15 December, 2015
UNAJUA JULIO AMESEMA NINI KUHUSU UTEUZI WA NAPE NNAUYE? HAJAISHIA HAPO, KACHIMBA MKWARA WANAOMCHONGANISHA…
Siku chache mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR. John Pombe Magufuli kumteuwa Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wadau wa michezo wameendelea kumpongeza Nnauye kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kocha wa Mwadui FC ambaye timu yake itashuka uwanjani December 19 kuikabili Ndanda FC amesema amefurahishwa na uteuzi huo huku akisema sekta ya michezo imepata Waziri kijana.
Julio ameweka wazi story hiyo wakati akizungumza na kituo cha Radio One cha jijini Dar es Salaam kupitia kipindi chake cha michezo.
“Rais Magufuli kumteuwa Nape Nauye kuwa Waziri atakaeshughulikia michezo mimi ninaupongeza uteuzi huo, alichofanya ni sahihi, isipokuwa ninamasikitiko makubwa nimepata taarifa kwenye magazeti yameandika mimi nimesema Mh. Nape aanze na TFF ambayo inauozo kuna kuna watu wanamdanganya Malinzi. Habari hizi si za kweli mimi sikusema na sikutaka mtu anisemee, mimi nina akili timamu ninapotaka kusema langu hakuna mtanzania asiyejua kuwa Julio ni muwazi na anaweza kusema dakika yoyote”, alifunguka Julio.
“Nakumbuka kuna mwandishi aliniuliza kuhusu Nape, sasa atakapokuwa anasema kitu ambacho kitanigombanisha na kunichonganisha na watu wengine sipendi na nakemea kwa nguvu kubwa na waandishi wa aina hii nitawapeleka mahakamani haraka sana”.
Julio ametoa pongezi kwa Nape Nnauye juu ya uteuzi wake wa kuwa Waziri atakaeshughulikia pia masuala ya michezo lakini pia amesema hapendi kuchonganishwa wala kugombanishwa na watu.
Jumamosi ya December 12, Julio alikiongoza kikosi cha Mwadui kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa mji mmoja Stand United na kukisaidia kikosi chake kufikisha pointi 18 kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment