15 December, 2015

MOURINHO ALIA KUSALITIWA

Mo 4
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amewatupia lawama wachezaji wake kwa kile anachosema anasalitiwa. Akiongea mara baada ya kupokea kichapo cha goli 2-1 toka kwa Leicester City jana usiku, kocha huyo anasema haelewi kitu gani kinawasumbua wachezaji wake hasa ikizingatiwa kuwa amekua akijitahidi sana kama mwalimu kuwaandaa lakini haoni hilo kwa wachezaji.
Mourinho anasema kuwa, alifanya kitu kikubwa sana msimu uliopita na kuwapandisha wachezaji katika viwango ambavyo wameshindwa kuvirudia tena msimu huu, na kwamba anaona kama anasalitiwa.
Kipigo hicho cha jana kimeifanya Chelsea wawe tayari wamepoteza michezo 9 ya ligi kuu hadi hivi sasa wakishika nafasi ya 16 na points zao 15 tofauti ya point moja tu na yule aliye katika mstari wa kushuka daraja.
Aidha Mourinho ameshangazwa na kitendo cha mchezaji wake Eden Hazard kuamua kujitoa mwenyewe uwanjani baada ya kugongana na mshambuliaji Jamie Vardy wa Leicester katika dakika ya 30, kitu kilichotafsiriwa kama uvivu na ukosefu wa uzalendo.
Lakini pamoja na matokeo hayo, kocha huyo wa Chelsea anasema hana wasiwasi na kibarua chake kwakua anaamini mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich hatomtimua na badala yake atamsapoti katika kuokoa jahazi la mabingwa hao watetezi.
Ushindi huo wa magoli 2-1 wa Leicester City yaliyopachikwa na washambuliaji wao hatari Jamie Vardy na Mahrez yameipandisha Leicester hadi nafasi ya kwanza na sasa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 35.
Angalia video Mourinho akiwachana wachezaji wake kwa kile anachokiita wanamsaliti.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...