28 August, 2015

MOURINHO ALAUMU MAREFA, AKATAA KUMZUNGUMZIA JOHN STONES

momo

Story hii inamuweka tena kwenye vyombo vya habari JM kwa kuendeleza tabia yake ya kulaumu watu kutokana na club yake kufanya vibaya.
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amewalaumu waamuzi kua ndio sababu ya timu yake kua na mwanzo mbaya wa ligi.Amewalaumu marefa kwa kitendo cha kuwapa red card wachezaji wake John Terry pamoja na kipa Thibaut Courtois na kuwazawadia penati West Bromwich na Swansea city.
Mourinho amesema “Kitu ambacho sio cha kawaida katika mwanzo wa msimu huu ni kua na mechi tatu alafu kati ya hizo mbili mnacheza watu kumi uwanjani na kupata adhabu ya penati mbili kutokana na maamuzi”
“Sio kitu tunachokitaka ila kua na point nne sio masihara, itabidi tusonge mbele,tujiimarishe.Tunajua tutaimarika na tutaimarika ili tupate matokeo mazuri zaidi”
Vile vile Mourinho amekataa kuzungumzia suala la mlinzi wa Everton John Stones kwa kusema anafuraha na kikosi alichonacho.
“Sipendi kuzungumzia wachezaji wa timu nyingine, nina furaha na kikosi chang ,kama tukipata mchezaji mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa ni vizuri kama tukikosa nitaendelea na kikosi nilichonacho” alisema Mourinho

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...