
AY na Diamond hawajasema kitu. Lakini kampuni inayotengeneza video yake imeumwaga ubuyu kwenye Instagram. Kampuni hiyo iitwayo Studio Space Pictures ya Afrika Kusini, imeweka picha hiyo juu ya wakali hao na kuandika: Earlier today with @aytanzania @ @diamondplatnumz #ZigoRemix #studiospacepictures.”
Haijulikani kama ni Diamond pekee ndiye aliyemo kwenye remix hiyo lakini kuna uwezekano mkubwa wasanii wengine wakali kuipandia beat hiyo ya Nahreel.
Hii si mara ya kwanza Diamond na AY kukutana kwenye kazi ya pamoja. Diamond amewahi kuweka ladha kwenye wimbo wa AY ‘Asante.’
CV ya Studio Space Pictures si haba. Imefanya video kali zikiwemo Phumakim ya Casper Nyovest, Sim Dope ya AKA, Marry You ya Ice Prince, Easy to Love ya Bucie, Show ya Victoria Kimani na zingine.
No comments:
Post a Comment