Hoteli iliyoshambuliwa katika mji mkuu wa Mali, Bamako, mwezi jana itafunguliwa tena leo.
Watu
wenye silaha walishika mateka wageni 170 kwa saa tisa katika hoteli ya
Radisson Blu, na kuua watu 22 na kujeruhi wengine 14.Polisi na wanajeshi wa Mali, wakisaidiwa na vikosi vya usalama kutoka nje, waliingia kwenye hoteli hiyo na kuwaua washambuliaji.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kupitia Twitter kwamba hoteli hiyo itafunguliwa.
No comments:
Post a Comment