23 August, 2015

KAMPUNI YA APPLE YAZINDUA APP MPYA YA MUZIKI

Kampuni ya Apple imetangaza kubuni programu tumizi mpya inayojumuisha maktaba ya kupeperusha muziki moja kwa moja kwenye internet, programu ya kusikiliza redio kwenye internet na njia maalum ambayo wasanii wataweza kubadilishana vibao vya miziki ambayo bado haijachapishwa rasmi.
App hiyo mpya inajumuisha mfumo wa kubashiri na kupendekeza utakaotumia mwelekezo wa binadamu kuchagua pamoja na sheria ya hisabati ya kutegua kitendawili kwa mifumo au algorithms.
150608221644_2
App hiyo mpya inalenga kuzipa upinzani Spotify, Tidal na app nyinginezo za muziki.
Kadhalika Apple imefichua kwamba Uingereza ndiyo itakayokuwa nchi ya kwanza kupata huduma ya kulipia ya Apple Pay nje ya Marekani. Watumiaji wa simu pamoja na vifaa vingine vya apple kupaa njia mpya ya kusikiliza muziki pamoja na redio.
” Watu wengi katika sekta hii wanachukulia kuzinduliwa kwa huduma hii ya muziki kama jambo kubwa, na matumaini yao ni kwamba hii itasaidia kubadili upokeaji wa huduma kwa usajili wa malipo kuwa bure,” amesema Chris Cooke, kutoka tovuti ya maswala ya muziki Complete Music Update.
“Lakini Spotify ina mbinu yenye matangazo ya kibiashara inayotolewa bure kuisadia kutangaza bidhaa zake jambo ambalo Apple haina.”
Huduma hii mpya ya Apple inazindua kituo cha radio cha Beats 1, mtangazaji katika kituo hicho ni aliyekuwa DJ wa BBC Zane Lowe miongoni mwa watangazaji wengine mashuhuri.
150608203311_apple_music_640x360_apple.com_nocredit
App hiyo vile vile ina uwezo wa kufanya kazi pamoja na programu tumizi ya Siri inayotoa msaada wa maelekezo kwa sauti na kuwawezesha watumiaji kuiamuru icheze wimbo kutoka sauti ya filamu au mwaka bila kuhitaji kujua jina la wimbo huo.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...