15 December, 2015

WACHEZAJI 6 WATARUDI KWENYE TIMU ZAO ZA ZAMANI KWENYE MICHEZO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE HATUA YA 16 BORA

zamani
Jumatatu December 14 draw ya UEFA Champions League hatua ya mtoano ilitangazwa. Ratiba hiyo imezua gumzo kubwa mitaani pamoja na kwenye mitandao ya kijamii huku michezo kadhaa ikipewa uzito wa juu. Michezo inayozikutanisha timu za Bayern Munich vs Juventus, Chelsea vs PSG, na Arsenal vs Barcelona inatazamwa kama ni fainali ambazo zitakuwa zikichezwa kwenye hatua ya mapema.
Michezo hiyo ya hatua ya 16 bora itaanza kuchezwa February 2016, kuelekea kwenye michezo hiyo mtandao huu umeangalia baadhi ya wachezaji ambao watakuwa wakirejea kwenye klabu zao za zamani ambazo waliwahi kuzitumikia katika nyakati tofauti.
6. Kingsley Coman-Bayern Munich
Arsenal's Mathieu Debuchy, left, holds Bayern's Kingsley Coman during the Champions League Group F soccer match between Bayern Munich and Arsenal FC in Munich, southern Germany, Wednesday, Nov. 4, 2015. (AP Photo/Matthias Schrader)
Bayern Munich itakutana na Juventus kwenye hatua ya mtoano, Kingsley Coman atakuwa mchezaji ambaye anakutana na klabu yake ya zamani. Kwasasa yupo kwa mkopo kwenye kikosi cha Bayern Munich akitokea Juventus. Amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu alipotua Bayern na kocha Pep Guardiola amekuwa akimuamini na kumpa nafasi ya kucheza.
5. Mario Mandzukic-Juventus
zamani 2
Striker wa Juventus Mario Mandzukic atakua akicheza dhidi ya klabu yake ya zamani Bayern Munich wakati klabu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora. Alitwaa taji la UEFA Champions League akiwa na The Bavarians alipokuwa akikitumikia kikosi hicho mwaka 2013.
4. Thomas Vermaelen-Barcelona
zamani 3
Beki wa Barcelona Thomas Vermaelen pia atakuwa akikutana na timu ya Arsenal, timu ambayo aliitumika miaka kadhaa iliyopita. Alijiunga na miamba ya Catalan majira ya kiangazi msimu wa mwaka 2014 na msimu uliopita ametwaa mataji matatu (treble) akiwa na kikosi hicho.
3. Aturo Vidal-Bayern Munich
zamani 4
Kiungo wa Bayern Munich Aturo Vidal atakuwa akicheza dhidi ya Juventus wakati klabu hizo mbili zitakapomenyana kwenye raundi ya 16 bora mwaka ujao. Vidal alikosa taji hilo wakati Juventus ilipopoteza mchezo wake wa fainali dhidi ya Barcelona mwezi May mwaka huu lakini wiki kadhaa baadaye akajiunga na wakali wa Allianz Arena.
2. David Luis-PSG
zamani 5
Mlinzi wa Paris Saint Germain David Luiz aliifunga timu yake ya zamani Chelsea na kuisaidia timu yake ya sasa kuitupa nje Chelsea kwenye michuano ya UEFA mapema mwaka huu lakini timu hizo zitakutana tena kwenye hatua ya 16 mwezi February mwaka ujao.
1. Alexis Sanchez-Arsenal
zamani 6
Star wa Arsenal Alexis Sanchez aliondoka Barcelona baada ya muda mwingi kuishia kukaa kwenye benchi. Kwasasa ni moja ya  wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Arsenal na anakutana na timu yake ya zamani ambayo haikuonesha kumuamini. Wakati huu Sanchez atapata nafasi ya kuwaonesha Barcelona kuwa walimwacha mchezaji bora timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...