Rais wa Ufaransa Francois Hollande
amatoa tuzo la juu zaidi nchini Ufaransa kwa Waamerika wanne ambao
walitibua shambulizi la kigaidi kwenye treni ya mwendo wa kasi kwenda
mjini Paris siku ya Jumamosi.
Mwanajeshi Mmarekani ambaye
alijeruhiwa Spencer Stone alipomuangusha mwanamgambo huyo sakafuni ,
alipewa tuzo hilo pamoja na Waamerika wengine na Muingereza mmoja ambao
wote wametajwa kuwa mashuja.Bwana Hollande alisema kuwa kungetokea maafa kwenye treni hiyo iwapo abiria hao hawangechukua hatua.
Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel na balozi wa Marekani nchini Ufaransa Jane Hartley walishudhuia sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment