katika michezo ya ligi ya Europa
FC Steaua București 1-1 FC ZürichFK Krasnodar 0- 1 Schalke
FC Slovan Liberec 1-3 Fiorentina
Hapoel Be'er Sheva 0-1 Sparta Prague
Inter Milan 1-0Southampton
Osmanlispor 2-2 Villarreal
FK Qarabag 2-0 PAOK Salonika
Celta Vigo 2-2 Ajax
Standard Liege 2-2 Panathinaikos
Konyaspor 1-1 Sporting Braga
Shakhtar Donetsk 5-0 KAA Gent
FC RB Salzb 0-1 Nice
No comments:
Post a Comment