Jay Mo amwagia misifa Juma Nature

Msanii Jay Mo amesema ukongwe wa Juma Nature kwenye game ya bongo fleva ni kitu cha kuthaminiwa sana kwani ameleta mchango mkubwa kwenye muziki huo mpaka kufikia hapa ulipo.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jay Mo amesema wataendelea kumheshimu Juma Nature kwani vitu ambavyo amevifanya, ndivyo vimesababisha wasanii kama kina Diamond kujulikana kimataifa.
“Tutamkumbuka kwa kufanya vitu ambavyo vimewafanya mpaka kina Diamond wakajulikana, muziki anaoimba Juma Nature ni ule muziki wa watu wa chini, amegusa maisha ya watanzania halisi, unajua sisi hata kama tulikuwa tunafanya muziki lakini haikuwa kama ya Juma Nature, kipindi hicho unaenda kweny show ya Juma Nature unakuta watu wanapanga foleni ndefu kukata tiketi, alikuwa anaweka kiingilio cha chini ili kila mtu aweze kuingia, hajajichukulia mi super star na kuvaa ukinondoni au u ilala, muziki wake ulikuwa umelalia maisha ya mtaa na watu wengi, alikuwa mjanja kutarget hawa watu wenye uwezo wa chini kimaisha”, alisema Jay Mo.

Jay Mo amesema kutokana na aina hiyo ya muziki wa Juma Nature, ndiyo ume'inspire' vijana wengi na kufuata nyayo zake, ikiwemo yeye mwenyewe na kuandika mistari ya wimbo wa stori 3 na Jua na mvua.

CHANZO: eatv.tv

Comments

Popular posts from this blog

Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo

Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.