Aliyekuwa Askofu wa kanisa la
Katoliki kutoka Poland, ambaye alitarajiwa kufikishwa mahakamani kwa
madai ya dhuluma za ngono amefariki.
Jozef Wesolowski alipelekwa hospitali mwezi uliopita, saa chache tu kabla ya kufishwa mahakamani.Askofu huyo anatuhumiwa kuwapa watoto pesa na kuwadhulumu kingono wakati alikuwa balozi wa Vatican katika Jamuhuri ya Domincan.
Kamati maalum ya kanisa la Katoliki ilimpata na hatia na ikamsimamisha kazi mapema mwaka huu.
Wesolowski angelikuwa mtu wa kwanza wa ngazi ya juu katika kanisa hilo la Katoliki kufikisha mahakamani mjini The Vatican kwa madai ya kuwadhulumu watoto kingono.
BBC
No comments:
Post a Comment