Headlines za Chris Brown ni mpya kila siku mtu wangu… siku chache zilizopita Chris Brown alitangaza kuwa anaipa Album yake mpya jina la mwanae ‘ROYALTY’ ikiwa zawadi kwa mwanae ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa sana kubadilisha maisha yake.
Ninayo nyingine kutoka kwa C Breezy mtu wangu, nimepita kwenye page yake ya Instagram na nimekutana na video ya sekunde 15 ya wimbo wake mpya ‘Liquor’, wimbo ambao unapatikana kwenye album yake mpya tunayoisubiria.
Ukitembelea pia ukurasa wa Chris Brown wa Twitter utakutana na post nyingine kutoka kwake ikisema; “Coming soon. Directed by yours truly”… so good news kwa wewe shabiki wa Chris mtu wangu ni kwamba video wa wimbo huu mpya Chris anasimama pia kama Director!
Nimeisogeza kwako kipande cha video kutoka kwa Chris Brown niliyoweza kuinasa kupita ukurasa wake wa Instragram @chrisbrownofficial.
No comments:
Post a Comment