24 August, 2015

USAIN BOLT AWEKA REKODI MPYA BEIJING

Hatimaye binadamu mwenye kasi zaidi duniani hivi sasa mjamaica Usain Bolt amethibitisha uwezo wake baada ya kushinda ubingwa wa dunia wa riadha za mita 100 mjini Beijing, China.
bolt
Usain Bolt alitumia sekunde 9.79 kumshinda mwanariadha mwenye kashifa mbili za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu ‘doping’ aitwae Justin Gatlin ambaye wiki yote hii alikua akitajwa kama mpinzani wa kweli wa Bolt kutokana na kuwa na rekodi nzuri sana katika riadha.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Usain Bolt amekiri kuwa hiyo ilikua ni mechi ngumu kuwahi kukutana nayo lakini hakusita kusifia uwezo wake na ufalme wake katika riadha.
Aidha akizungumza kuhusu kashifa zinazochafua mchezo huo hivi sasa za matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu ‘doping’ Bolt ameuthibitishia ulimwengu kwamba mazoezi na kujituma ndio siri pekee ya kufanya vizuri na kwamba madawa hayana tija yeyote mbele ya kujituma mazoezini.
Wawili hao sasa watapambana tena katika mbio za mita 200 jumatano hii huku Bolt akisema pamoja na kujiandaa vya kutosha lakini anatarajia ushindani mkubwa kutoka kwa Gatlin aliyekuwa kifungoni kwa matumizi ya dawa tangu 2011.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...