20 October, 2016

Simba: Ushindi tu, sare hazikubaliki

Wakati leo inamenyana na Mbao FC ya Mwanza katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imesema inachokitaka kuanzia mechi zote sasa, ni ushindi tu na kwamba hata sare hazikubaliki tena.
 
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara, aliliambia Gazeti la Nipashe jana jijini Dar es Salaam kuwa, ingawa Mbao FC imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini hawataidharau.
 
 “Hatupaswi kubweteka kwa matokeo mazuri ya sasa, tunatakiwa tuendelee kufanya vizuri, tusipoteze hata pointi moja. Hatutaki hata sare, lazima tushinde kila mechi, ili tuendelee kuwaacha washindani wetu katika mbio za ubingwa (Azam na Yanga),”alisema. 
 
Hajji amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi leo Uwanja wa Uhuru kuisapoti timu yao ikimenyana na Mbao inayocheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu. 
 
 Simba ambayo imeweka kambi Hoteli ya Ndege Beach, Mbweni, Dar es Salaam, ikijifua Uwanja wa Boko Veterani, itaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar iliyoshinda mabao 2-0 Uwanja huo huo wa Uhuru. Wekundu wa Msimbazi hao wanaongoza Ligi Kuu wakiwa wamejikusanyia pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa, wakifuatiwa na Stand United ya
Shinyanga yenye pointi 20 za mechi 10, wakati mabingwa watetezi, Yanga wenye wakiwa na pointi 18 za mechi tisa.
 
CHANZO: Nipashe

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...