Baada
ya miaka nane tangu aondoke Barcelona, staa wa zamani wa klabu hiyo,
Ronaldinho amerudi katika klabu hiyo huku akikabidhiwa jukumu
lingine tofauti na kucheza soka.
Ronaldinho
ambaye aliichezea Barcelona msimu wa 2003-2008 na kufunga magoli 91,
kutoa pasi za magoli 52 katika michezo 198 kwa sasa atakuwa balozi wa
dunia wa Barcelona.
Taarifa
zinaeleza kuwa sababu ya Barcelona kumtumia Ronaldinho kuwa balozi ni
kutokana na umaarufu alionao maeneo mbalimbali na lengo lao ni kukuza
jina la Barcelona zaidi ya ilivyo sasa ili kuiwezesha kufahamika zaidi
na hata kufungua milango mipya ya kibiashara.
Baada
ya kupewa nafasi hiyo Ronaldinho amepost picha katika ukurasa wake wa
Instagram akiwa nje ya uwanja wa Nou Camp unaotumiwa na Barcelona na
tayari amehudhuria uzinduzi wa ofisi za Barcelona za New York, Marekani.
No comments:
Post a Comment