Meneja wa
Manchester United, Louis van Gaal amethibitisha kwamba bado anahitaji
kusajili wachezaji wawili majira haya ya kiangazi licha ya ukweli kuwa
ameshanasa saini ya wachezaji wanne mpaka sasa.
Van Gaal ametumia paundi
milioni 80 kumsajili winga wa PSV Eindhoven, Memphis Depay, beki wa
kulia wa Torino, Matteo Darmian na viungo Bastian Schweinsteiger kutoka
Bayern na Morgan Schneiderlin Southampton.
Mholanzi huyo ameiambia MUTV kuwa bado ana mapengo mawili katika kikosi chake.
“Hapana, hatujamaliza usajili”.
Amesema Van Gaal na kuongeza: ” Tutanunua mchezaji ambaye anaweza
kuleta mchango, nadhani bado tunahitaji kuongeza wachezaji wawili katika
sehemu mbili na tutafanya hivyo pale inapowezekana”.
Van Gaal pia anamuwinda mlinzi
wa kati Sergio Ramos, lakini dau la paundi milioni 40 alilotuma Real
Madrid limekataliwa mara kadhaa, wakati huo inaelezwa kwamba Man United
wanataka kumuuza Jonny Evans.
Van Gaal amesema kwamba Javier Hernandez “Chicharito” atakuwa sehemu ya kikosi chake.
No comments:
Post a Comment