28 August, 2015

Hii ndio kamati mpya yaShindano la Miss Tanzania, Jokate na yeye yupo


Kamati mpya ya Miss Tanzania imetangazwa Leo ikiwa ni wiki moja baada ya Baraza la sanaa la Taifa ( BASATA) kulifungua shindano hilo lililokua limefungiwa miaka miwili.
Jokate ambaye ndio msemaji wa kamati hiyo mpya amesema “Kwa niaba ya kamati mpya ya Miss Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya Lino International Agency Limited kwa kutuamini na kututeua kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Miss Tanzania yenye majukumu ya kuandaa, kuratibu ns kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania”
“Kwa leo hatutakuwa na mengi ya kusema kwa sababu ndio kwanza tumekabidhiwa jukumu hili hivyo kamati yetu itakutana kupanga mipango na mikakati endelevu ya kuendeleza sanaa hii ya urembo ndani hadi nje ya mipaka yetu  ya Tanzania” Aliongeza msemaji wa kamati hiyo.
Hii ndio orodha ya wajumbe wa kamati hiyo
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Wajumbe wa Sekretarieti :
1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

Source: Millardayo.com

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...