24 August, 2015

HIKI HAPA KIKOSI CHA STARS KILICHOENDA UTURUKI

Stars 1Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ tayari imeondoka kuelekea Uturuki ambako itaweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa Septemba 5 mwaka huu.
Kikosi cha Taifa Stars kilichosafiri kuelekea Uturuki kimejumuisha wachezaji wa Azam na Yanga waliokuwa wakisubiri kumalizika kwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ulipigwa siku ya Jumamosi na Yanga kuibuka kidedea kwa kutwaa ngao hiyo kwa mikwaju ya penati 8-7.
Hiki hapa kikosi kamili cha Stars kilichosafiri kuelekea Uturuki, Walinda mlango: Ali Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam FC ) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam FC ), Abdi Banda, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba), Juma Abduli, Mwinyi Haji Mngwali, Kelvin Yondani na Nadir Haroub (Yanga).
Viungo: Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo (Azam FC), Salum Telela, Deusi Kaseke (Yanga) na Said Ndemla (Simba).
Washambuliaji: John Bocco, Farid Musa (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Simon Msuva (Yanga), na Ibrahim Ajibu (Simba).
Kocha wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wakulipwa wa Tanzania wo watajiunga na Stars kulingna na kalenda ya FIFA pindi itakapohitaji wachezaji wa vilabu kwenda kuzitumikia timu zao za taifa.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...