Michuano ya klabu bingwa ulaya
imeendelea kwa michezo nane kupigwa ambapo Arsenal waliiadhibu
Ludogorets Razgrad ya Bulgaria 6-0, wakati Mesut Ozil akipata hat trick.
Barcelona
nayo wakiwa nyumbani walimdhalilisha kocha wao wa zamani Pep Guardiola
kwa kumpa kichapo cha 4-0, Messi nae akipiga hat-trick, ambapo katika
mchezo huo ilishuhudiwa mlinzi wa Man city Claudio Bravo akilambwa kadi
nyekundu huku pia mlinzi wa Barcelona aliyeingia akitokea benchi Jeremy
Mathieu naye akizawadiwa kadi nyekundu.Makosa ya wazi ya mlinzi wa Celtic Kolo Toure yakaipa Borussia
Monchengladbach ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini, magoli yakifungwa
na Lars Stindl pamoja na Andre Hahn.Matokeo ya michezo mingine
Bayern Munich 4-1 PSV EindhovenParis Saint-Germain 3-0 Basel
Dynamo Kiev 0-2 Benfica
Napoli 2-3 Besiktas
FC Rostov 0-1 Atlético Madrid
No comments:
Post a Comment