Mawasiliano muhimu sana mtu wangu, ndio
maana watu wengi wanaona umuhimu wa kuwa na smartphone ili mawasiliano
ya njia nyingi yaweze kumfikia.
Wataalam wa mambo wakaingia kazini na
kubuni kitu kinaitwa powerbank… ambayo kama smartphone yako ikiisha
chaji basi hiyo inakusaidia uendelee kubaki hewani, lakini
simu+powerbank ni sawa na mizigo miwili ya kubeba mkononi, usijali…
Wachina wanajali mahitaji yako.
Kwa sababu unahitaji kitu nafuu,
usipitwe na stori kwamba Wachina wameingia chimbo na kuja na mzigo wa
smartphone ambazo zinaweza kukaa chaji kwa siku 15, hesabu hiyo kwa
lugha nyingine ni kwamba inakaa na chaji kwa wiki mbili kamili !!
Simu yenyewe inaitwa Oukitel K10000 ambayo
Wachina wenyewe wamesogezewa tayari sokoni ndani ya nchi yao na pia
inapatikana Marekani kwa bei ya kama dola 239 ambazo kwa TZ inasomeka
kwa shilingi 515,000/=…. Kaa tayari mtu wa nguvu, mzigo unaweza kugusa
sokoni Afrika pia.
Unaweza kuiangalia simu yenyewe hapa, kama huna imani na vitu vya kichina cheki na hiki
No comments:
Post a Comment