28 August, 2015

Mshukiwa wa kike wa ugaidi asakwa-Kenya


Serikali ya Kenya imetoa zawadi ya $20,000 wa mtu yeyote atakaye toa habari za kukamatwa kwa mshukiwa mmoja wa ugaidi wa kike, Rukia Faraj.
Idara ya polisi imesema kuwa Rukia anasakwa kwa madai ya kuwasajili na kuwasafirisha watu wachanga kujiunga na mme wake nchini Somalia kwa mafunzo ya ugaidi na pia kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Mume wake Ramadhan Kufungwa pia anasakwa na polisi kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi nchini Kenya.
Rukia sasa anajumuika na washukiwa wengine ambao wanasakwa na serikali ya Kenya kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi.
Wengine ni pamoja na Mohammed Kuno anayejulikana kwa jina lingine Gamadere au Dhuliadein ambaye anatuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa, ambapo zaidi ya watu 148 waliuawa

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...