19 December, 2015

BAADA YA KUFUKUZWA MOURINHO, VAN GAAL AHOFIA KIBARUA CHAKE

Van Gaal +Mourinho
Baada ya kocha Jose Mourinho kutupiwa virago na klabu ya Chelsea, presha ni kubwa kwa kocha wa Manchester United Louis Van Gaal ambaye anasema anahofia kibarua chake na kwamba hajui kwamba inaweza kuwa ni zamu yake kuondoka kama hatopata matokeo haraka.
Van Gaal ambaye amesikitishwa kufukuzwa kazi kwa kocha wake huyo msaidizi wa zamani wakiwa wote Barcelona, na kusema hawezi kudadisi zaidi chanzo cha kufukuzwa kocha huyo aliyemzungumzia kuwa bora zaidi wa kizazi chake na mwenye rekodi ya kipekee.
Kocha huyo amesema anahofia kumalizia career yake ya ukocha kwa kufukuzwa na kwamba anahitaji kupata matokeo kuepusha hilo mara baada ya kuenda mechi tano bila ushindi huku wakifungwa na Vfl Wolfsburg na Bournemouth mfululizo.
Tayari wachambuzi wa soka duniani wanaona ni wakati Manchester United inatakiwa kuachana na Louis Van Gaal na badala yake kumnasa kocha Pep Guadiola ambaye anamaliza muda wake Bayern Munich ama Jose Mourinho ambaye ni chaguo la mashabiki, huku ikielezwa pia kuwa bado Van Gaal anapata sapoti kubwa kutoka katika bodi ya klabu hiyo.
Wakati huo huo, kocha Manuel Pellegrine wa Manchester City akizungumzia sakata hilo amesema kuwa yeye binafsi hawezi mkumbuka Jose Mourinho lakini akakiri kuwa ni pengo kubwa katika ligi kuu England kutokana na uwezo wa mreno huyo. Pellegrine akiendelea zaidi amesema katu hana presha yeyote ile pamoja na mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ya kumuhusu Gadiola kurithi mikoba yake msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...