24 August, 2015

Manchester City ilipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini, Goodson Park dhidi ya wenyeji Everton

Ni ushindi wa Tatu mfululizo kwa kikosi cha Manuel Pellegrini na sasa wanashikilia kilele cha msimamo wakiwa na alama tisa. Mlinzi wa Kushoto, Alexandar Kolarov alifunga bao la kungoza dakika ya 60 kisha Samir Nasri akamaliza mechi dakika ya 88 kwa kuzamisha goli la ushindi.
City imeanza msimu tofauti na matarajio ya wengi, kasi yao ni ya kiwango cha timu inayohitaji hasa ubingwa. Walianza na ushindi mkubwa wa 3-0 ugenini The Hawthoms Stadium dhidi ya West Brom iliyo ‘ ienyesha’ Chelsea siku ya Jumapili. Kiungo na nguzo kuu ya timu hiyo, Mu-Ivory Coast, Yaya Toure ndiye mfungaji wa goli la kwanza la City msimu huu, ambalo alilifunga dakika ya 24’ kwa umbali wa ‘ yard 20’.
nasri
Nahodha, Vicent Kompany akafunga kwa mpira wa kona ya David Silva na kuwa mlinzi wa kwanza kufunga katika klabu hiyo msimu huu. Silva alifunga pia katika gemu hiyo ya kwanza na kuthibitisha uimara, kuanzia katika safu ya ulinzi ambayo iliweza kuwazima washambuaji Saido Berahino na Lickie Lambert.
Ilikuwa ni timu mpya tofauti na ile iliyomaliza katika nafasi ya Tatu msimu uliopita. Akiwa tayari amemsaini Muargentina, otamedi kutoka Valencia ya Hispania kama ingizo jipya katika safu ya ulinzi wa kati, Pellegrini ameshuhudia safu yake ya ulinzi ikicheza gemu Tatu mfululizo pasipo kuruhusu nyavu zao. Bacary Sagna tayari ameoneka ‘ ku-hodhi’ nafasi ya beki ‘ 2’ wakati Alexandar Kolarov akishika nafasi ya beki ‘ 3’.
Kompany na Eliaquim Mangala wamekuwa imara katika beki ya kati. Bado ‘ Wanne’ Hao wana safari ya kuthibisha ujio wa safu ya ulinzi ya City ambayo imetajwa mara kwa mara kama sababu ya kuanguka kwa timu hiyo anapokosekana, Kompany. Pellegrini sasa ana wigo mpana katika beki ya kati na ile ya pembeni. Gael Clichy, Martin Demichelis ni namba zaidi katika idara hiyo. Demichelis tayari amecheza kwa dakika kumi msimu huu ( aliingia kuchukua nafasi ya Yaya dakika ya 80 dhidi ya West Brom).
Silva, Yaya na kiungo Mbrazil, Fernandinho walianza katika idara ya kiungo katika mechi ya kwanza. Wilfried Bonny ambaye alishiriki katika utengenezaji wa goli la Yaya Toure, Raheem Sterling na Jesus Navas walianza katika safu ya mashambulizi. Sergio Aguero aliingia dakika ya 63 kuchukua nafasi ya Bony, Samir Nasri akaingia kuchukua nafasi ya Sterling dakika ya 74’.
Hiki ni kikosi kikubwa, kilikosa nguvu Fulani ya hamasa ya kuhitaji mafanikio zaidi msimu uliopita hasa baada ya kufeli katika malengoya kuingia miongoni wa klabu Nane Bora za ulaya. Asilimia kubwa ya wachezaji wa City ni wale walioshinda mataji mawili ya ligi kuu ndani ya misimu minne iliyopita hivyo suala la uzoefu wa kushinda kitu kigeni upande wao.
Mechi Tatu bila kuruhusu nyavu zao?
Ndiyo, City ilichapa Chelsea 3-0 katika gemu yao ya Pili nay a kwanza katika uwanja wa Etihad. Aguero ( mfungaji bora wa msimu uliopita) alifunga goli lake la kwanza msimu huu akiwa katikati ya mabeki wanne wa Chelsea, dakika ya 31’, Kompany akafunga tena kwa stahili ya kuunganisha mpira wa kona ya Silva kisha kiungo, Fernandinho akafunga goli maridadi la mpira wa kiki ya moja kwa moja na kuwamaliza mabingwa watetezi.
nasri 2
City ilitengeneza nafasi kumi ( 18) katika gemu na Chelsea ambao walimumudu kufanya hivyo mara Kumi ( 10). Dhidi ya West Brom walitengeneza nafasi 20. Nafasi ( 8) za hari walitengeneza dhidi ya Chelsea, na ( 7) dhidi ya West Brom siku ambayo walimiki mchezo kwa asilimia 69. West Brom walitengeneza jumla ya nafasi ( 9) na kumfanya kipa Joe Hart ‘ ku-save’ mara mbili.
Dhidi ya Chelsea, Hart ‘ ali-save’ mara tatu na timu ilizidiwa kwa asilimia moja katika umiliki wa mpira. Safu ile ile ya ulinzi iliyo anza dhidi ya West BroM, Chelsea ndiyo ilitumika katika gemu ya Tatu na Everton. Iliendeleza ubora wao, safari hii dhidi ya kina Arouna Kone na Romelu Lukaku. Chelsea ilikuwa na Eden Hazard, Diego Costa katika mashambulizi lakini walizimwa.
Silva, Yaya na Fernandinho wameanza pamoja katika gemu zote msimu huu na walikutana na wachezaji wa ‘ Kingereza’, Tom Cleverley, Gareth Barry, Ross Barkley na James McCarthy na kutengeneza mchezo moja ya michezo migumu katika wiki ya Tatu.
Aguero, Navas na Sterling walianza pamoja dhidi ya Chelsea, watatu hao walibanwa mno dhidi ya Everton lakini mlinzi wa kushoto, Kolarov dakika ya 60’ akiwa katika ‘ angle’. Nasri akafunga akiunganisha mpira wa faulo dakika ya 88’ na kukamilisha asilimia 100 ya ushindi.
Licha ya kutoruhusu nyavu zao safu ya ulinzi ya City tayari imefunga mara Tatu kati ya magoli Nane waliyokwisha funga hadi sasa. Kopany katupia kambani mara mbili wakati Kolarov amefanya hivyo mara moja.
Wachezaji waliotakiwa kubeba majukumu hayo kimsingi ( washambuaji) wamefunga mara moja tu ( Aguero) lakini bado timu imefanikiwa kupata alama Tisa katika gemu Tatu tena wakifunga mara Nane. Yaya, Silva, Nasri, Fernandinho, viungo hawa wanne kila mmoja afunga goli moja. Hii inaonesha kuwa wachezaji wa kila idara hawako tayari kupoteza gemu kwa sababu ya kutofunga magoli.
RAHEEM STERLING……
Usajili ghali hadi sasa msimu huu katika ligi ya England. Sterling ameanza vizuri katika timu hiyo huku kasi yake ikisaidia safu ya mashambulizi kutengeneza nafasi nyingi katika kila mchezo. City walitengeneza nafasi ( 16) huku ( 9) zikiwa za hatari katika gemu na Everton. Kama si uimara wa mlinda lango, Tim Howard ( ali-save mara 7) bila shaka City ingeibuka na ushindi mkubwa zaidi.
Everton walitengeneza nafasi ( 10) tu huku Moja pekee ikiokolewa na Hart haikuwa na kasi pindi walipokuwa na mpira na viungo wa kati walisumbuliwa na uwezo wa kukimbiza mpira wa Navas na Sterling katika wings. Kuwa na mchezaji kama Sterling kisha ndani yake una Navas na Silva ni ishara mbaya kwa timu nyingine.
Sterling anaifanya City itengeneze nafasi nyingi katika gemu zake licha ya kwamba hajafunga wala kupiga pasi ya mwisho mchezaji huyo wa England ameongeza kasi, nguvu na maarifa katika timu ya Pellegrini. Kilichobaki ni kusubiri nini ataendelea kufanya. Watacheza na Watford mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Ethad, kisha Cystal Palace ugenini, West Ham United nyumbani, Spurs ugenini……

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...