Akizungumza mjini Monaco wakati
wa kupanga makundi ya UEFA Champions League, amesema makubaliano kati
yao na Man City yanakaribia kukamilika. Amefafanua kuwa dili hilo
litakalovunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumuuza De Bruyne kwa kitita cha
pauni milioni 54 linaweza kukamilika ndani ya masaa 48 baada ya
makubaliano ya pande mbili kufikiwa.
Mgurugenzi huyo wa Wolfsburg amesema, ofa kutoka Man City imekuwa kubwa mno na wao hawawezi kupambana kuwazuia.
“Tumekuwa kwenye mazungumzo na
sasa tumekaribia kukamilisha lakini dili bado halijakamilika. Lakini
nadhani tutafikia muafaka muda si mrefu”.
Allofs amesema, timu yake haiwezi
kushindana na matajiri hao wa EPL ambao wameahidi kumpa De Bruyne
mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki kiungo huyo mwenye miaka 24.
No comments:
Post a Comment