16 July, 2015

Victor Valdes na Kocha Louis Van Gaal hakuna amani


Ndani ya masaa 72 tu mahusiano mazuri kati ya golikipa wa Manchester United Victor Valdes na kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal yamevunjika, tofauti kati yao ilianza wakati Valdes alipogoma kucheza kikosi cha wachezaji wa akiba.
Maswali yalianza kutawala baada ya Valdes kuenguliwa na David de Gea kujumuishwa kikosini licha ya kuhusishwa pia na story kwamba ana mpango wa kuihama klabu hiyo, katika kikosi kilichosafiri na timu kwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya.
Valdes ameachwa na timu na wengi walianza kudhani labda kaachwa sababu ya majeruhi kabla ya Van Gaal kufichua ukweli katika kikao na waandish wa habari jumatano hii Marekani.
Lakini sasa majibu kamili ya nini kimetokea kati ya wawili hao kimejulikana, Van Gaal amemuacha Valdes kwa sababu hataki kufuata falsafa zake hivyo ni mtovu wa nidhamu na hana nafasi katika kikosi chake.
“hafuati falsafa zangu, hivyo hakuna nafasi ya mtu kama huyo”>>> Van Gaal
Van Gaal anamtuhumu Valdes kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kucheza mechi na kikosi cha wachezaji wa akiba akiba msimu uliopita. Kufuatia mvutano huo Valdes kuna uwezekano mkubwa wa kutoendelea kuvaa jezi ya Manchester United msimu ujao.
Valdes alijiunga na Man United january 2015 kama mchezaji huru akiwa amemaliza mkataba wake na klabu  ya FC Barcelona.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...