Vilabu tofauti ulimwenguni ikiwemo Barcelona, ambapo kocha hugo alishinda mara mbili Champions League pamoja na makombe matatu ya La Liga, wapinzani wao Real Madrid nao pia wanaonekana kuvutiwa baada ya kuonekana wana nia ya kuachana na Rafa Benitiez.
Arsenal pia inaweza kuhusika ikiwa Guardiola ataamua kupumzika mpaka mkataba wa Wenger utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao.
Guardiola alitoboa siri kwenye kitabu chake “Pep Confidential” kwamba, baada ya kuondoka Barcelona na kabla hajaamua kujiunga na Bayern, alikuwa na nafasi ya kujiunga na City na Chelsea.
Manchester United pia walidhaniwa kwamba walikuwa wanamtaka Guardiola kabla ya kumuajiri Louis Van Gaal.
Sasa inaonekana United wanaweza kuachana LvG, na wanapewa nafasi ya kumtwaa Guardiola ambaye anatajwa kuvutiwa na utamaduni wa United hasa katika matumizi ya kutumia academy yao.
Kadri siku zinavyoenda ndivyo inavyoonekana ngumu kwa Van Gaal kuweza kumaliza misimu yake mitatu ya mkataba wake – mashabiki na inaripotiwa baadhi ya wachezaji wameanza kumpinga.
Lakini baadhi ya vyombo vya habari Uingereza vinaeleza kwamba Guardiola ataichagua United mbele City ikitokea United wakionyesha nia ya dhati ya kumhitaji.
Carlo Ancelotti anatajwa kwamba ndio mrithi wa Guardiola ndani ya Allianz Arena
No comments:
Post a Comment