Mahali pekee utakapopata habari za Burudani,Michezo,Urembo udaku na Kuelimika
14 July, 2015
Lil Wayne karushiwa chupa na Birdman night club akashtukia.. tukio lilirekodiwa kwenye hii video.
Kwa muda mrefu sasa hivi kumekuwepo na beef kati ya rapper Lil Wayne
na Birdman wa Cash money na hii ni baada ya Wayne kujitoa Cash Money kwa
kutoridhishwa na ishu kadhaa ikiwemo kutosikilizwa anachotaka hasa
kwenye ishu ya album yake kucheleweshwa kutoka.
Picha za tukio lenyewe, Lil Wayne akishangaa kurushiwa chupa alafu kwenye hii ya kulia ndio birdman anaonekana na timu yake.
Baada ya kujitoa Cash Money,
Wayne ameendelea na show zake kama kawaida ambapo weekend iliyopita
alikuwepo Miami Marekani kwenye club moja ya usiku ambapo kumbe na
‘mbaya wake’ Birdman nae alikuwepo tena akimtazama Lil Wayne kwa chini wakati akiperform.
Inadaiwa Birdman alirusha kwa Lil Wayne
chupa ya kinywaji alichokua anakunywa na kusababisha show kusimama kwa
sekunde chache huku watu wakijiuliza chupa imetoka wapi lakini badae
ndio ikaja kujulikana kwamba Birdman ndio aliirusha.
Hivi vipisi vya video vinaonyesha hiyo moment kwenye hili tukio.
No comments:
Post a Comment