Shirikisho la soka la Urusi
limethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha mkuu wa
timu ya Taifa ya nchi hiyo, Fabio Capello baada ya kushindwa kutimiza
malengo waliyojiwekea.
Katika taarifa yake, RFU
wamemshukuru Capello kwa kazi yake aliyofanya na wamemtakia kila la
kheri katika maisha yake yajayo, huku naye akilishukuru Shirikisho hilo,
mashabiki pamoja na wachezaji kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika
kipindi chote alichofundisha timu hiyo.
Mkataba wa Capello unatakiwa
kumalizika mwaka 2018 ambapo Urusi itahodhi kombe la Dunia, lakini
maamuzi yaliyochukuliwa yanalifanya Shirikisho hilo limlipe fidia ya
paundi milioni 11.
Ripoti kutoka Urusi zinasema
kwamba, kocha wa CSKA Moscow, Leonid Slutsky anapewa nafasi kubwa ya
kurithi mikoba ya Capello mwenye umri wa miaka 67 ambaye amekinoa
kikosi cha Urusi kwai kwa miaka mitatu.
Capello alianza kuifundisha Urusi
mwaka 2012, muda mfupi baada ya kujiuzulu kuifundisha timu ya Taifa ya
England, lakini alishindwa kuwaongoza vizuri Warusi katika fainali za
kombe la Dunia mwaka jana nchini Brazil na mwaka huu nchi hiyo imefanya
vibaya katika mechi za kufuzu kombe la Mataifa ya Ulaya 2016.
Urusi inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi G ambapo imeshinda mechi mbili tu kati ya sita ilizocheza.
No comments:
Post a Comment