18 October, 2016

Napenda kufanya kazi na undergrounds - Manecky

Mtayarishaji wa muziki kutoka katika studio za 'AM Records' Manecky amefunguka na kusema kuwa yeye anapenda sana kufanya kazi na wasanii chipukizi au wasanii ambao tayari walikwisha potea kwenye muziki.

Amesema kupitia wasanii hao yeye kama producer anaweza kuonesha uwezo wake katika kufanya muziki tofauti na kufanya kazi na wasanii ambao tayari ni wakubwa au ambao wapo kwenye soko kwa wakati huo.

Manecky alipokuwa akizungumza na shirika la habari la taifa alidai kuwa yeye kama mtayarishaji anaweza kuonesha uwezo wake pindi anapofanya kazi na wasanii wachanga na wasanii ambao wamepotea kwenye 'game'.

"Mimi huwa napenda kufanya kazi na 'undergrounds' kwa sababu kupitia hao wasanii naweza kuonesha uwezo wangu kama producer hawa wasanii wakubwa wanaweza kukubana kuonesha uwezo wako, lakini leo hii ukifanya na mwanamuziki mkubwa ni kweli utafahamika na utakuwa unasikika mara kwa mara lakini siku akiacha kufanya kazi na wewe ndiyo na wewe umeshapotea kwenye ramani, lakini ukiweza kumtoa msanii mchanga na kuwa mkubwa ina maana utakuwa na uwezo wa kumtoa mwingine na kuwa mkubwa pia, hivyo utaendelea kuwepo kwenye tasnia siku zote" alisema Manecky

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...