18 July, 2015

MAKALA : MUZIKI WETU BONGO.

Katika maisha ya kawaida Muziki umekua sehemu kubwa mno kutokana na kwamba muziki ni njia mojawapo inayotumika katika maswala ya uelimishaji, burudani, na hata uamasishaji katika jamii zetu.
Leo nimemona niandike makala hii na ikufikie wewe msomaji wangu na makala hii inauzungumzia MUZIKI WETU HAPA BONGO.

    Miaka ya nyuma kuanzia miaka ya 2000 hadi 2005 na 2006 muziki wetu wabongo(BONGO FLEVA) ulianza kuonekana ukilipa na kukua kwa kasi kiasi ambacho liliongezeka kundi kubwa la wasanii wa muziki huo wengi wao wakiufanya muziki huo kwa makundi au kama msanii mojamoja yaani SOLO ARTIST.

Image result for wakali kwanza
MAKAMUA NA Q JAY
Yalikuwapo makundi makubwa kama vile TMK WANAUME, ambao kwa sasa kundi hilo limevunjikia mbali, WAKALI KWANZA, ambao nao hatufaham walipotelea wapi, EAST COST TEAM, kundi ambalo lilisheheni wakali kama vile AY, KING CRAIZY GK, FA na wakali kibao ambao nao hatufahamu walipoishia. 

     Hayo ni baadhi ya makundi makubwa yaliyotikasa mno katika muziki huu wa BONGO FLEVA, Kuna wasanii waliotisha mika hiyo na hadi leo wengi wetu hatufahamu walipo na wanafanya nini kwa sasa baadhi yao tumekuwa tukiwaona katika mitandao yetu yakijamii na mara tuu wanapo ulizwa VIPI MBONA HATUKUONI KATIKA GAME  TENA? majibu ya swali hili Kutoka kwa wana WAPOTEVU hawa ni majibu yanayo tukosesha raha au kutufanya sisi kuwaona kama wamepoteza moja kwa moja VIPAJI vyao HADIMU ambovyo sisi wadau tume vikosa kwa muda mrefu, moja ya majibu wanayo tupatia ni NAJIANDAA NA PROJECT MPYA SO MASHABIKI WANGU MKAE TAYARI KWA UJIO WANGU MPYA, Mimi nadhani huambizana kwa maana kila msinii kati yao anapohojiwa mahali popote kwa muda tofauti huja na jibu moja.

   Tuyaache hayo ya WANA WAPOTEVU hawa, kazi yetu sisi ni kuwangoja kwa hamu na shauku kubwa na tuje kwenye swala letu moja kwa moja.

             Ni kwa nini Muziki wetu hautambuliki kimataifa?
Kila mmoja wetu hujiuliza swali hili na ni matumaini yangu yakwamba swali hili huleta shida na utata katika upatikanaji wa majibu yake.

   Jibu ni kwamba muziki wetu ni uleeee waku kopi na kupest, na hii inaonekana wazi kwa kila mmoja wetu hapa BONGO. Kuanzia utayarishaji hadi usambazaji wake umekua ni wakuiga tuu na sio tulio buni sisi. Tujiulize ni kwa nini wenzetu UGANDA muziki wao una kua kila siku na wanapata kujulikana Karibu ulimwengu mzima ilhali nchi yao kiuchumi bado ipo chini? Je wao ni bora kuliko sisi? laa hasha, ni Aina pekee waliyo ibuni na kuitumia wao kama wao na hadi leo hii wana wika. Huu ni ukweli na wa weza bisha lakini kiuhalisia ndivyo mambo yalivyo.

  Leo hii huwezi kumlinganisha mwana muziki wa Bongo na wa UG, kiuchumi na hata kimuziki kwani wenzetu wanajua wanacho kifanya katika game ya muziki hasa katika kanda hii ya Afrika Mashariki.

  Wabongo tumekuwa tuki iga na wala  sio kubuni kilicho chetu. Mfano mzuri na kwamba Kipindi Suma lee  aliporudi katika game baada yakipindi kirefu kukaa kimya alikuja na Ngoma ya HAKUNAGA ngoma yenye mahadhi ya KWAITO na alitisha sana katika vituo mbali mbali vya redio na TV za hapa BONGO na katika kumbi mbali mbali za starehe

 Chakushangaza baada ya muda mfupi watu waliiga staili ile ya KWAITO jambo ambalo kila mwana muziki alijaribu kufanya KWAITO. Wazi mpaka hapo? Tukumbuke yakwamba KWAITO sio MUZIKI WETU  huu ni muziki wa AFRICA KUSINI kuleee kwa mzee madiba.
    
Mziki wetu Sasa umehamia Nigeria?
Ni ukweli usio pingika yakwamba wasanii wetu wa hapa nyumbani wamekua wakiiga muziki wa NIGERIA ambao kwa sasa watoto wa uswahilini wanasema ni HABARI YA MJINI. Utaskia ngoma ya hapa nyumbani na utashindwa kutofautisha Kati yao na sisi WABONGO.

  Huku ni kuwatukuza Na kuwapa wenzetu MAUJIKO na kwa hakika kwa halii hii tuta fail kama tunavyozidi kufail kwenye nyanja nyingine za kimaendeleo hapa kwetu.

Tuu ache UJINGA HUU na tutengeneze kile kilicho chetu na tukifanye kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote na Mabadiliko haya yaanzie Huko kwa MAPRODUCER hadi WASANII.
 Wenye misemo yoa walisema "MTAKA CHA UVUNGUNI SHARTI AINAME" na "NGUO YAKUAZIMA HASITIRI MAUMBILE"

Je Diamondi ndio msanii mwakilishi wa Tanzania Kimataifa?
Siwezi sema moja kwa moja NDIO kwani mimi binafsi Bado naona wapo wasanii kibao na MALEGENDARY wanaofanya vizuri Kimataifa akiwepo AY na wenzake ambao walianza Kuitambulisha Tanzania kimataifa hata kapla ya DIAMOND kujulikana

   Ni kwamba mwenzetu Kaokota DODO chini ya MUAROBAINI. Ni jambo la faraja kuona kijana wetu anafanya poa nyumbani na ugenini na hii inatokana na Jitihada anazozifanya ili azidi kung'ara mthili ya nyota angani.
  
Tufanye nini ili na sisi tutoke?
     Hapa ndo penyewe. Chakufanya ni kila msanii kujituma na kuacha kukopi vya watu, ebu kila msanii ajaribu kutoka kwa staili ya kipekee kama wenzetu wanavyofanya. Na sisi WADAU tuache ushabiki usio na tija na tuungane kuwapa shime vijana wetu kwani mziki NI BIASHARA na wengi wetu ndipo FARAJA ZETU HUPATIKANA.Niliyo yasema ni machache mno hayo ni baadhi tuu yapo mengi yanayo husu muziki wetu hapa BONGO.


 Kipekee nipende kukushukuru wewe uliechukua mda wako wa thamani kusoma makala hii na ni imani yangu umepata picha angalau wapi muziki wetu unapokwenda. kwa maoni au ushauri tafadhali wasiliana nami kupitia namba 0767322193 au tembelea ukrasa wangu wa facebook MAWERE MTOKA MBALI na twitter @mawere3.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...