21 October, 2016

Pete yangu siyo ya kishirikina - Young Killer

Msanii wa Hip Hop kutoka Mwanza Young Killer amesema pete yake aliyoivaa katika kidole chake ni urembo kama urembo mwingine kama miwani au hereni na siyo ya kishirikina au ya bahati kama watu wanavyoidhania.
Akiongea ndani ya Kipindi cha eNewz Msodoki amesema amekuwa ni mtu mwenye bahati kabla hata ya kuivaa pete hiyo au kuwa Young Killer hivyo pete hiyo haihusiki katika mafanikio yake “hofu ndo ugonjwa wako na kama mtu anafanya ushirikina ni imani yake imempelekea awe hivyo lakini kwa mimi sina imani na mambo ya kishirikina japokuwa najua kuwa yapo” alisema Msodoki.

Hata hivyo Msodoki alisema pamoja na mawazo ya watu kuhusisha pete yake na mambo ya kichawi lakini yeye hawezi kuivua itaendelea kukaa kidoleni kwake "... na kwa wale wanaoona tofauti waendelee tu kuwa na imani yao kwa kuwa ni vyema kutafuta haki yako bila kumkwaza mwenzako" alimalizia hivyo Young Killer

CHANZO: eatv.tv

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...