Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi
maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Rais Magufuli amesema
hajaridhishwa "na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake
katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya
serikali katika bandari ya Dar es salaam.”Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Dkt Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Kwa mujibu wa Bw Sefue, Dkt Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa "utendaji kazi wa Takururu chini ya Dkt Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka”.
- Magufuli avunja bodi ya bandari Tanzania
- Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Hazina Kuu
- Magufuli aongoza Watanzania kufanya usafi
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, a libadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma.
Majuzi alivunja bodi inayosimamia bandari.
No comments:
Post a Comment