Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba mbele ya Libya baada ya kufungwa kwa goli 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kuelekea mechi yake dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kucheza mashindano ya Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka 2017 huko Gabon.
Mchezo huo uliochezwa nchini
Uturuki ambako Stars imeweka kambi, ulikuwa ni wa mazoezi na ulikuwa
hautambuliwi na CAF wala FIFA ila ulikuwa unatumiwa na makocha wa timu
zote mbili kwa ajili ya kutathmini vikosi vyao kuelekea michuano ya
kutafuta tiketi ya kushiriki michuano hiyo ya Afrika.
Kwenye mchezo huo, goli pekee la
Tanzania limefungwa na John Bocco ‘Adebayor’ kwa mkwaju wa penati baada
ya Simon Msuva kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari na mwamuzi
kuamuru ipigwe penati ndipo Bocco akaipatia Stars goli la kufutia
machozi.
Stars bado inaendelea na kambi
yake nchini humo ambapo ikirejea jijini Dar es Salaam itafanya
maandalizi kwa siku chache kabla ya kuivaa Nigeria Septemba 5 mwaka huu
kwenye uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment