14 July, 2015

Saa 72 za Lulu Ndani Ya Gold Digger Ni Hatari

Saa 72 za Lulu Ndani Ya Gold Digger Ni Hatari


UNAPOONGELEA Muigizaji wa kike mwenye mvuto na anayejua kuigiza basi msanii huyo si mwingine unamuongelea binti mwenye nyota kali Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu, baada ya kimya cha muda mrefu kuwepo likizo Lulu kwa karudi kwa nguvu kubwa katika sinema.

Nakutonya ni zaidi ya saa 72 Lulu anasimama kuigiza huku wasanii anaoshiriki nao wakibadilishana naye akibadilisha nguo tu na kurudi katika scene nyingine baada ya kumaliza scene moja baada ya moja, bila kupumzika hata akiambiwa sasa unaweza kupumzika anasema kuwa tumalizie hiyo ya moja.

Muongozaji wa sinema hiyo Karabani anasema kuwa Lulu ni msanii wa kipekee kwani kwanza hakosei kuongea wala kuigiza nje ya script ni msanii wa kipekee Karabani anasema kuwa katika aliofanya nao kazi toka Ulaya huyu ni wa aina yake.
Baba James mmoja ya wasanii anashiriki naye katika sinema ya Gold Digger anasema Lulu yupo katika viwango vya kimataifa anajua kuigiza na anabadilika kulingana na tukio tofauti na wale wasanii wanaobebwa na wasanii wengine au script.
“Lulu ni msanii hatari sana unapocheza naye jipange na kama haujui ni utajua kwanza hana makuzi kazini yeye ni mtu wa utani lakini baada ya kazi na hawezi kuacha scene eti njaa hiyo kwake hakuna,”anasema Baba James.
Msanii huyo anasema kuwa katika filamu ya Gold Digger kulikuwa na ushindani mkubwa sana wasanii kuonyeshana uwezo, wasanii kama Dude, Isarito, Baba James, Kojack na wasanii wengine zaidi ya 200 kuifanya sinema hiyo kuwa ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...